Chama Cha Mawakili wa Serikali kufanya mkutano Aprili 14-15 jijini Dodoma | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

Chama Cha Mawakili wa Serikali kufanya mkutano Aprili 14-15 jijini Dodoma

Rais wa Chama Cha Mawakili wa Serikali Tanzania Amedeus Shayo amesema Chama hicho kinatarajia kufanya Mkutano wake Mkuu Aprili 14 hadi 15 mwaka huu Jijini Dodoma huku akiwataja zaidi ya Wanachama 2000 kuwa wanaweza kushiriki mkutano huo.

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
12 Apr 2025
Chama Cha Mawakili wa Serikali kufanya mkutano Aprili 14-15 jijini Dodoma

Ameeleza hayo Aprili 12,2025 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari
na kueleza kuwa Naibu Waziri Mkuu,Doto Biteko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano huo.

Rais huyo amesema mkutano huo utakuwa ni jukwaa la Mawakili kupata fursa ya kujaliana mambo ya kitaaluma na changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta hiyo.

Licha ya hayo ameeleza kwa Wanachama wa Chama hicho ni Mawakili na wanasheria wanaotoka kwenye taasisi za umma ambapo amedai kutakuwa na jukwaa la kitaaluma kujadili maslahi na maendeleo ya sekta ya Sheria na maadili kwenye Utumishi wa Umma.

Amesema hiyo itakuwa ni fursa na sehemu ya mafunzo kwa mawakili hao ambapo watajengeana uwezo.

Kutokana na hayo ametoa rai kwa Waajiri wote kuwaruhusu wafanyakazi wao na kuwawezesha kushiriki Mkutano na kueleza kuwa ushiriki huo ni muhimu kwa tathmini na mwelekeo kama walinzi wa uchumi.

SERIKALI KUTEKELEZA MFUKO WA UBUNIFU WA SAMIA “SAMIA INNOVATION FUND” WENYE THAMANI YA BIL 2.3

SERIKALI KUTEKELEZA MFUKO WA UBUNIFU WA SAMIA “SAMIA INNOVATION FUND” WENYE THAMANI YA BIL 2.3

SERIKALI YAENDELEA KUTOA MAFUNZO KWA WALIMU 70,657 UTEKELEZAJI MITAALA ILIYOBORESHWA, YAANZA MAPITIO SHERIA YA ELIMU

SERIKALI YAENDELEA KUTOA MAFUNZO KWA WALIMU 70,657 UTEKELEZAJI MITAALA ILIYOBORESHWA, YAANZA MAPITIO SHERIA YA ELIMU

BODI YA ITHIBATI  YATAMBULISHWA RASMI BUNGENI

BODI YA ITHIBATI YATAMBULISHWA RASMI BUNGENI

SERIKALI Imeendelea Kujenga na Kuboresha Miundombinu ya Viwanja vya Ndege

SERIKALI Imeendelea Kujenga na Kuboresha Miundombinu ya Viwanja vya Ndege

TUME YATAKA WANANCHI KUTAZAMA DAFTARI LA AWALI,KUHAKIKI TAARIFA ZAO

TUME YATAKA WANANCHI KUTAZAMA DAFTARI LA AWALI,KUHAKIKI TAARIFA ZAO