Wananchi wa mialo na ziwa waiomba serikali kuboresha miundombinu | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

Wananchi wa mialo na ziwa waiomba serikali kuboresha miundombinu

Wananchi wa Mialo ya Chaamchuzi,Lukombe pamoja Ziwa la Lwakajunju Wilayani Karagwe wameiomba Serikali kujenga miundombinu katika mialo na Ziwa hilo ili kuweza kufanya kazi yao katika mazingira yatakayoongeza mapato ya Serikali.x

NICHOLAUS KINYARIRI (OUT)
By NICHOLAUS KINYARIRI (OUT)
29 Apr 2025
Wananchi wa mialo na ziwa waiomba serikali kuboresha miundombinu

Wananchi wa Mialo ya Chaamchuzi,Lukombe pamoja Ziwa la Lwakajunju Wilayani Karagwe wameiomba Serikali kujenga miundombinu katika mialo na Ziwa hilo ili kuweza kufanya kazi yao katika mazingira yatakayoongeza mapato ya Serikali.

Wananchi hao wameyasema hayo wakati ziara ya Bodi ya Wakurugenzi  wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) wakati Bodi hiyo ilipotembelea mialo hiyo pamoja na Ziwa wilayani Karagwe mkoani Kagera.

Mwananchi wa Mwalo wa Chamchuzi Leonard Lupenda amesema ujio wa TASAC ni muokozi kwa changamoto zinazowakabili katika mwalo kuhusiana na kukosekana kwa gati la kuegeshea vyombo vya usafiri majini,sehemu ya abiria kupumuzikia abiria pamoja na miundombinu ya kuhifadhi mizigo katika safari zao katika nchi ya Rwanda.

Amesema kuwa mizigo wanatoa nchini Rwanda kuja Karagwe ambapo wakiweka mazingira mazuri Serikali itaongeza mapato pamoja na shughuli za uvuvi utasaidia katika kupata masoko ya samaki kutokana na miundumbinu itakayowekwa.

Kwa upende wa Jonas Bakonga amesema miundombinu katika mwalo wa Lukombe ni changamoto  ikiwemo barabara ,magati ambapo serikali kuna  siku itakosa mapato kwani maeneo hayo yatashindwa kufikika.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha  Kavunjo Deus Kaijage amesema kuwq suala la usalama ni changamoto  na kuitaka serikali kuangalia kutokana na biashara za maeneo hayo ni kwenda katika nchi jirani hivyo wanaweza kuingia wahamiaji haramu.

Akizungumzia changamoto  hizo Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nah.Mussa Mandia  amesema serikali inafanya kazi kubwa na kuahidi changamoto hizo zitashughulikiwa kutokana na umuhimu wa maeneo hayo katika serikali kuendelea kuongeza mapato.

Amesema kuwa ziara hiyo katika  mialo hiyo pamoja na ziwa ni kuangalia usalama wa vyombo vya usafiri majini pamoja na miundombinu yake ikiwa ni kuchukua maoni ya wadau waliopo katika mnyororo huo kwa kupeleka katika ngazi mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji.

Hata hivyo amesema kuwa katika mkoa wa Kagera kuna maziwa 15 ambapo kazi ni kuangalia juu ya shughuli zinazofanyika.

Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Julius Laizer amesema kuwa wamekuwa wakidhibiti shughuli  za mageto na hawatakuwa na huruma ya majadiliano kwa mtu atakayejihusisha na mageto.

Hata hivyo amesema ujio wa TASAC ni kwenda katika kuboresha maeneo hayo ambapo ni faida kwa serikali  katika kuongeza mapato yake.

Mwenyekiti  wa Wasafirishaji kutoka Karagwe kwenda nchini Rwanda amesema kuwa wanaiomba Serikali kuendelea kuboresha miundombinu  katika kuchochea ukusaji wa mapato na wako tayari kuendelea kushirikiana na Serikali.

KAPINGA AZINDUA KITUO MAMA CHA GESI ASILIA ILIYOSHINDILIWA (CNG) JIJINI DAR ES SALAAM.

KAPINGA AZINDUA KITUO MAMA CHA GESI ASILIA ILIYOSHINDILIWA (CNG) JIJINI DAR ES SALAAM.

WANANCHI LUHITA WALIA NA MAGUGU ZIWA BURIGI.

WANANCHI LUHITA WALIA NA MAGUGU ZIWA BURIGI.

BODI YA TASAC:SERIKALI IMEWEKA MIKAKATI YA KUIMARISHA BANDARI ZOTE NCHINI.

BODI YA TASAC:SERIKALI IMEWEKA MIKAKATI YA KUIMARISHA BANDARI ZOTE NCHINI.

BODI YA WAKURUGENZI  TASAC YARIDHISHWA NA MABORESHO YA BANDARI ZA KEMONDO NA BUKOBA.

BODI YA WAKURUGENZI TASAC YARIDHISHWA NA MABORESHO YA BANDARI ZA KEMONDO NA BUKOBA.

TPDC,  ZPDC  ZAENDELEA KUSHIRIKIANA UENDELEZAJI SEKTA YA GESI NCHINI.

TPDC, ZPDC ZAENDELEA KUSHIRIKIANA UENDELEZAJI SEKTA YA GESI NCHINI.