

MWENYEKITI wa Kamati ya Itifaki ya Maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) Kitaifa mwaka 2025, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Moses Machali, amewataka wafugaji wa samaki nchini kujitokeza kwa wingi kutembelea mabanda ya taasisi za elimu ili kujifunza teknolojia mpya zinazoboresha sekta hiyo.
Akizungumza baada ya kutembelea mabanda mbalimbali kwenye maonesho hayo yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, Machali alisema amevutiwa na ubunifu wa mabinti wanaojihusisha na utengenezaji wa mafuta asilia yanayosaidia kuondoa mikunjo ya ngozi.
Machali pia alieleza kufurahishwa na teknolojia mpya inayotumika katika ufugaji wa samaki, ikiwemo mashine maalum zinazotumika kukamata vifaranga vya samaki bila kutumia mikono, hatua ambayo husaidia kupunguza vifo vya samaki wachanga ambavyo kwa kawaida hujitokeza endapo wanashikwa kwa mikono.
Amesisitiza kuwa matumizi ya teknolojia hizo ni muhimu kwa wafugaji wote wa samaki ili kuboresha uzalishaji na kuokoa mifugo midogo isiyokomaa.
Katika hatua nyingine, Machali amelitaja Banda la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Ndaki ya Masuala ya Kilimo na Teknolojia, kuwa ni eneo muhimu kwa wakulima na wafugaji kutembelea na kujifunza teknolojia mbalimbali zinazohusiana na kilimo cha kisasa.
Ameeleza kuwa moja ya teknolojia za kuvutia zinazopatikana katika banda hilo ni mtandao wa kidijitali unaowaunganisha wakulima moja kwa moja na maafisa ugani, kwa njia inayofanana na mfumo wa kuomba usafiri kwa kutumia simu za mkononi.
Maonesho ya Nanenane mwaka 2025 yameendelea kuvutia washiriki kutoka sekta mbalimbali, yakiongozwa na kaulimbiu isemayo: “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.”
DKT.SAMIA,DKT.NCHIMBI KUCHUKUA FOMU YA URAIS KESHO AGOSTI 9,2025.
TUME YATANGAZA RATIBA YA VYAMA KUCHUKUA FOMU ZA WAGOMBEA WA URAIS
TANESCO YAANZA ZOEZI LA UKAGUZI WA MITA KUBAINI UPOTEVU NA WIZI WA UMEME UNAOFANYWA NA BAADHI YA WATEJA.
CUF KUPITISHA WAGOMBEA URAIS AGOSTI 9 MAJINA YATAJWA.
PBPA YAELEZEA MAFANIKIO YAKE YA MIAKA MINNE KATIKA UONGOZI WA RAIS DK.SAMIA.
VIONGOZI WA DINI WAASWA KUSHUGHULIKIA MIGOGORO YAO YA NDANI PASIPO KUZUA TAHARUKI ILI KULINDA AMANI YA NCHI.
Coop Bank Imejipanga Kutoa Huduma Maalum kwa Washiriki wa Maonesho ya NaneNane.
SENYAMULE AIPONGEZA DIB UTOAJI WA ELIMU KWENYE MAONESHO NANENANE.
CUF KUPITISHA WAGOMBEA URAIS AGOSTI 9 MAJINA YATAJWA.
WAANDISHI WA HABARI WAHIMIZWA KUHAMASISHA USHIRIKI WA WANANCHI KUPIGA KURA