KIBAHA YAANZA MAFUNZO YA WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025 | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

KIBAHA YAANZA MAFUNZO YA WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025

Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha imeanza rasmi mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata katika Jimbo la Kibaha Mjini, ikiwa ni maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
04 Aug 2025
KIBAHA YAANZA MAFUNZO YA WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025

Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha imeanza rasmi mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata katika Jimbo la Kibaha Mjini, ikiwa ni maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo, washiriki wote wameapishwa rasmi na Mheshimiwa Frederick U. Shayo kutoka Mahakama ya Wilaya ya Kibaha, ikiwa ni hatua muhimu ya kisheria kabla ya kushiriki katika zoezi hilo nyeti la kitaifa.

Akizindua mafunzo hayo, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kibaha Mjini, Bi. Theresia Kyara, aliwataka washiriki kusikiliza kwa makini na kushiriki kikamilifu. Alisisitiza kuwa lengo kuu la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo na uelewa wa kina kuhusu majukumu yao ili kuhakikisha uchaguzi wa mwaka 2025 unafanyika kwa ufanisi, uwazi na haki.

"Ni muhimu msikie kwa makini, mzingatie katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sheria na miongozo ya Tume Huru ya Uchaguzi katika utekelezaji wa majukumu yenu," alieleza Bi. Kyara.

Mafunzo haya ya siku tatu yanatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 4 hadi 6 Agosti 2025, na yanajumuisha mada mbalimbali na amewataka kuzingatia Katiba , Sheria,Kanuni na miogozo ya Tume huru ya taifa ya uchaguzi.

Uchaguzi Mkuu wa Kumchagu Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika tarehe 29/10/2025 na kauli Mbiu ni " Kura yako Hakika yako Jitokeze kupiga"

KAILIMA ASEMA TUME ITAFANYA KAZI KWA KARIBU NA WAANDISHI WA HABARI KIPINDI CHOTE CHA UCHAGUZI MKUU 2025.

KAILIMA ASEMA TUME ITAFANYA KAZI KWA KARIBU NA WAANDISHI WA HABARI KIPINDI CHOTE CHA UCHAGUZI MKUU 2025.

INEC YAWATAKA WAZALISHAJI MAUDHUI MTANDAO KUZINGATIA WELEDI NA TAALUMA ILI KULINDA AMANI YA NCHI.

INEC YAWATAKA WAZALISHAJI MAUDHUI MTANDAO KUZINGATIA WELEDI NA TAALUMA ILI KULINDA AMANI YA NCHI.

WAANDISHI WA HABARI WAHIMIZWA KUHAMASISHA USHIRIKI WA WANANCHI KUPIGA KURA

WAANDISHI WA HABARI WAHIMIZWA KUHAMASISHA USHIRIKI WA WANANCHI KUPIGA KURA

TUME YAVIHIMIZA VYOMBO VYA HABARI KURIPOTI HABARI ZA UCHAGUZI KWA USAHIHI

TUME YAVIHIMIZA VYOMBO VYA HABARI KURIPOTI HABARI ZA UCHAGUZI KWA USAHIHI

WATANZANIA WAHAMASISHWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA UCHAGUZI MKUU WA 2025

WATANZANIA WAHAMASISHWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA UCHAGUZI MKUU WA 2025