Waziri Simbachawene "Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali" | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

Waziri Simbachawene "Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali"

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe.George Simbachawene amesema sio lazima Kila mhitimu aajiriwe na Serikali kwani Serikali haina uwezo wa kuajiri kila mtu ndio maana Serikali inashirikiana na taasisi pamoja na Sekta binafsi kutoa ajira katika ujenzi wa uchumi na kutokomeza tatizo la ajira

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
17 Apr 2025
Waziri Simbachawene "Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali"

Waziri Simbachawene amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mafanikio na mwelekeo wa Wizara hiyo katika kipindi Cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita Aprili 17,2025 katika  ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dodoma.

Aidha amesema Katika kipindi cha kuanzia Mwaka 2020 hadi Mwezi Agosti, 2024 Taasisi 275 katika Utumishi wa Umma zilijengewa uwezo kuhusu uzingatiaji wa  Sheria,  Kanuni  na  Taratibu kwenye  ushughulikiaji  wa  masuala  ya Kiutumishi.

Aidha, Taasisi 543 zilikaguliwa kwa lengo la kuangalia uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu zinazosimamia masuala ya Kiutumishi.

Aidha ameongeza kuwa Katika kupambana na upungufu wa ajira, Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ilifanikisha mchakato wa Ajira na kuwapangia vituo vya kazi jumla ya waombaji kazi 55,162 ambapo waombaji kazi waliopangiwa vituo vya kazi waliongezeka kutoka 7,659 mwaka 2020 hadi 20,158 mwaka 2024, sawa na ongezeko la asilimia 163.19

"Serikali kupitia Ofisi hii baada ya kuona kuna tatizo la upungufu wa watumishi katika maeneo mengi, ilitafuta namna bora ya kuondoa changamoto hiyo kwa kujenga Mfumo wa Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu (HR-Assessment). Mfumo huu wa Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu ni msaada mkubwa kwani unabainisha idadi ya watumishi walioko katika kila kituo cha kazi na upungufu au ziada iliyopo ili kuwa na idadi ya watumishi sahihi katika sehemu sahihi za utekelezaji wa majukumu yao"

"Kupitia mfumo huu, taasisi za umma zimewezeshwa kuandaa mahitaji ya watumishi. Hadi kufikia Mei, 2024 Mfumo umechakata takwimu  kwa Mikoa yote 26 ya Tanzania na kuzifikia taasisi 534. Baada ya majumuisho ya Taarifa za tathmini ya mahitaji ya watumishi kwa Taasisi hizo ilibainika kuwa watumishi waliopo ni 597,396, mahitaji ni 1,036,762 na hivyo kuwa na upungufu wa 441,366 ambayo ni zaidi ya asilimia 73 ya Watumishi waliopo"

Aidha Kupitia Mfumo wa e-Mrejesho, Ofisi imepokea mrejesho jumla ya hoja 146,204, ambapo hoja 144,222 zilishughulikiwa na hoja 1,313 zinaendelea kushughulikiwa kupitia Idara na Vitengo.

"Utaratibu huu umeleta mafanikio makubwa ambapo uwajibikaji umeongezeka kwasababu ya urahisi wa ufuatiliaji kupitia mifumo ya TEHAMA, na wananchi wameongeza imani yao kwa Serikali kutokana na namna wanavyohudumiwa na kupata mrejesho kwa njia rafiki zinazowapunguzia gharama za usafiri kwa ajili ya ufuatiliaji"

Sanjari na hayo Katika kipindi cha mwaka 2021-2024 Taasisi ya UONGOZI imeandaa na kutoa mafunzo kwa zaidi ya viongozi 13,200 Barani Afrika,kupitia mafunzo haya Viongozi wameweza kuimarisha mahusiano kati yao na watendaji wengine, yameongeza uwezo wa timu kufanya kazi kwa pamoja na ufanisi, yameongeza uelewa wa kuchambua changamoto kwa kina na kuzitafutia ufumbuzi, Vilevile mafunzo haya yamewawezesha viongozi kuboresha usimamizi wa rasilimali za Serikali na rasilimaliwatu.

Aidha, pamoja na programu mbalimbali zinazotekelezwa na Taasisi hiyo ya UONGOZI kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kifini cha Aalto, mwaka 2022, Programu ya Uongozi kwa Wanawake ilizinduliwa inayohusisha wataalamu waandamizi wa masuala ya uongozi kutoka sehemu mbalimbali duniani.

TASAC YAWAJENGEA UWEZO MAWAKALA WA MELI, FORODHA NA WAKUSANYAJI NA WATAWANYAJI WA MIZIGO MWANZA.

TASAC YAWAJENGEA UWEZO MAWAKALA WA MELI, FORODHA NA WAKUSANYAJI NA WATAWANYAJI WA MIZIGO MWANZA.

NYONGO: SEKTA BINAFSI INA MCHANGO MKUBWA KWA TAIFA.

NYONGO: SEKTA BINAFSI INA MCHANGO MKUBWA KWA TAIFA.

NIDA KUSITISHA MATUMIZI YA NAMBA ZA UTAMBULISHO (NINs) KWA WASIOCHUKUA VITAMBULISHO VYAO.

NIDA KUSITISHA MATUMIZI YA NAMBA ZA UTAMBULISHO (NINs) KWA WASIOCHUKUA VITAMBULISHO VYAO.

NACHINGWEA YAANZA KUNUFAIKA NA VITUO VYA KUDHIBITI WANYAMAPORI WAHARIBIFU

NACHINGWEA YAANZA KUNUFAIKA NA VITUO VYA KUDHIBITI WANYAMAPORI WAHARIBIFU

JWTZ lajivunia Ushirikiano na Jeshi la Ujerumani

JWTZ lajivunia Ushirikiano na Jeshi la Ujerumani