

MKURUGENZI wa Wilaya ya Mkalama, Mkoani Singida, Asia Juma Messos ametoa wito kwa Wizara ya Nishati kuendelea kusimamia vyema Taasisi zake ili ziendelee kutekeleza miradi ya Sekta ya Nishati kwa ufanisi na hivyo kuleta maendeleo kwa Wananchi.
MKURUGENZI wa Wilaya ya Mkalama, Mkoani Singida, Asia Juma Messos ametoa wito kwa Wizara ya Nishati kuendelea kusimamia vyema Taasisi zake ili ziendelee kutekeleza miradi ya Sekta ya Nishati kwa ufanisi na hivyo kuleta maendeleo kwa Wananchi.
Messos amesema hayo Agosti 6, 2025 wakati alipoitembelea Banda la Wizara ya Nishati na Taasisi zake katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ( Nanenane) Jijini Dodoma.
Ameeleza kuwa Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa Wananchi ikiwemo miradi ya umeme na Gesi Asilia hivyo Wizara iendelee kuzisimamia Taasisi zake, ziweze kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Mkalama pia ametembelea Mabanda ya Taasisi za Wizara ambazo ni TANESCO, REA, EWURA, PURA, TPDC, PBPA na TGDC ili kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa katika Maonesho hayo.
Katika ziaza hiyo Messos ameambatana na Katibu Tawala Wilaya ya Mpwapwa, Michael Maganga, Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala kutoka Wizara ya Kilimo, Eliasifu Mlay
DKT.SAMIA,DKT.NCHIMBI KUCHUKUA FOMU YA URAIS KESHO AGOSTI 9,2025.
TUME YATANGAZA RATIBA YA VYAMA KUCHUKUA FOMU ZA WAGOMBEA WA URAIS
TANESCO YAANZA ZOEZI LA UKAGUZI WA MITA KUBAINI UPOTEVU NA WIZI WA UMEME UNAOFANYWA NA BAADHI YA WATEJA.
CUF KUPITISHA WAGOMBEA URAIS AGOSTI 9 MAJINA YATAJWA.
PBPA YAELEZEA MAFANIKIO YAKE YA MIAKA MINNE KATIKA UONGOZI WA RAIS DK.SAMIA.
TADB Yawawezesha Wakulima Wadogo Mikopo Yenye Dhamana Nafuu.
MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA 2025.
VIONGOZI WA DINI WAASWA KUSHUGHULIKIA MIGOGORO YAO YA NDANI PASIPO KUZUA TAHARUKI ILI KULINDA AMANI YA NCHI.
Coop Bank Imejipanga Kutoa Huduma Maalum kwa Washiriki wa Maonesho ya NaneNane.
SENYAMULE AIPONGEZA DIB UTOAJI WA ELIMU KWENYE MAONESHO NANENANE.