

Takwimu hapa nchini kwetu zinaonesha kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kimepungua kwa takribani asilimia 45 kutoka asilimia 14.8 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 8.1 mwaka 2022.
Takwimu hizo zinaonesha Mkoa wa Tabora unaongoza kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya Malaria kwa asilimia 23, ukifuatiwa na Mkoa wa Mtwara wenye kiwango cha maambukizi asilimia 20, Kagera asilimia 18, Shinyanga asilimia 16 na Mkoa wa Mara wenye asilimia 15.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya Mhe.Jenista Mhagama wakati akizungumza na waandishi wa habari Aprili 25 katika Siku ya Malaria Duniani kwenye Ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma.
Aidha amesema mikoa yenye kiwango cha chini cha maambukizi ya malaria kwa chini ya asilimia moja ni Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Dodoma, Songwe, Mwanza, Dar Es Salaam, Iringa, na Singida.
Aidha mafanikio ambayo yamepatikana kupitia Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika utekelezaji wa mikakati na afua mbalimbali za kupambana na ugonjwa wa Malaria hapa nchini ni kupungua kwa idadi ya wagonjwa waliothibitika kuwa na malaria kwa asilimia 45 kutoka wagonjwa milioni 6.0 mwaka 2020 hadi kufikia wagonjwa milioni 3.3 kwa mwaka 2024.
"Kupungua kwa idadi ya wagonjwa wanaolazwa kutokana na malaria kwa asilimia 33 kutoka wagonjwa 306,633 kwa mwaka 2020 hadi kufikia wagonjwa 206,453 mwaka 2024,kupungua kwa idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa malaria kwa asilimia 39 Kutoka vifo 2,460 kwa mwaka 2020 hadi kufikia vifo 1503 kwa mwaka 2024"
"Kuongezeka kwa Mikoa yenye kiwango cha maambukizi ya malaria chini ya asilimia moja, kutoka mikoa 5 mwaka 2020 hadi kufikia mikoa 6 kwa mwaka 2024 na kutoka Halmashauri 36 mwaka kwa 2020 hadi kufikia Halmashauri 51 kwa mwaka 2024. Mikoa hii ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida, Dodoma, Songwe, Iringa, Dar es Salaam na Mwanza"Amesema Mhe.Mhagama
Na kuongeza kuwa "Kuimarika kwa upatikanaji wa huduma za kupima ugonjwa wa malaria kwa kutumia kipimo kinachotoa majibu kwa haraka (mRDT) na dawa za kutibu malaria kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za Afya pamoja na kuimarika kwa upatikanaji wa dawa na bidhaa muhimu za malaria kwenye vituo vyote vya umma vya kutolea huduma ambapo upatikanaji wa bidhaa hizo ni zaidi ya asilimia 90"
Sanjari na hayo katika kuendelea kuboresha upatikanaji wa huduma za Malaria hapa nchini Wizara, imeimarisha na kuongeza msisitizo wa utekelezaji wa mikakati na afua zote za kupambana na malaria. Msisitizo mkubwa kwa sasa unawekwa kwenye uwekezaji katika udhibiti wa mbu waenezao malaria kwa njia jumuishi ikiwemo kutoa kipaumbele katika afua ya usimamizi na udhibiti wa mazingira ili kuzuia mbu kuzaliana kwa kusimamia usafi wa mazingira na unyunyiziaji wa viuadudu vya Kibaiolojia kwenye mazalia ya mbu.
"Napenda nichukue nafasi hii kuishukuru na kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita, kwa kutenga fedha, jumla ya Shilingi za Kitanzania bilioni 10 kwa ajili ya kununua viuadudu vya kibaiolojia kutoka kwenye Kiwanda cha viuadudu cha “Tanzania Biotech Products Ltd” kilichopo Kibaha Mkoani Pwani ili kuwezesha utekelezaji wa afua ya unyunyiziaji viuadudu kwenye Halmashauri zote 184 nchini"
"Utekelezaji wa afua hii huongeza kasi katika kupunguza mbu waenezao malaria na hatimaye maambukizi ya malaria nchini. Afua hii ikisimamiwa na kutekelezwa ipasavyo kupitia usimamizi wa Sheria ya Afya ya Jamii ya Mwaka 2009 na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004, itawezesha kudhibiti mbu waenezao magonjwa mbalimbali wakiwemo waenezao malaria"Amesisitiza
Siku ya Malaria Duniani mwaka huu 2025 imebeba kauli mbiu isemayo“Malaria Inatokomezwa na Sisi: Wekeza, Chukua Hatua - Ziro Malaria Inaanza na Mimi”
JWTZ YATANGAZA Nafasi Kwa Vijana wa Kitanzania.
WANANCHI LUHITA WALIA NA MAGUGU ZIWA BURIGI.
Wananchi wa mialo na ziwa waiomba serikali kuboresha miundombinu
RAIS SAMIA Ameziagiza Wizara ya Fedha,Kilimo Kukaa pamoja na BOT Kuja na Sera ya Taifa.
BODI YA TASAC:SERIKALI IMEWEKA MIKAKATI YA KUIMARISHA BANDARI ZOTE NCHINI.
JWTZ YATANGAZA Nafasi Kwa Vijana wa Kitanzania.
Wizara ya Afya Imesisitiza Umuhimu wa Elimu ya Afya ya Uzazi Kwa Watoto na Vijana.
BODI YA WAKURUGENZI TASAC YARIDHISHWA NA MABORESHO YA BANDARI ZA KEMONDO NA BUKOBA.
SINGIDA KASKAZINI WAIAMBIA TUME JIMBO LIITWE ILONGERO.
RAIS SAMIA Ameziagiza Wizara ya Fedha,Kilimo Kukaa pamoja na BOT Kuja na Sera ya Taifa.