

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala Meli Tanzania (TASAC), Nahodha Mussa Mandia amesema kuwa Serikali imeweka mikakati ya kuimarisha bandari zote nchini pamoja mialo ya Uvuvi ili kuongeza huduma za maendeleo kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala Meli Tanzania (TASAC), Nahodha Mussa Mandia amesema kuwa Serikali imeweka mikakati ya kuimarisha bandari zote nchini pamoja mialo ya Uvuvi ili kuongeza huduma za maendeleo kwa wananchi.
Nah.Mandia ameyasema hayo wakati Bodi hiyo ilipotembelea Bandari ya Magarini na Mwalo wa Lwazi katika Wilaya Muleba mkoani Kagera.
Amesema kuwa kama wadhibiti kazi yao kuangalia usalama wa Bandari, Mialo ya Uvuvi pamoja na shughuli zinazofanyika katika maeneo hayo katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na salama ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa Taifa.
“Miradi inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali inatokana na rasilimali zilizopo kwa sasa na maeneo ambayo bado serikali inaendelea kufanyia kazi na kuwataka wananchi kuwa na subira huku wakiendelea kufanya shughuli zao"Amesema.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kikuku Abdul Hassan amesema changamoto yao katika Mwalo wa Lwazi ni kukosekana kwa Ghati ya kuegeshea vyombo vya usafiri maji hivyo ameiomba ³Serikali kutatua changamoto hiyo ambapo itasaidia kuongeza vyombo vya usafiri wa majini vinavyohudumia wananchi wa visiwa mbalimbali.
Amesema kuwa ziara ya Bodi ya TASAC ni moja ya njia ya Serikali kuwafikia wananchi kuwasikiliza na kushauriana ili kupata mwanga katika utatuzi wa changamoto zao. Amewaomba wananchi waendelee kuwa na imani ya Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi yake katika kutatua changamoto kwa wananchi wake na kuwaletea maendeleo.
Nae,Mwenyekiti wa Umoja wa Wasafirishaji wa Bandari ya Magarini amesema kuwa wanaishukuru TASAC kwa kuwapa elimu ya usalama wa vyombo vya majini ambapo wanaendelea kuwa kujisimamia kutokana na elimu hiyo.
JWTZ YATANGAZA Nafasi Kwa Vijana wa Kitanzania.
WANANCHI LUHITA WALIA NA MAGUGU ZIWA BURIGI.
Wananchi wa mialo na ziwa waiomba serikali kuboresha miundombinu
RAIS SAMIA Ameziagiza Wizara ya Fedha,Kilimo Kukaa pamoja na BOT Kuja na Sera ya Taifa.
SINGIDA KASKAZINI WAIAMBIA TUME JIMBO LIITWE ILONGERO.
JWTZ YATANGAZA Nafasi Kwa Vijana wa Kitanzania.
Wizara ya Afya Imesisitiza Umuhimu wa Elimu ya Afya ya Uzazi Kwa Watoto na Vijana.
Kiwango Cha Maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria Kimepungua Kwa takribani asilimia 45
BODI YA WAKURUGENZI TASAC YARIDHISHWA NA MABORESHO YA BANDARI ZA KEMONDO NA BUKOBA.
SINGIDA KASKAZINI WAIAMBIA TUME JIMBO LIITWE ILONGERO.