PBPA YAELEZEA MAFANIKIO YAKE YA MIAKA MINNE KATIKA UONGOZI WA RAIS DK.SAMIA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Nishati

PBPA YAELEZEA MAFANIKIO YAKE YA MIAKA MINNE KATIKA UONGOZI WA RAIS DK.SAMIA.

Wakala wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja(PBPA) wameeleza mafanikio waliyoyapata katika kipindi cha miaka minne ya uongozi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ikiwemo ajira mpya kwa watumishi mbalimbali katika majukumu ya kuratibu uagizaji wa mafuta.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
08 Aug 2025
PBPA YAELEZEA MAFANIKIO YAKE YA MIAKA MINNE KATIKA UONGOZI WA RAIS DK.SAMIA.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Erasto Mulokozi, amesema kuwa kiwango cha uagizaji mafuta nchini kupitia Mfumo wa BPS (Bulk Procurement System) kimeendelea kuongezeka kwa kasi katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza leo Agosti 7, 2025 katika mkutano wa wahariri na waandishi wa habari ulioandikwa na ofisi ya Msajili wa Hazina  wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu na mafanikio ya PBPA, Mulokozi amesema kuwa kiwango cha uagizaji mafuta kupitia mfumo huo kimeongezeka kutoka wastani wa Tani 5,805,193 mwaka 2021 hadi kufikia Tani 6,365,986 mwaka 2024, sawa na ongezeko la asilimia 9.6.

Mulokozi ameongeza kuwa hadi kufikia Desemba 2025, PBPA inatarajia kuwa jumla ya Tani 7,090,165 zitakuwa zimeagizwa, hatua inayowakilisha ongezeko la asilimia 11.4 ikilinganishwa na kipindi kama hiki mwaka uliopita.

“Ongezeko hili linadhihirisha ufanisi wa Serikali ya Awamu ya Sita katika kusimamia upatikanaji wa mafuta kwa njia ya pamoja, ambayo imeleta uwazi, ushindani na kuimarisha usalama wa nishati nchini,” amesema Mulokozi.

Wakala wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja(PBPA) wameeleza mafanikio waliyoyapata katika kipindi cha miaka minne ya uongozi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ikiwemo ajira mpya kwa watumishi mbalimbali katika majukumu ya kuratibu uagizaji wa mafuta.

Pia,mamlaka hiyo inashirikiana na Mamlaka ya bandari Tanzania ili kupanga meli za kuleta bidhaa hiyo na kuongeza ufanisi wa matumizi ya bandari nchini.

Aidha Mulokozi ameongeza kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la makampuni ambayo wanashirikiana katika mchakato wa uagizaji ambapo mpka sasa kampuni 73. 

"Mikataba ya zabuni za uletaji mafuta zilizotangazwa na kufunguliwa zimeongezeka   hivyo kama nchi tumepiga hatua kubwa sana",ameongeza Mkurugenzi huyo.

Aidha Mulokozi ameongeza kuwa serikali Tanzania imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mafuta yanapatikana kwa uhakika na kuwaondolea wananchi changamoto za ukosefu wa mafuta zilizokuwa zinawakabili.

"Katika kipindi cha miaka minne serikali imeweza kufungua mifumo ya upokeaji wa mafuta ikiwemo 'flowmeters na SCADA' ili kudhibiti udanganyifu katika kiasi cha mafuta yanayopokelewa kwenye meghala ya kuhifadhia mafuta na kupunguza upotevu wa mafuta".alieleza Mulokozi

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inanunua mafuta katika nchi zote zisizo na migogoro ya kutokufuata mashinikizo katika ununuzi ikiwemo India,Saudi Arabia,Oman na Dubai

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania(TEF)Deodatus Balile amesema Mamlaka hiyo umewapa elimu wahariri nchini kuhusu sekta ya hiyo hali.

Pia Balile aliongeza kuwa "Natoa pongezi kwa serikali  kwa sababu vidumu vimepungua sana kwenye magari hofu ya kukosa mafuta imepungua sana na mfumo huu umetuweka kwenye mazingira mazuri".

MD TWANGE AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA UPANUZI WA VITUO VYA KUPOZA UMEME JIJINI DAR ES SALAAM.

MD TWANGE AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA UPANUZI WA VITUO VYA KUPOZA UMEME JIJINI DAR ES SALAAM.

WIZARA YA NISHATI ENDELEENI KUSIMAMIA UFANISI WA MIRADI YA NISHATI- DED MKALAMA.

WIZARA YA NISHATI ENDELEENI KUSIMAMIA UFANISI WA MIRADI YA NISHATI- DED MKALAMA.

WANANCHI WAKARIBISHWA NANENANE KUFAHAMU KWA KINA MPANGO MAHSUSI WA NISHATI 2025-2030.

WANANCHI WAKARIBISHWA NANENANE KUFAHAMU KWA KINA MPANGO MAHSUSI WA NISHATI 2025-2030.

RAIS SAMIA AWAFUTA MACHOZI YA KUNI AKINA MAMA NCHINI.

RAIS SAMIA AWAFUTA MACHOZI YA KUNI AKINA MAMA NCHINI.

WIZARA YA NISHATI NA TAASISI ZAKE ZASHIRIKI  MAONESHO YA KIMATAIFA  YA KILIMO DODOMA.

WIZARA YA NISHATI NA TAASISI ZAKE ZASHIRIKI MAONESHO YA KIMATAIFA YA KILIMO DODOMA.