Kilundumya Aipongeza e-GA Kwa Kuimarisha Ushirikiano na Sekta ya Kilimo Kuleta Mapinduzi Kidigitali. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kilimo

Kilundumya Aipongeza e-GA Kwa Kuimarisha Ushirikiano na Sekta ya Kilimo Kuleta Mapinduzi Kidigitali.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhe. Athumani Kilundumya, ameipongeza Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kwa kuimarisha ushirikiano na sekta ya kilimo katika kuleta mapinduzi ya kidijitali katika sekta hiyo.

Moreen Rojas, Dodoma
By Moreen Rojas, Dodoma
06 Aug 2025
Kilundumya Aipongeza e-GA Kwa Kuimarisha Ushirikiano na Sekta ya Kilimo Kuleta Mapinduzi Kidigitali.

Mhe. Kilundumya ameyasema hayo leo wakati alipotembelea banda la e-GA katika maonesho ya Kilimo na Wafugaji “Nanenane” yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Alibainisha kuwa, Wizara ya Kilimo imeshuhudia jitihada mbalimbali zinazofanywa na e-GA katika ujenzi wa mifumo ya TEHAMA kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini ya sekta ya kilimo ili kuimarisha sekta hiyo.

“Natambua jitihada za e-GA ikiwemo ujenzi wa Mfumo wa Usimamizi wa mbolea kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) ambao unawezesha usajili na utoaji wa leseni  kwa wauzaji na wasambazaji wa mbolea, utambuzi wa maghala ya utunzaji wa mbolea pamoja na udhibiti wa soko la mbolea” alifafanua.

Aliongeza kuwa, kupitia mfumo huo Serikali inaweza kudhibiti soko la mbolea na kuhakikisha mbolea inauzwa kwa bei rafiki kutokana na ruzuku ya Serikali katika mbolea na hivyo wakulima kuweza kulima na kupata faida.

Aidha, alitaja taasisi nyingine zilizoshirikiana na e-GA katika ujenzi wa mifumo ya TEHAMA kuwa ni pamoja na Tume ya Maendeleo ya Vyama vya Ushirika kwa kujenga Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushiriki na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa kujenga Mfumo wa Usimamizi wa Shughuli za Umwagiliaji.

“Nafahamu kuna Mfumo wa eKilimo ambao unarahisisha utendaji kazi katika sekta ya kilimo natamani kuona baadaye mfumo huu ukituwezesha kupata taarifa za wakulima wote hata wale wadogo waliopo vijijini ambao hawajasajiliwa, ni Imani yangu Wizara tukileta mahitaji haya e-GA mtayafanyia kazi”, alifafanua.

Naye Meneja wa Mawasiliano wa e-GA, Bi. Subira Kaswaga, amemshukuru Naibu Waziri kwa kutembelea banda la e-GA na kuahidi kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa sambamba na kuendeleza ushirikiano wa e-GA na sekta ya kilimo katika kuimarisha TEHAMA katika taasisi hiyo.

Alisema kuwa, e-GA imekuwa mstari wa mbele katika kutengeneza bunifu za mifumo ya kimkakati kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi ya kidijitali kwa jamii ya mijini na vijijini.

Maonesho ya kitaifa ya nanenane ,mwaka 2025 yanafanyika katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma yanaongozwa na kaulimbiu isemayo: ‘Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi’.

Machali Apongeza Ubunifu wa Vijana UDSM,Awataka Wafugaji wa Samaki Kujifunza Teknolojia Mpya Zinazoboresha Sekta Hiyo

Machali Apongeza Ubunifu wa Vijana UDSM,Awataka Wafugaji wa Samaki Kujifunza Teknolojia Mpya Zinazoboresha Sekta Hiyo

EQUITY BANK YAINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA BAJAJ KWA AJILI YA KUWASAIDIA WAKULIMA

EQUITY BANK YAINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA BAJAJ KWA AJILI YA KUWASAIDIA WAKULIMA

Coop Benki na AGITIF Watenga Shilingi Bilioni 8.5 kwa Mikopo ya Wakulima Vijana na Vyama vya Ushirika.

Coop Benki na AGITIF Watenga Shilingi Bilioni 8.5 kwa Mikopo ya Wakulima Vijana na Vyama vya Ushirika.

TADB Yawawezesha Wakulima Wadogo Mikopo Yenye Dhamana Nafuu.

TADB Yawawezesha Wakulima Wadogo Mikopo Yenye Dhamana Nafuu.

SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.

SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.