EQUITY BANK YAINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA BAJAJ KWA AJILI YA KUWASAIDIA WAKULIMA | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kilimo

EQUITY BANK YAINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA BAJAJ KWA AJILI YA KUWASAIDIA WAKULIMA

Equity Bank yaingia mkataba na kampuni ya Bajaj Processpark limited kwa ajili ya kuwasaidia wakulima ili kuhakikisha wanahifadhi mazao yao na kuyaongezea thamani katika soko la Kitaifa na Kimataifa na mkulima kupata faida kupitia kilimo chake hususani wakulima wa mbogamboga na matunda.

Moreen Rojas, Dodoma
By Moreen Rojas, Dodoma
06 Aug 2025
EQUITY BANK YAINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA BAJAJ KWA AJILI YA KUWASAIDIA WAKULIMA

Akizungumza na waandishi wa habari tarehe 06 Agosti 2025 Bw.Shabani  K. Millao Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya kondoa ambaye yuko kama kiongozi wa timu ya maandalizi ya maonesho ya 88 kufanya Ukaguzi kwenye taasisi za fedha zinazowasaidia wakulima amesema ameshuhudia  utiaji Saini kati ya Bajaj processpark limited pamoja na equity Bank mkataba unaohusisha Bajaj katika kusaidia kuthaminisha mazao ya wakulima.

"Tunaposema wakulima inamaanisha ni pamoja na mifugo kuingia mkataba na equity Bank ili kusaidia uzalishaji wa Maziwa ili yaweze kupata thamani kwani Maziwa yanapopatikana ndani ya muda mfupi na hayana sehemu sahihi ya kuhifadhia yanaweza kuharibika hivyo kupitia hawa wenzetu wa bajaj yataweza kuhifadhiwa sehemu sahihi"

Na kuongeza kuwa"Sio Maziwa pekee hata mbogamboga na hii itamsaidia pia mkulima kwani mara nyingi anapovuna anajikuta Kwa namna moja ama nyingine mazao yanakosa thamani anauza ndani ya muda mfupi lakini Kwa Sasahivi wakulima wa parachichi wameshapata mkombozi"

Aidha amesema kuwa kupitia Equity Bank mkataba walioingia wanapata vifaa vizuri Kwa ajili ya kuhakikisha wanahifadhi mazao yao sehemu salama ili thamani iongezeke.

"Tunaposema kuhifadhi mazao yao maana tunasema mkulima anakuwa na muda mzuri inamaana hata Bei ya mazao itaongezeka hivyo ni wasihi wakulima wanaohusika na matunda wasiwe na hofu Bali wawasiliane na watu wa Equity Bank Kwa Maelezo zaidi ya nini Cha kufanya"Ameongeza

Sanjari na hayo amesema kuwa sio wakulima wa matunda pekee Bali hata wale wafugaji wa mifugo inayotoa Maziwa nao ni wakati wao wa kuchangamkia fursa kwani Equity Bank iko Tanzania nzima kwa Sasa na matawi yapo kote nchini hivyo wanapaswa kufika ili waweze kuelekezwa cha kufanya Kwa usahihi.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo Cha Kilimo Biashara kutoka  Equity Bank Bi.Teofola Madilu amesema kuwa wao wanojihusisha na shughuli za Kilimo na kuongeza thamani lakini pia Kwa ajili ya kupata Mikopo ambapo kikubwa katika mkataba walioingia ni mkataba uliolenga kuleta na kuongeza thamani au kupunguza hasara ya mazao.

Aidha amesema kuwa mazao hayo yaliyolengwa ni pamoja na Maziwa na wakulima wa mbogamboga na matunda ili kupata uhifadhi wa mazao yao ili kumuwezesha mkulima kuhifadhi mazao Kwa muda ambao atautaka yeye mwenyewe na kuingia mkataba na makampuni makubwa ambayo yananunua Maziwa kama Asas na makampuni mengine.

"Maziwa yatatoka kokote na kuweza kumfikia mzalishaji mkubwa wa Maziwa kwani Kwa kufanya hivyo Kwa Kiasi kikubwa tutakuwa tumechangia ukuaji wa uchumi wa mkulima mdogomdogo lakini pia na Taifa Kwa ujumla.

Aidha amesema Tanzania Kwa Sasa ni mzalishaji mkubwa wa parachichi na anamasoko nje ya Tanzania hivyo kitu kikubwa kinachofanya wakulima washindwe kupata bei nzuri ni uhifadhi ule ubora wa Bidhaa unakuwa haupo kulingana na kiwango Cha masoko.

"Tunawakaribisha sana wananchi katika Benki yetu ya Equity wote walioko kwenye mnyororo wa thamani ya Kilimo Cha  mazao lakini wote walioko kwenye Kilimo Cha mifugo kwani tuko mikoa 8 Tanzania Bara ikiwemo Dodoma,Mbeya,Morogoro,Geita,Mwanza, Kilimanjaro,Shinyanga pamoja na Arusha"

Aidha amesema pia wanafanya kazi na mashirika na taasisi za wakulima ili kuweza kuwafikia wakulima kwani Mkoa wa Ruvuma hawana tawi lakini wameweza kuwafikia zaidi ya wakulima elfu 20 kwani wana taasisi inayowasimamia ambayo inawasaidia wao kuweza kufikisha huduma kwa wakulima hivyo huduma zao zinafika kote nchini.

Maonesho ya kitaifa ya nanenane ,mwaka 2025 yanafanyika katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma yanaongozwa na kaulimbiu isemayo: ‘Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi’.

Machali Apongeza Ubunifu wa Vijana UDSM,Awataka Wafugaji wa Samaki Kujifunza Teknolojia Mpya Zinazoboresha Sekta Hiyo

Machali Apongeza Ubunifu wa Vijana UDSM,Awataka Wafugaji wa Samaki Kujifunza Teknolojia Mpya Zinazoboresha Sekta Hiyo

Kilundumya Aipongeza e-GA Kwa Kuimarisha Ushirikiano na Sekta ya Kilimo Kuleta Mapinduzi Kidigitali.

Kilundumya Aipongeza e-GA Kwa Kuimarisha Ushirikiano na Sekta ya Kilimo Kuleta Mapinduzi Kidigitali.

Coop Benki na AGITIF Watenga Shilingi Bilioni 8.5 kwa Mikopo ya Wakulima Vijana na Vyama vya Ushirika.

Coop Benki na AGITIF Watenga Shilingi Bilioni 8.5 kwa Mikopo ya Wakulima Vijana na Vyama vya Ushirika.

TADB Yawawezesha Wakulima Wadogo Mikopo Yenye Dhamana Nafuu.

TADB Yawawezesha Wakulima Wadogo Mikopo Yenye Dhamana Nafuu.

SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.

SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.