Mnamo tarehe 11/08/2024 majira ya saa 12:00 mchana katika Hospitali ya rufaa Mkoa wa Dodoma, JOSEPH FRANCIS MICHAEL maarufu kama MANDOJO, mwenye Miaka 46, Mkurya na Mwanamuziki, Mkazi wa Nzuguni B, alifariki akiwa anaendelea na matibabu.
Hayo yameelezwa na Kaimu Kamanda Mkoa wa Dodoma ANANIA. AMO SACP wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utata wa kifo cha msanii huyo pamoja na matukio ya kutisha yanayoendelea jijini hapa.
Aidha amesema tarehe 11/08/2024 majira ya 05:00 alfajiri JOSEPH FRANCIS MICHAEL (MANDOJO) alikutwa ndani ya uzio wa Kanisa Katoliki Parokia ya Watakatifu wote lililopo Nzuguni B huku akiwa amejificha katika banda la mbwa.
Aidha ameongeza akiwa kwenye banda hilo mlinzi wa eneo hilo aitwaye RAPHAEL KENETH NDAMAHNUWA, miaka 26, Mgogo, mkazi wa Nzuguni B alisikia mbwa wanabweka kwa nje ya kibanda chao na alipofika eneo hilo aligundua kuna mtu amejifungia ndani ya chumba kimojawapo cha banda hilo lenye vyumba viwili hivyo alifungia mbwa kwenye chumba kimoja na kuanza kupambana na mtu aliyejifungia ndani na aliomba msaada kwa waumini walioenda kanisani kwa ajili ya ibada ya misa ya kwanza ambapo walifanikiwa kumdhibiti na Polisi walifika eneo la tukio na kumchukua kumpeleka Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia RAPHAEL KENETH NDAMAHNUWA, miaka 26, Mgogo, Mlinzi, mkazi wa Nzuguni B kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo huku mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na daktari ili kubaini chanzo cha kifo chake.
Katika tukio lingine lililotokea tarehe 10/08/2024 majira ya saa nne usiku huko kitongoji cha Juhudi, Kijiji na Kata ya Ibihwa, Tarafa na Wilaya ya Bahi, Mkoa wa Dodoma watu wawili ambao ni FRANCO FILBERT MTASOKA, Miaka 29, Mhaya, Dereva, Mkazi wa Kisasa na RAMADHAN ABEID, Miaka 27, Mzigua waliuawa kwa kushambuliwa sehemu mbalimbali za miili yao na kisha kuchomwa moto ndani ya gari namba T. 583 BEW aina ya Toyota Cresta na wananchi waliojichukulia sheria mkononi.
"Watu hao walifika katika kijiji cha Ibihwa majira ya saa mbili usiku wakitokea Dodoma Mjini wakiwa na gari namba T. 583 BEW aina ya Toyota Cresta wakielekea Kitongoji cha Tea, Kijiji cha Ilindi, Kata ya Ilindi, Wilaya ya Bahi kwa ajili ya kupeleka token ya micheo ya kubahatisha yaani bonanza" Amesema
Aidha uchunguzi wa awali umebaini kwamba chanzo cha tukio hilo ni baada ya baadhi ya wananchi kuona gari lililoegeshwa usiku katika eneo la wazi njia ya umeme mkubwa na ndani ya gari hilo kukiwa na watu watatu wasio fahamika na wakiwa wamekaa kwa muda mrefu wakawatilia mashaka kwamba kuna matukio ya wizi wa watoto maeneo mengine ndipo wakaanza kukusanyana na kuwashambulia na kuwaua kisha kuwachoma kwa moto kwenye gari,miili ya marehemu imehifadhiwa katika kituo cha afya Bahi ikisubiri uchunguzi wa daktari.
Sanjari na hayo ametoa wito kwa wananchi Mkoa wa Dodoma kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani kufanya hivyo ni kinyume na sheria za nchi na amewasihi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwenye vyombo husika ili wachukuliwe hatua stahiki.
DKT. BITEKO ataka TANESCO kuongeza kasi utekelezaji miradi ya umeme wa gridi
Ndaisaba azidi kumwaga Fedha katika sekta ya Michezo Wilayani Ngara
"Hatutawavumilia wanaochochea Machafuko Nchini" Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan
(LHRC) chatoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama Kufuatia mauaji ya watoto watatu wa familia moja
TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini
VIJANA NDIO WALINZI WA NCHI HII: MEJA JENERALI RAJABU MABELE
BRIGEDIA Jenerali Ngata Apongezwa uongozi makini SUMAJKT
VIONGOZI SOKO LA MACHINGA DODOMA WASIMAMISHWA KUPISHA UCHUNGUZI
TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini
(LHRC) chatoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama Kufuatia mauaji ya watoto watatu wa familia moja