

Mtangazaji maarufu wa kituo cha redio cha EFM, #DrKumbuka, ametoa kauli kali kuhusu kuvunjika kwa ndoa ya aliyekuwa msemaji wa klabu ya Simba, #HajiManara, na mrembo wake #Zaiylissa.
Akizungumza kwenye kipindi chake, #DrKumbuka amesema kuwa, “Mwanaume kurogwa kwenye mapenzi ni kitu cha kawaida kabisa. Wengine tunarogwa kimapenzi na hatujui.”
Kauli hiyo imekuja baada ya taarifa kusambaa mtandaoni zikionesha kuwa ndoa ya Manara na Zaiylissa imevunjika rasmi, huku wawili hao wakidaiwa kutoleana vitu vya ndani na kuacha nyumba ikiwa tupu.
Katika ushauri wake kwa Haji Manara, Dr Kumbuka alieleza kuwa endapo atahitaji kufunga ndoa tena, ni muhimu kutafuta mwanamke aliyekomaa kiakili, kihisia, na ambaye wanalingana kiumri.
“Ndoa si picha za Instagram, ni maisha halisi. Tafuta mtu ambaye amemaliza kila kitu – siyo bado yupo kwenye kipindi cha kujaribu maisha.” – aliongeza.
Hadi sasa, Manara hajatoa kauli rasmi kuhusu kilichojiri, lakini mashabiki wake mitandaoni wameendelea kumshauri apumzike kwanza kabla ya kurudi tena kwenye anga za mapenzi.
Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali: Waziri Simbachawene.
Waziri Simbachawene "Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali"
TASAC YAWAJENGEA UWEZO MAWAKALA WA MELI, FORODHA NA WAKUSANYAJI NA WATAWANYAJI WA MIZIGO MWANZA.
Awamu ya pili uboreshaji, uwekaji wazi wa dafatri la wapiga kura kuanza mei.
NYONGO: SEKTA BINAFSI INA MCHANGO MKUBWA KWA TAIFA.
PPAA yawanoa wazabuni Kanda ya Kaskazini
NIDA KUSITISHA MATUMIZI YA NAMBA ZA UTAMBULISHO (NINs) KWA WASIOCHUKUA VITAMBULISHO VYAO.
Shule mpya ya wavulana kugharimu zaidi ya bilioni tatu
WADAU WA UNUNUZI WAASWA KUZINGATIA MAADILI KAZINI
Chama Cha Mawakili wa Serikali kufanya mkutano Aprili 14-15 jijini Dodoma