Katika jitihada za kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi za kifedha na mihimili ya Serikali, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB),Adam Mihayo, amemtembelea na kuzungumza na Spika wa Bunge la Tanzania,Dkt Tulia Ackson.
Mihayo ameambatana na Mkurugenzi wa Biashara za Wateja Wadogo na wa Kati wa benki hiyo Lilian Mtali, katika ziara hiyo ambayo inafungua ukurasa mpya wa ushirikiano baina ya Benki ya TCB na Bunge la Tanzania katika kuwainua wajasiriamali wadogo na wa kati nchini.
Mazungumzo na kiongozi huyo wa Bunge linaloundwa na wabunge 393 kutoka majimbo 239 yamejikita katika masuala nyeti yanayohusu majimbo mbalimbali katika jitihada za kuendelea kuwainua wajasiriamali wadogo na wa kati.
Wakitambua mchango mkubwa wa kundi hili katika ukuaji uchumi na uzalishaji wa ajira mpya, mazungumzo yao yamejikita katika mpango wa utoaji wa mikopo yenye riba nafuu kwa wajasiriamali. Miradi hii itasaidia kukuza na kuchochea mazingira ya biashara kwa wajasiriamali pamoja na biashara zao.
“Lengo letu sio kutoa jibu moja kwa nchi nzima. Huwezi kuwa na suluhisho moja kwa watu wote, ndiyo maana ni muhimu kuwasikiliza wadau wengi iwezekanavyo. Njia hii itatusaidia kutoa majibu yatakayokidhi mahitaji ya wajasiriamali kulingana maeneo wanayoishi hata wale walioko vijijini,” amesema Mihayo.
Kwa upande wake, Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson amebainisha umuhimu wa ushirikiano huo na kusisitiza wajibu wa Bunge katika kutunga sera zinazowezesha maendeleo ya wajasiriamali na kuhakikisha kwamba biashara zao zinapata rasilimali zinazohitajika ili kukua.
“Maendeleo ya wajasiriamali ni muhimu kwa ukuaji uchumi wa taifa letu, kupitia ushirikiano huu na Benki ya TCB, tunaweza kutengeneza mazingira yatakayowezesha ukuaji wa biashara,“ amesema.
Kikao hicho kimehitimishwa kwa azimio la ushirikiano wa pamoja na kuendelea kubuni nyanja mbalimbali za ushirikiano lengo likiwa kuinua sekta ya wajasiriamali
DKT. BITEKO ataka TANESCO kuongeza kasi utekelezaji miradi ya umeme wa gridi
Ndaisaba azidi kumwaga Fedha katika sekta ya Michezo Wilayani Ngara
"Hatutawavumilia wanaochochea Machafuko Nchini" Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan
(LHRC) chatoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama Kufuatia mauaji ya watoto watatu wa familia moja
TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini
VIJANA NDIO WALINZI WA NCHI HII: MEJA JENERALI RAJABU MABELE
BRIGEDIA Jenerali Ngata Apongezwa uongozi makini SUMAJKT
VIONGOZI SOKO LA MACHINGA DODOMA WASIMAMISHWA KUPISHA UCHUNGUZI
TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini
(LHRC) chatoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama Kufuatia mauaji ya watoto watatu wa familia moja