SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limesema kuwa tukio lililotokea Novemba 3,2024 ambalo lilisababisha treni ya mchongoko (EMU) kusimama kwa takribani saa sita ni hujuma zilizohusisha kukatika ama kukatwa kwa nyaya (catenary) zinazochukua umeme kutoka njia ya umeme kupeleka kwenye treni.
Taarifa iliyotolewa leo Novemba 06,2024 na Mkuu wa Kitemgo cha Uhusiano TRC,Fredy Mwanjala imesema taarifa zilizosambaa kuwa treni hiyo ilizimika kutokana na changamoto za umeme si kweli kwakuwa hakuna treni ya mchongoko iliyopata hitilafu ya kiufundi.
“Tayari baadhi ya wahusika wamekamatwa na hatua stahiki dhidi yao zimeshaanza kuchukuliwa ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo husika,tunawashukuru wenzetu wa TANESCO kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa,shirika linauhakikishia umma kuwa hakuna treni iliyopata hitilafu ya kiufundi,”amesema Mwanjala.
Amesema TRC imeutaka umma kupuuza taarifa potofu zinazosambazwa na watu mbalimbali na kwamba ukweli ni kuwa tangu kuanza kwa safari ya kwanza ya treni zinazotumia nishati ya umeme Juni 14, 2024 hakujawahi kuwa na changamoto ya umeme.
“Shirika linawakumbusha wananchi kuwa bado tuko kwenye kipindi cha mwaka mmoja cha matazamio, na kama changomoto zozote zinajitokeza, TRC itaujulisha umma kwa uwazi kama siku zote tunavyofanya, na taarifa rasm mtazipata kwenye vyanzo vyetu rasmi na si vinginevyo.,”amesema Mwanjala.
WATU WENYE ULEMAVU WAMEPATA UFADHILI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA KATIKA MASWALA YA UONGOZI NA KUKUZA DEMOKRASIA.
SERIKALI YA SAMIA KUZALISHA AJIRA MPYA MILIONI 1.2 KILA MWAKA
RAIS SAMIA APELEKA KICHEKO KWA WANANCHI WA SONGWE
UZINDUZI WA TEKNOLOJIA MPYA YA UREKEBISHAJI NA UTUNZAJI WA MAGARI KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI.
SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE
CCM YASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.
RC.CHALAMILA AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KUPIGA KURA NOVEMBA 27.
THE WHEEL YALETA MAPINDUZI KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI NCHINI.
DCEA YAZIDI KUVUNJA MTANDAO WA DAWA ZA KULEVYA NCHINI.
TANZANIA MWENYEJI MKUTANO WA 7 WA KIMATAIFA WA JUMUIYA YA MAMLAKA YA USIMAMIZI YA USAFIRI MAJINI.