

Wizara ya Afya imesisitiza umuhimu wa elimu ya afya ya uzazi kwa watoto na vijana, pamoja na upatikanaji wa chanjo ya HPV kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 14, kama hatua ya kudhibiti kuenea kwa ugonjwa hatari wa Saratani ya Mlango wa Kizazi.
Pia, wanawake wamehimizwa kufanya uchunguzi wa mara kwa mara ili kugundua ugonjwa huo mapema na kupata matibabu stahiki.
Hayo yameelezwa na Kaimu Meneja mpango wa taifa wa chanjo Lodalis Gadao Aprili 24, 2025 Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari katika madhimisho ya wiki ya chanjo kitaifa.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Gadao amesema, tatizo hili ambalo huwakumba wanawake hutokea kwenye mlango wa kizazi katika sehemu inayounganisha mfuko wa uzazi (Uteras) Pamoja na uke (Vagina) kutokana na seli za mlango huu kukua kwa kasi isiyo ya kawaida.
Aidha amesema Licha ya jitihada zinazofanywa na serikali kupitia Wizara ya Afya, na wadau mbalimbali kukabiliana na ugonjwa wa saratani ya malango wa kizazi bado tatizo hili limendelea kuwa tishio.
Tatizo la ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi limezidi kuwa tishio licha ya jitihada zinazofanywa na serikali kupitia Wizara ya Afya na wadau mbalimbali kukabiliana na changamoto hiyo.
Hata hivyo takwimu zilizotolewa na taasisi ya Saratani ya Ocean Road imeonyesha kuwa takribani asilimia 36 ya vifo vinavyotokana na ugonjwa Saratani nchini husababishwa na aina hii ya saratani.
Lakini pia wizara ya afya imesema zaidi ya wanawake 10,000 huambukizwa saratani ya mlango wa kizazi kila mwaka, huku zaidi ya wanawake 6,000 wakipoteza Maisha kutokana na ugonjwa huu.
Kaimu Meneja mpango wa taifa wa chanjo Lodalis Gadao amesema, ugonjwa huo kwa sasa ni tishio kwa wanawake, kutokana na uelewa mdogo juu ya ugonjwa huo Pamoja na mwitikio mdogo kwa wanawake kujitokeza kupata chanjo.
“Wanawake wengi hawana utamaduni wa Kwenda vituoni kupima afya zao hivyo inapelekea ugumu kugundua mapema kama wana tatizo hili ili kuanza matibabu mapema jambo linaloleta ufanisi katika uponaji.”Amesema Gadao.
Amesema wanawake wengi hufika hospitali wakiwa tayari wako katika hatua za mwisho za ugonjwa huu hivyo kupata matibabu ambayo huweza kupelekea kupona au kupoteza Maisha.
“Asilimia zaidi ya 70 ya wagonjwa wanaofika hospitali kupata matibabu, hufika kwa kuchelewa sana, na wanakuja wakiwa katika hatua ya mwisho jambo linalopelekea ugumu katika uponaji wa tatizo hili.”Amesema.
Hata hivyo amewataja wanawake walio na maambukizi ya VVU kuwa kundi hatari zaidi kuambukizwa ugonjwa huu, kutokana kudhurika kwa maumbile yao ambayo huwezesha kirusi hiki kukaa kwa urahisi.
Aidha katika taarifa hiyo pia Gadau amebainisha kuwa watoto wa kike wanaoanza kujihusisha na ngono katika umri mdogo wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa aina hii ya saratani.
Amesema uchunguzi wa hivi karibuni umeonyesha kuwa kati ya Watoto wakike wanne wanaojihusisha na mapenzi katika umri mdogo watatu hupata maambukizi ya ugonjwa huu.
Mbali na hatari za ugonjwa huu Gadao pia ametaja mikakati mbalimbali inayoendelea ili kutokomeza tataizo hili, ikiwemo utoji wa chanjo kwa Watoto wadogo wenye umri kuanzia miaka 9.
Lakini pia kuwakinga watoto wa kike wenye umri mdogo, kushiriki katika mahusiano ya kimapenzi.
Lakini pia ameitaka jamii kubadilika, na kuachana mara moja na tabia ya kushiriki kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.
’’Kitu kingine ambacho kitasaidia kuepukana na ugonjwa huu kwa wanawake ni kubadili tabia yakuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwananume Zaidi ya mmoja, kwasababu kirusi hiki huambukizwa kwa njia ya kujamiiana na hupatikana kwa wanaume.’’Amesema.
Kwa upande wake Afisa Programu wa Elimu ya kwa umma katika mpango wa taifa wa chanjo Dk.Tumaini Haonga amesema licha ya kuwepo kwa utaratibu wa utoaji wa chanjo ya ugonjwa huu bado zipo baadhi ya changamoto ambazo husababisha walengwa kutokupata chanjo au kushindwa kumaliza dozi.
Amesema baadhi ya wanajamii hususani wafugaji na wakulima hushindwa kufikiwa kwa urahisi wakati wa utoaji wa chanjo kutokana na tabia kuhamahama ili kuendesha shughuli zao.
Lakini pia baadhi ya wazazi wanaoishi mijini kushindwa kuwafikisha Watoto wao kupata huduma ya chanjo kutokana na kukosa muda.
’’Changamoto tunazokutana nazo ni baadhi ya wazazi wanaoishi mijini hushindwa kuwapeleka watoto wao kupata huduma ya chanjo kutokan kubanwa na kazi jambo linalorudisha nyuma mapambano dhidi ya ugonjwa huu.’’Amesema Haonga.
JWTZ YATANGAZA Nafasi Kwa Vijana wa Kitanzania.
WANANCHI LUHITA WALIA NA MAGUGU ZIWA BURIGI.
Wananchi wa mialo na ziwa waiomba serikali kuboresha miundombinu
RAIS SAMIA Ameziagiza Wizara ya Fedha,Kilimo Kukaa pamoja na BOT Kuja na Sera ya Taifa.
BODI YA TASAC:SERIKALI IMEWEKA MIKAKATI YA KUIMARISHA BANDARI ZOTE NCHINI.
JWTZ YATANGAZA Nafasi Kwa Vijana wa Kitanzania.
Kiwango Cha Maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria Kimepungua Kwa takribani asilimia 45
BODI YA WAKURUGENZI TASAC YARIDHISHWA NA MABORESHO YA BANDARI ZA KEMONDO NA BUKOBA.
SINGIDA KASKAZINI WAIAMBIA TUME JIMBO LIITWE ILONGERO.
RAIS SAMIA Ameziagiza Wizara ya Fedha,Kilimo Kukaa pamoja na BOT Kuja na Sera ya Taifa.