

Wakala wa Usajili wa biashara na Leseni(BRELA) yawaita wakazi wa Dodoma na Mikoa jirani kujitokeza kwa wingi kufika katika Banda lao ili kupata Elimu ya usajili wa biashara na leseni.
Hayo yamesemwa na Afisa Leseni Mwandamizi Koyan Abubakari kutoka Brela wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangal Park Jijini Dodoma.
Abubakar amesema lengo la Brela kushiriki katika wiki ya Utumishi wa Umma ni kusogeza huduma na kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kujua majukumu ya Brela na kusajili biashara pamoja na kupewa leseni za biashara zao.
"Huduma tunazozitoa ni kusajili leseni ya biashara,Kusajili majina ya biashara,Kusajili viwanda vidogo,Usajili wa alama za biashara ambapo kusajili jina la biashara ni Tsh.20,000 ili mfanyabiashara aweze kufanya majukumu yake bila bugdha."Amesema Abubakar.
Ameongeza kuwa, BRELA imefanikiwa kuongeza mapato kupitia huduma bora kwa wateja na upanuzi wa wigo wa usajili wa biashara na leseni nchini.
Ongezeko la gawio kwa mwaka wa fedha 2024/2025 unatokana na huduma za usajili ambapo hadi kufikia Aprili 2025, BRELA imesajili Kampuni 13,794, Majina ya biashara 23,644, Leseni za Biashara kundi “A” 17,595, Leseni za Viwanda 298, Hataza 37, Alama za Biashara na Huduma 2601. Hiyo ni ishara ya kuimarika kwa uendeshaji wa taasisi na mchango wake kwa maendeleo ya taifa.
Kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo, BRELA imechangia gawio la wastani wa Shilingi bilioni 16.8 kila mwaka na hivyo kutambuliwa rasmi kwa kupewa tuzo ya taasisi bora katika utoaji wa gawio kwa Serikali.
Kwa upande wake mmoja wa wananchi aliyepata huduma katika Banda la Brela Bi Nzurika Zavala ambaye ni mjasiriamali ameishukuru Brela kwa kumpatia huduma nzuri ambapo anasema amepata ushirikiano tofauti na ulivyotarajia.
"Nimepata ushirikiano mzuri na tayari nimepewa cheti changu mwanzo nilidhani nitasumbuliwa kuwa Rudi baada ya siku kadhaa" amesema Nzurika.
Maiko Salali Arejesha Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Mpwapwa, Apongeza CCM kwa Ujumuishwaji wa Makundi Maalum
DIB YAHIMIZA WANANCHI KUDAI FIDIA ZAO KUTOKA BENKI ZILIZOFILISIKA
USHIRIKI WA TAWA KATIKA MAONESHO YA 49 YA BIASHARA YA KIMATAIFA
DWIGHT DANDA KIJANA MDOGO NA MHITIMU WA CHUO KIKUU ATIA NIA UBUNGE KIBAMBA
BoT YAWATAKA TAMFI NA TAMIU KUBORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA.
Aliyeongoza kura maoni Vunjo 2020, kumkabili tena Dkt. Kimei
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
Serikali kufanya mageuzi ya kimtazamo katika nafasi za uongozi kwa wanawake
Dkt.Tulia Aweka Jiwe La Msingi Ujenzi wa Shule ya Wavulana Bunge.
Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma