RAIS DKT SAMIA ATAJWA SHUJAA WA UWEKEZAJI. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

RAIS DKT SAMIA ATAJWA SHUJAA WA UWEKEZAJI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametajwa kuwa Shujaa namba moja wa uwekezaji ambaye amejipambanua kuufanya uwekezaji kuwa ni moja ya nyenzo muhimu ya kuletea maendeleo nchini pamoja na kuongeza ajira.

Sophia kingimali.
By Sophia kingimali.
25 Jul 2024
RAIS DKT SAMIA ATAJWA SHUJAA WA UWEKEZAJI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametajwa kuwa Shujaa namba moja wa uwekezaji ambaye amejipambanua kuufanya uwekezaji kuwa  ni moja ya nyenzo muhimu ya kuletea maendeleo nchini pamoja na kuongeza ajira.

Hayo yamesemwa leo Julai 25,2024 Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) Gilead Teri wakati wa Mkutano kati ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Wawekezaji wa ndani 

lengo likiwa kuwaeleza uwekezaji na nafuu zilizowekwa na serikali ya awamu ya sita  chini ya Rais Dkt. Samia ili kuwarahisishia na kuwasaidia wao kuanza uwekezaji na biashara yao kwa urahisi

Teri amesema Juhudi za Rais samia zimepeleka kuwepo kwa ongezeko kubwa la uwekezaji wa ndani wa Tanzania ambapo kwa mwaka wa fedha wa mwaka 2023/24 kituo cha uwekezaji kilisajili miradi 707 ambayo ni ongezeko la asilimia 91 ukilinganisha kiradi 360 iliyosajiliwa mwaka wa fedha 2022/23

Aidha amesema kumekuwa na ongezekola wawekezaji wa ndani watanzania ambao wamesajili miradi yao TIC ambapo mwaka jana  kwa asilimia 38 huku watanzania walioshirikiana na wageni wabia ikiwa ni asilimia 20 hivyo asilimia 58 ya miradi ambayo imesajiliwa katika kituo cha uwekezaji Tanzania kwa mwaka uliopita ina mikono ya watanzania

“Hili ndiyo lengo la Rais samia alikuwa nalo alipobadilisha sheria ya uwekezaji mwaka 2022”

“Tangu kuanzishwa kwake kituo hiki mwaka 1997 hii ni kwa mara ya kwanza watanzania  wao wenyewe wananufaika na vivutio vya uwekezaji ambavyo viko 

katika kituo cha uwekezaji”

Kwa upande wake Mwekezaji wa Ndani, Amir Hamza amesema Rais samia amefanya kazi nzuri kuhamasisha uwekezaji  ambapo kupitia mkutano huo wamefanikiwa kuelewa sheria na kanuni mpya zilizobadilishwa tangu mwaka 2022 na ambazo zinalinda na kuhamasisha wawekezaji wa ndani kuweza kuwekeza katika nchi yao wenyewe.

Naye Meneja wa utafiti na mipango wa TIC, Anna Lyimo amesema takwimu za TIC zinaonyesha kwamba sekta ya usafirishaji ina asilimia kubwa ya wawekezaji wa ndani hivyo kumekuwa na maboresho ya serikali ambayo yamelenga katika kusaidia wawekezaji wa ndani kuweza kujisajili TIC na kuweza  kunufaika na vivutio vya kodi ambavyo serikali inavitoa.

Sambamba na hayo TIC imemtaja Shujaa wa pili mtanzania ambaye ni mwekezaji wa ndani aitwaje Amir Hamza aliyeanza kufanya uwekezaji tangu mwaka 1994 ambapo katikaKituo cha uwekezaji ni shujaa wanaemthamini.

JESHI LA POLISI LATOA TAMKO UTATA WA KIFO CHA MSANII MANDOJO.

JESHI LA POLISI LATOA TAMKO UTATA WA KIFO CHA MSANII MANDOJO.

RC CHALAMILA AIPONGEZA TPDC KWA KUTOA ELIMU YA UTUNZAJI MIUNDOMBINU YA SHIRIKA HILO.

RC CHALAMILA AIPONGEZA TPDC KWA KUTOA ELIMU YA UTUNZAJI MIUNDOMBINU YA SHIRIKA HILO.

Asali ya Tanzania Yapata Kibali Kuuzwa China.

Asali ya Tanzania Yapata Kibali Kuuzwa China.

BENKI YA BIASHARA TANZANIA (TCB) KUSHIRIKIANA NA  BUNGE LA TANZANIA KUWAINUA WAJASIRIAMALI NCHINI.

BENKI YA BIASHARA TANZANIA (TCB) KUSHIRIKIANA NA BUNGE LA TANZANIA KUWAINUA WAJASIRIAMALI NCHINI.

REA YAAHIDI KUENDELEA KUWAWEZESHA WAENDELEZAJI BINAFSI WA UMEME NCHINI.

REA YAAHIDI KUENDELEA KUWAWEZESHA WAENDELEZAJI BINAFSI WA UMEME NCHINI.