“Leo tumekusanyika hapa kuwasilisha zabuni ya pamoja yaani, “The East Afrca Pamoja Bid” kwaajili ya kuwa wenyeji wa mashindano ya Afcon mwaka 2027, dhana hii ya zabuni yetu yaani Pamoja inaa maana ya ‘umoja’ kwa lugha ya Kiswahili ambayo inaunganisha maono yetu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuileta pamoja Afrika kupitia nguvu ya mpira wa miguu.”
Ni sehemu ya maneno yaliyowasilishwa na kamati maalumu ya kuandaa zabuni kwaajili ya Mashindano ya Afcon 2027 kwa nchi za Tanzania, Kenya na Uganda huku sababu mbalimbali ziliwasilishwa, kwanini nchi hizo ziandae mashindano hayo makubwa barani Afrika.
Sababu nyingi zilitajwa ikiwemo kuwepo kwa miundombinu bora iliyokamilika na ile inayoendelea kujengwa, kuwepo kwa amani, historia ya mataifa hayo mwanachama wa Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) kutokuandaa mashindano hayo hata mara moja tangu kuanzishwa kwake, lakini pia utalii ni sehemu ya mambo muhimu yaliyopewa kipaumbele katika uwasilishaji.
Ikumbukwe kuwa Afrika Mashariki ni sehemu salama kwa utalii duniani (world tourism destinations) huku pia majarida pamoja na mashirika mbalimbali ya waongoza watalii yaikitajwa kuwa sehemu ya ndoto ya kila mtu kutembelea, ikiwa imesheheni vivutio vingi vya utalii ikiwemo mandhari nzuri za asili, maziwa na maporomoko ya maji, mbuga na hifadhi mbalimbali za wanyamapori.
Vivutio hivyo ni kama Ngorongoro, Serengeti National Park, Mlima Kilimanjaro, Maasai Mara National Park, visiwa vya Unguja na Pemba (Zanzibar) ambavyo vimekuwa vikishinda tuzo mbalimbali za kimataifa katika sekta ya utalii.
Maandalizi ya afcon 2027 hayajaicha sekta ya utalii nyuma wakati ambapo kila nchi ikijitahidi kuhakikisha inaweka mazingira mazuri ya kufanyika kwa mashindano hayo kwa mara ya kwanza katika ukanda huu, sekta ya utalii imeendelea kuwekewa miundombinu mizuri tayari kupokea wageni watakaojitokeza kushuhudia michezo itakayochukua nafasi katika viwanja mbalimbali.
Hifadhi ya Makuyuni Wildlife Park ambayo ni moja ya vivutio vya utalii Ukanda wa Kaskazini ambayo inatarajia kuchangamkia fursa ya kuwepo kwa mashindano hayo, imeanza kufanyiwa matengenezo makubwa ikiwemo ujenzi wa barabara ndani ya hifadhi hiyo, ujenzi wa bwawa la kuhifadhi maji wakati wa kiangazi.
Hifadhi hiyo iliyopo ndani ya mfumo wa Ikolojia wa Tarangire-Manyara, ina ukubwa wa kilomita za mraba 49 na iko umbali wa kilomita 70 kwa mwendo wa gari kutoka Jiji la Arusha katika makutano ya barabara kuu ya Arusha-Babati, Makuyuni-Karatu, imesheheni wanyamapori ikiwemo tembo, twiga, nyati, nyumbu, kudu, mbwa mwitu, simba, pundamilia na impala inatarajiwa kuboreshwa zaidi kwaajili ya kuvutia watalii wa ndani na nje ya nchi.
Dkt. Simon Mduma ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) amesema katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi na uimarishaji wa miundombinu kwenye hifadhi hiyo iliyofanyika Novemba 24, 2025, miradi ambayo ni wezeshi kwaajili ya utalii itakamilika kwa wakati na itasaidia kuinua maendeleo ya utalii na kuongeza mapato ya serikali kupitia shughuli za kitalii.
“Tumekuja tukiwa na malengo matatu katika kukagua miradi ya maendeleo katika eneo hili, kukagua ujenzi wa barabara, kazi hiyo tumeifanya tumzenguka na tumeona maendeleo ya ujenzi wa barabara ni kazi ambayo inaridhisha ni nzuri, shughuli ya pili ilikuwa ni kwenda kukagua eneo ambalo litajenga bwawa la kukusanya maji, tumezunguka na tumeona eneo lenyewe linaridhisha na hiyo kazi itaanza muda mfupi tu ujao mikataba imeshainiwa tayari kwa kuanza kazi hiyo.” Alieleza Dkt. Mduma.
Dkt. Mduma amesema kuwa eneo hilo limekuwa tatizo la upungufu wa maji kipindi cha kiangazi jambo ambalo limekuwa likisababisha ukame na kuwafanya wanyama kutoka ndani ya hifadhi na kusababisha migogoro kati ya wanyama hao na wananchi, hivyo kuchimbwa kwa bwawa hilo kutasaidia kuondoa changamoto hiyo, huku pia akitaja uondoaji wa miti ambayo haiendani na uhifadhi ni malengo ya tatu ambayo TAWA wanayasimamia katika hifadhi hiyo.
“Kwahiyo kama bodi ya mamlaka hiyo tumeridhika na kazi zote ambazo zilikuwa zimeelekezwa kazi ambazo zimekamilika na nyingine ambazo bado zinaendelea kufanyiwa kazi imekuwa ni mafanikio makubwa sana.” Amefafanua Dkt. Mduma.
Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, ambaye pia ni Kaimu Kamanda wa Uhifadhi Kanda ya Kaskazini ya TAWA, Privatus Kasisi, amesema kuwa maboresho yanayoendelea katika hifadhi hiyo yanalenga mashindano ya Afcon 2027 yanayotarajiwa kuleta wageni kutoka mataifa mbalimbali kuja kushuhudia mashindano hayo.
“Sisi tunakimbizana na muda kwasababu hili eneo tunaamini kabisa kutokana na ukaribu wake kutoka Arusha, linaweza kuwa kivutio kikubwa sana na malengo yetu makubwa ni Mashindano ya Afcon ya 2027 tukiamini kabisa nchi itapokea wageni wengi na Arusha ni moja ya miji itakayapokea wageni wengi na kuna kiwanja kwaajili ya mashindano hayo, kwahiyo uwepo wa hifadhi ya Makuyuni Wildlife Park karibu na Arusha tunaamini kama tutaiboresha vizuri na kuiendeleza basi ikifika kipindi hicho tutapokea wageni wengi na kuingiza mapato ya kutosha.” Amefafanua Kamishna Msaidizi Kasisi.
Hifadhi hiyo imeanzishwa, mwaka jana baada ya serikali kuyatwaa mashamba matatu makubwa, maarufu kama mashamba ya ‘STAIN’ yaliyokuwa yakimilikiwa na mwekezaji raia wa kigeni katika Wilaya ya Monduli.
Mashamba hayo ni Amani lenye ekari 9,007, Lente ekari 3,344 na Loldebes ekari 2,812, ambayo kwa sasa yanatumika kama eneo maalum la kuendeleza shughuli za uhifadhi na utalii.
WATU WENYE ULEMAVU WAMEPATA UFADHILI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA KATIKA MASWALA YA UONGOZI NA KUKUZA DEMOKRASIA.
SERIKALI YA SAMIA KUZALISHA AJIRA MPYA MILIONI 1.2 KILA MWAKA
RAIS SAMIA APELEKA KICHEKO KWA WANANCHI WA SONGWE
UZINDUZI WA TEKNOLOJIA MPYA YA UREKEBISHAJI NA UTUNZAJI WA MAGARI KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI.
SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE
CCM YASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.
THE WHEEL YALETA MAPINDUZI KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI NCHINI.
SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE
ARUSHA NA KILIMANJARO KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA DESEMBA
WATU WENYE ULEMAVU WAMEPATA UFADHILI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA KATIKA MASWALA YA UONGOZI NA KUKUZA DEMOKRASIA.