Kama Hujaripoti Kambi ya Mafunzo JKT Hutakiwi Tena | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

Kama Hujaripoti Kambi ya Mafunzo JKT Hutakiwi Tena

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limesitisha shughuli ya kupokea vijana waliochaguliwa kujiunga na jeshi hilo mwaka huu kufuatia muda wa kisheria uliowekwa kupokea vijana hao kumalizika

Flora Amon
By Flora Amon
13 Jun 2023
Kama Hujaripoti Kambi ya Mafunzo JKT Hutakiwi Tena

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limesitisha shughuli ya kupokea vijana waliochaguliwa kujiunga na jeshi hilo mwaka huu kufuatia muda wa kisheria uliowekwa kupokea vijana hao kumalizika

Akizungumzia kusitishwa kwa shughuli hiyo hiyo Mkuu wa JKT tawi la utawala Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema jeshi lilitangaza kupokea vijana hao na kuwataka kuripoti kuanzia Juni mosi mwaka huu hadi Juni 11,2023 hivyo mtu ambaye hajaripoti hadi sasa hatopokelewa tena.

Amesema kuwa walikuwa na muda wa kutosha tangu walipopata tangazo ambapo ilikuwa zaidi ya wiki mbili hivyo hawawezi kwenda kinyume na muda uliopangwa kutokana na kwamba wanaendana kwa utaratibu wa silabi.

"Ninaomba nitoe rai kwa wazazi na walezi na vijana wanapaswa kuhudhuria mafunzo haya mara tangazo litapotolewa  wafanye maandalizi yao mapema kwa kuwa muda wakiripoti ni mrefu basi waweze kuripoti kwa muda uliopangwa bila kuathiri mafunzo na ratiba ambazo zimepangwa ndani ya jeshi lakujenga Taifa," amesema Mabena

Ikumbukwe kuwa serikali ilivunja mafunzo ya JKT mwaka 1994 na baadaye kuamua kuyarejesha baada ya kuona uzalendo na maadili yanashuka miongoni mwa baadhi ya vijana hapa nchini.

Dkt.Tulia Aweka Jiwe La Msingi Ujenzi wa Shule ya Wavulana Bunge.

Dkt.Tulia Aweka Jiwe La Msingi Ujenzi wa Shule ya Wavulana Bunge.

Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma

Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma

Serikali kufanya mageuzi ya kimtazamo katika nafasi za uongozi kwa wanawake

Serikali kufanya mageuzi ya kimtazamo katika nafasi za uongozi kwa wanawake

Waziri Mhagama ametoa Agizo Vituo Vyote Vinavyotoa Huduma za Afya Viweke Wazi Mikataba Kwa Wateja

Waziri Mhagama ametoa Agizo Vituo Vyote Vinavyotoa Huduma za Afya Viweke Wazi Mikataba Kwa Wateja

CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA KUWA VINARA WA ULINZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME NA KUDUMISHA AMANI KWENYE MITAA YAO.

CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA KUWA VINARA WA ULINZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME NA KUDUMISHA AMANI KWENYE MITAA YAO.