Sera mpya ya Elimu na Mafunzo nchini, imeshaanza kutekelezwa nchini, kutokana na kufanyiwa kwa marekebisho kwa sera ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023.
Sera hiyo ilivyotoka ilisababisha mtaala kubadilishwa kuanzia ngazi za chini hadi vyuo na hivi sasa Taasisi za elimu ya juu nazo kuendana na Sera za elimu nchini.
Laurence Msofe ambaye ni Mkurugenzi wa elimu ya juu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema hayo wakati alipokuwa mgeni Rasmi kwenye kongamano la mradi wa mabadiliko katika ufundishaji wa wataalamu wa Afya.
Msofe amebainisha kuwa, mradi huo umeendeshwa kwa miaka 6 na unahusisha Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), lakini pia Chuo cha KUHAS, KCMS pamoja na vyuo viwili kutoka nje ya nchi ikiwa ni pamoja na Chuo cha DUKES na Chuo cha St. Francisco University of California Marekani.
"Maengo ya huu mradi ni kufanya mapitio makubwa katika namna ya kufundisha wataalamu wa Afya na kwajili ya kupata wataalamu wa Afya ambao wana ujuzi lakini pia wana uwezo wa kutenda kazi zao kwa umahiri mkubwa," ameeleza Msofe na kuongeza,
"Mradi huu umefanikiwa kutengeneza mitaala ya mfano katika mafunzo ya udaktari, lakini pia mafunzo ya uuguzi na ni mitaala ambayo imeshapitishwa na Taasisi yetu ya tume ya vyuo vikuu Tanzania na tunatarajia kwamba itatumika sasa sio tu kwa vyuo hivyo ambavyo nimevitaja lakini pia kwa vyuo vingine hapa Tanzania."
Katika Mradi huo ambao umefadhiliwa umelenga kuangalia ameongeza namna ya kupata tofauti ya ufundishaji katika masomo hayo ya tiba hasa kwa udaktari na uuguzi.
Naye Prof. Gideon Kwesigabo mratibu wa mradi huo amesema katika utekelezaji wake wamefuata njia tatu ambazo ni kubadilisha mtaala, kuongeza uwezo wa walimu kufundisha pamoja na kuhusisha wadau kuhakikisha kwamba wanashiriki katika mradi huo.
Aidha amesema kuwa kwa sasa wanashirikiana na wahitimu mbalimbali kutoka katika vyuo ili waweze kusaidia katika kuboresha mfumo wa elimu katika ngazi ya vyuo nchini.
Kwa upande wake Prof. Appolinary Kamuhabwa Makamu Mkuu MUHAS amesema malengo ya mradi ni kuangalia namna bora ya ufundishaji unaofanyika lakini pia namna wanavyowataini wataalamu wa afya na vitu gani wanatakiwa kuvijua kulingana na mazingira ya Tanzania na ulimwenguni, hivyo mradi umewasaidia kuweza kutekeleza mitaala pamoja na wataalamu wa kufundisha.
"Huu mradi tunaona kwa kiasi kikubwa unaenda kuinua ubora wa mafunzo ya afya kwa elimu ya juu hapa nchini na tunaishukuru Wizara ya elimu kwa kulipokea vizuri na baada ya kongamano hili tutawasilisha mapendekezo" Amesisitiza
WATU WENYE ULEMAVU WAMEPATA UFADHILI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA KATIKA MASWALA YA UONGOZI NA KUKUZA DEMOKRASIA.
SERIKALI YA SAMIA KUZALISHA AJIRA MPYA MILIONI 1.2 KILA MWAKA
RAIS SAMIA APELEKA KICHEKO KWA WANANCHI WA SONGWE
UZINDUZI WA TEKNOLOJIA MPYA YA UREKEBISHAJI NA UTUNZAJI WA MAGARI KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI.
SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE
CCM YASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.
THE WHEEL YALETA MAPINDUZI KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI NCHINI.
ARUSHA NA KILIMANJARO KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA DESEMBA
SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE
WATU WENYE ULEMAVU WAMEPATA UFADHILI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA KATIKA MASWALA YA UONGOZI NA KUKUZA DEMOKRASIA.