ACT WAJIPANGA KUIONDOA CCM MADARAKANI UCHAGUZI MKUU 2025. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

ACT WAJIPANGA KUIONDOA CCM MADARAKANI UCHAGUZI MKUU 2025.

Mwenyekiti wa Chama cha ACT WAZALENDO Othman Masoud Othman, amesema wamejipanga kwa umakini mkubwa kuhakikisha wanakiondoa Chama cha Mapinduzi (CCM) madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
06 Aug 2025
ACT WAJIPANGA KUIONDOA CCM MADARAKANI UCHAGUZI MKUU 2025.

Mwenyekiti wa Chama cha ACT WAZALENDO Othman Masoud Othman, amesema  wamejipanga kwa umakini mkubwa kuhakikisha wanakiondoa Chama cha Mapinduzi (CCM) madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ametoa Kauli hiyo leo Agosti 6, 2025 na  wakati akifungua Mkutano Mkuu Maalum wa Chama hicho unaoendelea katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho si mkutano wa kawaida, bali ni hatua muhimu ya kurejesha sauti, mamlaka na utu wa Mtanzania, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakinyimwa nafasi ya kushiriki kikamilifu katika uendeshaji wa nchi yao.

Kwa upande wake katibu mkuu wa ACT Addo Shaibu amesema ACT Wazalendo imejifunza kutokana na uzoefu wa historia ya vyama vingi nchini, kuanzia miaka ya 1990 hadi sasa.

Amesema tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, ACT Wazalendo imekuwa ikiweka mkazo mkubwa kwenye mipango ya kimkakati, ikitathmini mambo yaliyofanywa vyema na wapinzani tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini, sambamba na kufanyia kazi maeneo ya udhaifu ambayo yamekuwa kikwazo kwa upinzani kwa miaka mingi.

Naye,Kiongozi mkuu wa Chama hicho Dorothy Semu akizungumza katika Mkutano huo amesema wamechagua kushiriki uchaguzi sio kwa sababu ya mapenzi bali kwa sababu ya dhamira.

"Ninataka niweke wazi mbele ya wajumbe wote. Hatukuchagua kushiriki uchaguzi kwa sababu ya mapenzi. Tumechagua kushiriki kwa sababu ya dhamira. Dhamira ya kulinda haki ya kuchagua. Dhamira ya kurejesha thamani ya kura ili wananchi wawe na uwezo wa kuamua nani awe Kiongozi wao.” amesema Semu na kuongeza,

“Tumejifunza kutokana na historia, kususia hakujawahi kuleta mabadiliko. Mapambano ya kweli ni ya wale wanaojitosa uwanjani. Na sisi, ACT Wazalendo, tumeingia vitani na tutatoka na ushindi! Serikali ya CCM imeshindwa kusimamia ipasavyo uchumi, huduma za jamii, na masuala ya utawala bora,"Amesema

“Mkutano huu unakwenda kutengeneza ramani ya kuwapatia Watanzania kwanza sauti zao, ambazo zimekabwa, zimenyimwa na zimezuiwa kwa muda mrefu,” amesema Othman.

Amesisitiza kuwa mkutano huo haujaitishwa kwa lengo la kupanga miundombinu ya uchaguzi au kutafuta kura kwa ajili ya chama, bali ni kuandaa utaratibu mpya wa kurejesha mamlaka mikononi mwa wananchi, mamlaka ya kuchagua na kuwawajibisha viongozi wao.

Amewaonya wajumbe na viongozi waliohudhuria mkutano huo wasije wakawa sehemu ya kuwasaliti wananchi kwa kukosa maono ya mabadiliko au kushindwa kutekeleza wajibu wao.

DKT.SAMIA,DKT.NCHIMBI KUCHUKUA FOMU YA URAIS KESHO AGOSTI 9,2025.

DKT.SAMIA,DKT.NCHIMBI KUCHUKUA FOMU YA URAIS KESHO AGOSTI 9,2025.

TUME YATANGAZA RATIBA YA VYAMA KUCHUKUA FOMU ZA WAGOMBEA WA URAIS

TUME YATANGAZA RATIBA YA VYAMA KUCHUKUA FOMU ZA WAGOMBEA WA URAIS

CUF KUPITISHA WAGOMBEA URAIS AGOSTI 9 MAJINA YATAJWA.

CUF KUPITISHA WAGOMBEA URAIS AGOSTI 9 MAJINA YATAJWA.

Chama cha National League for Democracy (NLD) Klmezinduwa  Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya  kwa Mwaka 2025

Chama cha National League for Democracy (NLD) Klmezinduwa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya kwa Mwaka 2025

KIBAHA YAANZA MAFUNZO YA WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025

KIBAHA YAANZA MAFUNZO YA WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025