Chama cha Mapinduzi CCM kimeshinda nafasi 12,150 (99.01%) kwenye nafasi ya Wenyeviti wa Vijiji katika Vijiji vyote 12271 vilivyofanya Uchaguzi huku CHADEMA ikishinda nafasi 97 (0.79%).
Akitangaza matokeo ya jumla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa jana usiku , Waziri wa TAMISEMI, Mohammed Mchengerwa amesema ACT Wazalendo imeshinda nafasi 11 (0.09%) , CUF imeshinda nafasi 10, NCCR , UMD na ADC wameshinda nafasi moja kila Chama.
“Vijiji tisa havijafanya Uchaguzi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo vya Wagombea baada ya uteuzi” — Mchengerwa.
Chama cha Mapinduzi 'CCM' Pia kimeshinda nafasi 62728 sawa na asilimia 98.26 kwenye nafasi ya Wenyeviti wa Vitongoji Nchini ikifuatiwa na CHADEMA ambayo imeshinda nafasi 853 (1.34%) katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
ACT Wazalendo imeshinda nafasi 150 (0.23%) , CUF imeshinda nafasi 78, NCCR nafasi 10, UDP nafasi 6, UMD nafasi mbili na ADC wameshinda nafasi moja.
Aidha amesema Vitongoji nane wagombea wake walifariki dunia uchaguzi utarudiwa ambapo 37 havikufanya uchaguzi tarehe 27 Novemba, 2024. Kati ya hivyo, vitongoji havikufanya uchaguzi kwa kuwa wagombea wake walifariki baada ya zoezi la uteuzi.
" Wagombea hao walitoka katika Halmashauri za wilaya za Kilwa (2), Nanyumbu (1), Itilima (1), Ikungi (1), Manyoni (1), Uyui (1) na Mbarali (1),”amesema Mchengerwa.
Ambapo amesema vitongoji 29 havikufanya uchaguzi kutokana na sababu mbalimbali. Vitongoji 12 vitarudia uchaguzi kwa kuwa matokeo ya wagombea yalifungana. Vilevile, vitongoji 9 vitarudia chaguzi kutokana na wagombea pekee kutopata kura za kutosheleza.
Aidha, amesema katika mtaa mmoja wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga hakupatikana mshindi kwa sababu kura za wagombea wawili zilifungana.
KOREA KASKAZINI YAWANASA ‘SNIPER’ UKRAINE, YADAI RUSSIA INAWAUA MAJERUHI
MAREKANI HALI TETE, MOTO WAUA 16 LOS ANGELES, UPEPO WATARAJIWA KUONGEZEKA
Ajali ya gari yajeruhi mamia ya watu Ufaransa
Maria Sarungi atekwa Kenya wasiojulikana watajwa
BENKI KUU YAWAGEUKIA WATENGENEZAJI, WAUZAJI ‘PUTTY’