CUF KUPITISHA WAGOMBEA URAIS AGOSTI 9 MAJINA YATAJWA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

CUF KUPITISHA WAGOMBEA URAIS AGOSTI 9 MAJINA YATAJWA.

Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Wananchi (CUF) unatarajiwa kufanyika Kesho August 9,2025 kwa ajili yakupitisha wagombea wa Urais.upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliopendekezwa na Baraza kuu la Uongozi Taifa la Chama hicho uliyofanyika August 6 Mwaka huu.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
08 Aug 2025
CUF KUPITISHA WAGOMBEA URAIS AGOSTI 9 MAJINA YATAJWA.

Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Wananchi (CUF) unatarajiwa kufanyika Kesho August 9,2025 kwa ajili yakupitisha wagombea wa Urais.upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliopendekezwa na Baraza kuu la Uongozi Taifa la Chama hicho uliyofanyika August 6 Mwaka huu.

Taarifa hiyo imetolewa leo August 8,2025 na Mwenyekiti Taifa wa Chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba wakati akizungumza na Waandishi wa habari Makao Makuu ya Chama hicho Jijini Dar es salaam,nakubainisha kwamba wagombea waliopendekezwa kwa upande wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni pamoja Gombo Sambandito Gombo na Nkunyuntila Siwale.

Kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliopendekezwa kugombea nafasi ya Urais ni Mhandisi Mohamed Habib Mnyaa,Mhandisi Hamad Masoud Hamad,pamoja na Dr.Mohamed Habib Mikidadi ambapo wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum watapiga kura kwa ajili ya kumpata Mgombea mmoja atakayepeperusha bendera ya CUF katika kampeni za Uchaguzi Mkuu Oktoba Mwaka huu.

Aidha Prof. Lipumba pia ameongeza kuwa kupitia Mkutano Mkuu huo,CUF itazindua Ilani ya CUF kwa ajili ya kutangaza Sera za chama kwa Wananchi kwenye kampeni za uchaguzi mkuu ili kuwafanya Wananchi waweze kukiamini na kukipa ridhaa ya kushika dola.

"Baraza kuu la Uongozi Taifa limepokea na kupitisha rasimu ya Ilani ya Uchaguzi Mkuu upande wa Muungano,pamoja na rasimu ya Uchaguzi Mkuu upande wa Zanzibar na Kupitisha wagombea wa Ubunge,vilevile wagombea wa uwakilishi"amesema Prof. Lipumba.

Aidha amesema kuwa Ilani ya CUF imebeba maono mapana yakujenga Tanzania Mpya kupitia Serikali ya umoja wa kitaifa yenye misingi imara,ya usawa, mshikamano,uwajibikaji,demokrasia ya kweli na Maendeleo jumuishi kwa watu wote.

"Ilani ya CUF imejikita katika misingi yakuweza kuleta haki sawa na furaha kwa Wananchi wote,kujenga uchumi jumuishi unao ongeza ajira na kuondoa umasikini,kuimarisha misingi ya demokrasia na utawala wa Sheria kwa kupata katiba mpya inayotokana na maoni ya Wananchi,kuweka msingi wa maendeleo endelevu kwa kufanikisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu(Sustainable Development Goals)ifikapo mwaka 2030."amesema Profesa Lipumba.

Na kuongeza kuwa "Ilani yetu inatekeleza Sera ya CUF ya kipato Cha msingi ni haki ya kila Mtanzania kwa kuanza kuwalipa Wazee wote wenye miaka kuanzia 60 nakuendelea kipato cha msingi cha kujikimu,tunaamini kwamba uchaguzi Mkuu ukiwa huru nawa haki Wagombea wanaotokana na CUF chama Cha Wananchi watapata Ushindi kwenye Uchaguzi huo".

Katika hatua Nyingine Profesa Lipumba amesema kwamba amefurahishwa na mabadiliko yaliyofanywa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC)ikiwemo kuvipatia vyama vya siasa nakala halisi ya Daftari la Kudumu la Wapiga kura, hatua ambayo itasaidia mawakala kutambua idadi na majina kamili ya wapiga kura kwenye vituo vya kupigia kura.

DKT.SAMIA,DKT.NCHIMBI KUCHUKUA FOMU YA URAIS KESHO AGOSTI 9,2025.

DKT.SAMIA,DKT.NCHIMBI KUCHUKUA FOMU YA URAIS KESHO AGOSTI 9,2025.

TUME YATANGAZA RATIBA YA VYAMA KUCHUKUA FOMU ZA WAGOMBEA WA URAIS

TUME YATANGAZA RATIBA YA VYAMA KUCHUKUA FOMU ZA WAGOMBEA WA URAIS

ACT WAJIPANGA KUIONDOA CCM MADARAKANI UCHAGUZI MKUU 2025.

ACT WAJIPANGA KUIONDOA CCM MADARAKANI UCHAGUZI MKUU 2025.

Chama cha National League for Democracy (NLD) Klmezinduwa  Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya  kwa Mwaka 2025

Chama cha National League for Democracy (NLD) Klmezinduwa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya kwa Mwaka 2025

KIBAHA YAANZA MAFUNZO YA WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025

KIBAHA YAANZA MAFUNZO YA WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025