

Wananchi Kijiji cha Luhita Wilaya ya Karagwe Mkoa Kagera wanaotumia Ziwa la Burigi wameliomba Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kuangalia namna ya kutoa magugu katika Ziwa hilo kutokana na changamoto wanazozipata wakati wa kusafiri na kuvua samaki na vyombo vya usafiri majini.
Wananchi Kijiji cha Luhita Wilaya ya Karagwe Mkoa Kagera wanaotumia Ziwa la Burigi wameliomba Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kuangalia namna ya kutoa magugu katika Ziwa hilo kutokana na changamoto wanazozipata wakati wa kusafiri na kuvua samaki na vyombo vya usafiri majini.
Wananchi hao wameyasema hayo wakati ziara Bodi ya TASAC wakati walipotembelea Mwalo wa Luhita katika Ziwa Burigi kuangalia usalama wa usafiri wa majini katika Ziwa hilo.
Mwenyekiti wa Usimamizi wa Mazingira ya Fukwe (BMU) Nelson Atanas amesema kuwa katika kufany safari katika ziwa hilo upande wa Luhita imekuwa changamoto kutokana njia wanaoitumia wamechonga ambapo vyombo vya usafiri majini viwili haviwezi kupishana.
Amesema ujio wa Bodi kwao ni fursa ya kuweza kupata msaada namna ya kutoa au kupunguza magugu katika mwalo huo na kurahisisha usafiri wa kwenda upande wa pili ambapo wananchi wote wanategemeana kwa biashara.
Kwa upande mwananchi wa kijiji wa Mwalo wa Luhita Leopord Baltazal amesema kuwa utafika wakati kutokana na magugu hayo kuongezeka watashindwa kufanya shughuli za uvuvi pamoja na kusafiri kwenda upande wa pili na kufanya maisha yao kuwa magumu.
Akitolea ufafanuzi wa changamoto hizo Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nah.Mussa Mandia amesema kuwa TASAC wanachukua changamoto katika kufanyia kazi ili kuhakikisha shughuli zao ziendelee kutokana na kuwa na mchango kwa mapato na maisha yao kwa ujumla.
Amesema katika kushughulika na magugu ni pamoja kuwa na gati na miundombinu mingine ya huduma katika mwalo wa Luhita.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Bodi katika Mwalo huo amemwagiza Mtendaji wa kijiji kuandika kwa maandishi mahitaji yanayohitajika na kupeleka kwa Afisa Mfawidhi wa TASAC Mkoa Kagera.
Nahodha Mandia amesema kuwa licha kuwa na changamoto hizo usalama unahitajika kutokana na sheria ya kuhakikisha wanakuwa na vifaa vya uokozi wakati wote.
Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita ya Dkt.Samia Suluhu Hassan iko karibu na wananchi katika kutatua changamoto na mengi yamefanyika kwenye Bandari ,Mialo ya Uvuvi na usafirishaji wa abiria.
Polisi Watuliza Hofu: Usalama Waimarishwa Kwa Uchaguzi Oktoba 29
TUNAAMINI UCHAGUZI UTAKUWA WA AMANI NA USALAMA UTAKUWEPO- WANANCHI WA KIBAHA
RC MAKALLA AWAHAKIKISHIA USALAMA WAZEE WA MKOA WA ARUSHA SIKU YA UPIGAJI KURA OKTOBA 29.
Mfalme wa Mashairi Awasha Moto wa Uzalendo: “Kura Yako Ni Silaha”
MUFTI ATAKA WAISLAMU KUZINGATIA MAFUNDISHO YA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29.
BRIGEDIA JENERALI NDAGALA AFUNGUA KONGAMANO LA WADAU WA USIMAMIZI WA MAAFA JIJINI MBEYA
Mkomi Awasisitiza Wakuu wa Taasisi Kusimamia Mifumo ya Kielektroniki Serikalini.
WAZEE WAASWA KUHAMASISHA JAMII KUJITOKEZA KUPIGA KURA.
DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”
TUMEJIANDAA VYEMA KUDHIBITI UHALIFU NA WAHALIFU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU- POLISI