

Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye ulemavu Mhe.Ridhiwani kikwete amesema Maadhimisho ya Siku ya usalama na afya mahala pa kazi yanatarajiwa kufanyika tarehe 28 Aprili Mkoani Singida ambapo amewahimiza waajiri nchini kuendelea kufanya usajili wa sehemu za kazi.
Mhe.Ridhiwani kikwete wakati akizungumza na waandishi wa habari Aprili 23 kwenye Ofisi za OSHA jijini Dodoma amesema lengo la kusajili maeneo ya kazi ni ili yatambulike na kuendelea kuyasimamia na kuyapa miongozo muhimu itakayowezesha kuboresha mazingira ya kazi nchini.
"Hivyo kupitia maadhimisho haya,tunapenda kutoa wito Kwa waajiri wote kuhakikisha kwamba wanasajili maeneo yao ya kazi OSHA pamoja na kuendelea kutekeleza taratibu mbalimbali za usalama na afya kwa mujibu wa sheria Na.5 ya Usalama na Afya mahala pa kazi ya mwaka 2003"
"Sasa hivi usajili umerahisishwa sana,unaweza jisajili na OSHA ukiwa mahali popote bila ya kufunga safari kuja OSHA,kupitia mtandao wa Workplace Information Management System (WIMS)"
Aidha amesema moja ya majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni kulinda Afya na Usalama wa wafanyakazi wanapokua wanatekeleza majukumu yao ya kila siku kwani kanuni bora za usalama na afya zisipozingatiwa mahali pa kazi,inaweza kusababisha matukio ya ajali zinazosababisha ulemavu wa kudumu, magonjwa,vifo kwa wafanyakazi na hata uharibifu wa mali.
Aidha Kwa mujibu wa makadirio ya Shirika la kazi Dunia(ILO)na Shirika la Afya Duniani(WHO)ya mwaka 2023 takribani wafanyakazi milioni 2.93 hufariki Kila mwaka kutokana na ajali na magonjwa yanayohusiana na kazi.
"Idadi hii imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 5 ikilinganishwa na mwaka 2015,ikionyesha kuwa mazingira ya kazi yanaendelea kuwa chanzo kikubwa Cha hatari kwa wafanyakazi,kati ya vifo hivyo takribani milioni 2.6 vinatokana na magonjwa yanayohusiana na kazi,huku ajali kazini zikisababisha vifo 330,000 kila mwaka"
Aidha magonjwa yanayochangia idadi kubwa ya vifo hivyo ni pamoja na magonjwa ya mzunguko wa damu,saratani na magonjwa ya mfumo wa upumuaji,ambayo yanahisiana moja kwa moja na mazingira hatarishi ya kazi.
"Nchi yetu pia tumeendelea kupata matukio ya ajali na vifo sehemu za kazi,kwa mfano kati ya Julai 2019 na Juni 2021,Tanzania ilirekodi ajali za kazini 4,993 ambapo sekta ya viwanda na uzalishaji iliongoza kwa idadi kubwa ya matukio,katika kipindi hicho wafanyakazi 249 walipata magonjwa yanayohusiana na kazi na ajali 217 zilisababisha vifo,takwimu hizi zinaonyesha athari kubwa za kutokuwa na mazingira salama kazini"
Sanjari na hayo fidia kwa waathirika wa ajali kazini imekuwa mzigo mkubwa kifedha,hadi Juni 2023 fidia iliyotolewa ilifikia shilingi bilioni 27.93 ikilinganishwa na Shilingi bilioni 13.19 Kwa kipindi kilichoishia Juni 2021, ongezeko hili linaonyesha gharama kubwa zinazobebwa na waajiri wa Serikali kutokana na ajali kazini.
"Takwimu hizi zinadhihirisha kuwa kutokuwekeza katika usalama na afya kazini kunaweza kusababisha hasara kubwa,si tu kwa maisha ya wafanyakazi bali pia kwa gharama za kifedha kwa waajiri na taifa kwa ujumla,ni muhimu kwa waajiri kuelewa kuwa kuboresha mazingira ya kazi si gharama ya ziada bali ni uwekezaji unaoleta faida kwa kuongeza tija,kupunguza gharama za fidia na kulinda maisha ya wafanyakazi.
Aidha amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,inatambua umuhimu wa kulinda nguvukazi ya Taifa,kupitia taasisi ya OSHA Serikali inaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa sheria Na.5 ya Afya na Usalama mahali pa kazi ya mwaka 2003 miongoni mwa wadau wa watanzania wote kwa ujumla,lengo ni kuhakikisha kwamba maeneo yote ya kazi nchini yanakuwa na mifumo madhubuti ya kuwakinga wafanyakazi dhidi ya ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.
JWTZ YATANGAZA Nafasi Kwa Vijana wa Kitanzania.
WANANCHI LUHITA WALIA NA MAGUGU ZIWA BURIGI.
Wananchi wa mialo na ziwa waiomba serikali kuboresha miundombinu
RAIS SAMIA Ameziagiza Wizara ya Fedha,Kilimo Kukaa pamoja na BOT Kuja na Sera ya Taifa.
BODI YA TASAC:SERIKALI IMEWEKA MIKAKATI YA KUIMARISHA BANDARI ZOTE NCHINI.
JWTZ YATANGAZA Nafasi Kwa Vijana wa Kitanzania.
Wizara ya Afya Imesisitiza Umuhimu wa Elimu ya Afya ya Uzazi Kwa Watoto na Vijana.
Kiwango Cha Maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria Kimepungua Kwa takribani asilimia 45
BODI YA WAKURUGENZI TASAC YARIDHISHWA NA MABORESHO YA BANDARI ZA KEMONDO NA BUKOBA.
SINGIDA KASKAZINI WAIAMBIA TUME JIMBO LIITWE ILONGERO.