

Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imesema kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika miradi ya ujenzi wa Bandari za Kemondo na Bukoba hivyo fedha hizo zinatakiwa kuleta tija na zirudi kutokana huduma zitazotolewa na Bandari hizo.
Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imesema kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika miradi ya ujenzi wa Bandari za Kemondo na Bukoba hivyo fedha hizo zinatakiwa kuleta tija na zirudi kutokana huduma zitazotolewa na Bandari hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati ziara Bodi katika Bandari hizo Mwenyekiti wa Bodi hiyo Nah.Mussa Mandia amesema kuwa baada ya maboresho ya miundombinu ya ujenzi wa bandari watahudumia mizigo na abiria kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na ilivyokuwa awali.
"Fedha ya Bandari ya Kemondo bilioni 20 na ujenzi wake umekamilika ambapo huduma zake zimeongezeka hadi kufikia tani 150000 kwa mwezi na mapato yake yameongezeka mara tatu huku Bandari ya Bukoba ujenzi wake ukiwa katika hatua za mwisho na unaogharimu zaidi ya sh.Bilioni 19",Amesema.
Amesema kuwa kama wadhibiti ni kuhakikisha Bandari hizo zinaendelea kutoa huduma bora na tija kwa serikali huku akitaka wasimamizi wa bandari kusimamia kwa weledi.
Amesema Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Dkt.Samia Suluhu Hassan imeweza kutimiza ndoto katika upanuzi wa bandari za Kemondo na Bukoba ambapo miundombinu yake ilikuwa ya zamani na ilikuwa haiendani na mahitaji ya sasa.
Hata hivyo amesema bodi itaendelea kushauri katika taasisi wanayoidhibiti ambapo matokeo yake yataendelea kuonekana kwa miradi mbalimbali kwenye bandari za nchi nzima
Mtendaji mkuu wa Bandari ya Bukoba wa TPA Malick Ismail amesema kuwa maboresho ya ujenzi wa bandari hiyo baada ya kukamilika watahudumia meli nne kwa wakati mmoja tofauti na ilivyokuwa awali ambapo walikuwa wakihudumia meli moja.
Bodi hiyo ilitembelea Bandari ya Kemondo ,Bukoba pamoja na kiwanda cha Vic Fish TASAC inadhibiti uzito kwa ajili ya Usafirishaji wa Samaki nje ya nchi.
JWTZ YATANGAZA Nafasi Kwa Vijana wa Kitanzania.
WANANCHI LUHITA WALIA NA MAGUGU ZIWA BURIGI.
Wananchi wa mialo na ziwa waiomba serikali kuboresha miundombinu
RAIS SAMIA Ameziagiza Wizara ya Fedha,Kilimo Kukaa pamoja na BOT Kuja na Sera ya Taifa.
BODI YA TASAC:SERIKALI IMEWEKA MIKAKATI YA KUIMARISHA BANDARI ZOTE NCHINI.
JWTZ YATANGAZA Nafasi Kwa Vijana wa Kitanzania.
Wizara ya Afya Imesisitiza Umuhimu wa Elimu ya Afya ya Uzazi Kwa Watoto na Vijana.
Kiwango Cha Maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria Kimepungua Kwa takribani asilimia 45
SINGIDA KASKAZINI WAIAMBIA TUME JIMBO LIITWE ILONGERO.
RAIS SAMIA Ameziagiza Wizara ya Fedha,Kilimo Kukaa pamoja na BOT Kuja na Sera ya Taifa.