

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) limetangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu kuanzia elimu ya Sekondari hadi elimu ya juu ambapo uandikishaji utahusisha vijana wa Kitanzania wenye Taaluma Adimu.
Hayo yameelezwa na Kanali Gaudentius Gervas Ilonda Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)wakati akizungumza na waandishi wa habari Aprili 30 katika Makao Makuu ya Jeshi jijini Dodoma.
Aidha amesema wataalamu hao watakaoandikishwa Jeshini watapatiwa mafunzo mbalimbali muhimu ya kijeshi na mafunzo ya kuwaendeleza katika taaluma zao.
Aidha Vijana wa Kitanzania wenye nia ya kuandikishwa na Jeshi anatakiwa awe raia wa Tanzania mwenye kitambulisho cha Taifa,awe na afya nzuri na timamu,mwenye tabia na nidhamu nzuri,hajapatikana na hatia ya makosa ya jinai mahakamani na kufungwa,awe na Cheti halisi Cha kuzaliwa(Original Birth Certificate)Vyeti vya Shule na taaluma.
Vilevile awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza,Chuo Cha Mafunzo au kikosi Cha kuzuia Magendo,awe amehitimu Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT kwa mkataba wa kujitolea au mujibu wa sheria na kutunukiwa Cheti.
"Kwa Vijana wenye elimu ya kidato Cha Nne na kidato Cha Sita wawe na umri usiozidi miaka 24,Vijana wenye Elimu ya Stashahada umri usiozidi miaka 26, Vijana wenye elimu ya juu umri usiozidi miaka 27,na Madaktari Bingwa wa binadamu umri usiozidi miaka 35 ya kuzaliwa"
Aidha Taaluma adimu zinazohitajika ni Generall Surgeon,Orthopaedic Surgeon,Urologist Radiologist,ENT Specialist,Anaesthesiologist,Physician, Ophthalmologist, Paediatrician, Obstetrician & Gynaecologist,Ocologis, Pathologist, Psychiatrist, Emergency Medicine Specialist na Haematologist.
Pamoja na Medical Doctor, Dental Doctor, Veterinary Medicine,Bio Medical Engineer,Dental Laboratory Technician, Anaesthetic, Radiographer,Optometry, Physiotherapy na Aviation Doctor.
Aidha Taaluma za Uhandisi(Engineer) ni pamoja na Bachelor of Electronic Engineering, Bachelor of Mechanical Engineering, Bachelor in Marine Engineering, Bachelor in Marine transportation & Nautical Science, Bachelor in Mechanic in Marine Diesel Engine, Bachelor in Aviation Management, Bachelor in Aircraft Accident & Incident Investigation, Bachelor in Meteorology, Air Traffic Management & Aeronautic Engineering bila kusahau Fundi Mchundo Aluminum Welding na Welding & Metal Fabrication.
Sanjari na hayo utaratibu wa kutuma maombi kwa makundi yote mawili ni maombi yote yaandikwe Kwa mkono na yawasilishwe Makao Makuu ya Jeshi Dodoma kuanzia tarehe 01 Mei 2025 hadi tarehe 14 Mei,2025 yakiwa na Nakala ya kitambulisho cha Taifa au nambari ya NIDA,Nakala ya Cheti Cha kuzaliwa,vyeti vya Shule na chuo, Nakala ya Cheti Cha JKT kwa waombaji waliomaliza mkataba wa kujitolea pamoja na nambari ya simu ya mkononi ya Mwombaji.
Aidha ametoa angalizo kwa wananchi wote wasikubali kurubuniwa na matapeli ambao watajitokeza kwani hakuna nafasi ya kujiunga Jeshini kwa kutoa fedha na atakaye toa Rushwa na kupokea Rushwa Sheria itawashughulikia.
Maombi yatumwe Kwa anuani ya Mkuu wa Utumishi Jeshini,Makao Makuu ya Jeshi,Sanduku la Posta 194,DODOMA Tanzania.
WANANCHI LUHITA WALIA NA MAGUGU ZIWA BURIGI.
Wananchi wa mialo na ziwa waiomba serikali kuboresha miundombinu
RAIS SAMIA Ameziagiza Wizara ya Fedha,Kilimo Kukaa pamoja na BOT Kuja na Sera ya Taifa.
BODI YA TASAC:SERIKALI IMEWEKA MIKAKATI YA KUIMARISHA BANDARI ZOTE NCHINI.
SINGIDA KASKAZINI WAIAMBIA TUME JIMBO LIITWE ILONGERO.
Wizara ya Afya Imesisitiza Umuhimu wa Elimu ya Afya ya Uzazi Kwa Watoto na Vijana.
Kiwango Cha Maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria Kimepungua Kwa takribani asilimia 45
BODI YA WAKURUGENZI TASAC YARIDHISHWA NA MABORESHO YA BANDARI ZA KEMONDO NA BUKOBA.
SINGIDA KASKAZINI WAIAMBIA TUME JIMBO LIITWE ILONGERO.
RAIS SAMIA Ameziagiza Wizara ya Fedha,Kilimo Kukaa pamoja na BOT Kuja na Sera ya Taifa.