Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemuhakikishia Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi itahakikisha inasimamia kikamilifu ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami inayounganisha Mkoa wa Kagera na Kigoma kupitia Kibondo kukamilika ifikapo mwezi Oktoba, 2024.
Bashungwa amezungumza hayo Agosti 09, 2024 Wilayani Misenyi Mkoani Kagera wakati akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Nchimbi kufuatia maelekezo aliyoyatoa Mkoani Kigoma kwa Wizara ya Ujenzi.
“Mheshimiwa Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi tunakuhakikishia maelekezo uliyoyatoa Mkoani Kigoma ya kukamilisha barabara inayounganisha Mkoa wa Kagera na Kigoma, tunakuahidi ikifika mwezi wa kumi barabara ya kutoka Kagera hadi kibondo itakuwa imeshakamilika”, amesema Bashungwa.
Bashungwa ameahidi kushughulikia fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa barabara ya Mabamba - Kibondo pamoja na malipo ya Mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa barabara ya Kibondo Townlink Mkoani Kigoma.
Kuhusu Mkoa wa Kagera, Waziri Bashungwa ameeleza kuwa Serikali inaendelea kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuunganisha Wilaya ya Misenyi na Bukoba vijijini kwa barabara ya kiwango cha lami kuanzia Kyaka - Katoro hadi Kyetema (km 60.7) ambapo katika Bajeti ya Serikali ya mwaka 2024-2025 itaanza ujenzi wa barabara hiyo kipande cha kilometa 10 pamoja na ujenzi wa Daraja la Kalebe.
Aidha, Bashungwa amesema Serikali inaendelea na utekelezaji wa miundombinu ya barabara na madaraja ikiwa ni pamoja na upanuzi wa barabara njia nne kuanzia Rwamishenye Roundabout hadi Stendi Mpya ya Bukoba Mjini, barabara ya Karagwe - Benaco (km 60) pamoja na ukarabati wa barabara ya Lusahunga - Rusumo (km 92).
Bashungwa ameeleza kuwa Serikal inafungua barabara ya Nyabihanga - Minziro kwa kuanza na kilometa sita kuanzia Mtukula mpaka Minziro na hivi sasa Wakandarasi wapo katika barabara hiyo kuendelea kurekebisha maeneo yote korofi.
Kuhusu ufungaji wa taa za barabarani katika maeneo ya Kyaka, Bunazi na Mtukula, Bashungwa ameeleza kuwa TANROADS wanakamilisha hatua za manunuzi kwa ajili ya kufunga taa hizo ikiwa ni ombi la Mbunge wa Jimbo la Nkenge Wilayani Misenyi, Dkt. Florent Kyombo.
Naye, Mbunge wa Jimbo la Nkenge Wilayani Misenyi Dkt. Florent Kyombo ametoa ombi la Mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa barabara ya Bunazi - Kagera Sugar hadi njia panda ya Kitengule kwa kiwango cha lami kulipwa malipo ya awali ili ujenzi wa barabara hiyo uweze kuanza.
DKT. BITEKO ataka TANESCO kuongeza kasi utekelezaji miradi ya umeme wa gridi
Ndaisaba azidi kumwaga Fedha katika sekta ya Michezo Wilayani Ngara
"Hatutawavumilia wanaochochea Machafuko Nchini" Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan
(LHRC) chatoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama Kufuatia mauaji ya watoto watatu wa familia moja
TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini
VIJANA NDIO WALINZI WA NCHI HII: MEJA JENERALI RAJABU MABELE
BRIGEDIA Jenerali Ngata Apongezwa uongozi makini SUMAJKT
VIONGOZI SOKO LA MACHINGA DODOMA WASIMAMISHWA KUPISHA UCHUNGUZI
TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini
(LHRC) chatoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama Kufuatia mauaji ya watoto watatu wa familia moja