BoT YAWATAKA TAMFI NA TAMIU KUBORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

BoT YAWATAKA TAMFI NA TAMIU KUBORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA.

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Emanuel Tutuba amevitaka Chama cha Taasisi ndogo za Fedha Tanzania (TAMFI) na Umoja wa Taasisi za Fedha Ndogo Tanzania (TAMIU) kuweka mazingira wezeshi yanayoboresha ubora na upatikanaji wa huduma za fedha.

Sophia Kingimali.
By Sophia Kingimali.
01 Jul 2025
BoT YAWATAKA TAMFI NA TAMIU KUBORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA.

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Emanuel Tutuba amevitaka Chama cha Taasisi ndogo za Fedha  Tanzania (TAMFI) na Umoja wa Taasisi za Fedha Ndogo Tanzania (TAMIU) kuweka mazingira wezeshi yanayoboresha ubora na upatikanaji wa huduma za fedha.

Hayo ameyasema leo wakati wa utiaji saini hati ya makubaliano (MoU) kwa ajili ya kuanzisha mfumo mpya wa kujisimamia kwa taasisi za fedha ndogo za daraja la pili pamoja na vyama vyao.

Amesema Lengo kuu la makubaliano hayo ni kuimarisha na kuhalalisha shughuli za taasisi hizo kote nchini.

Makubaliano hayo yamesainiwa kwa ushirikiano na Chama cha Taasisi za Fedha Ndogo Tanzania (TAMFI) na Umoja wa Taasisi za Fedha Ndogo Tanzania (TAMIU), na yanaashiria uzinduzi rasmi wa mpango wa udhibiti ulioafikiwa Machi mwaka huu.

Gavana Tutuba, amesema kuwa lengo la makubaliano hayo ni kuunda mazingira bora ya sera na sheria kwa ajili ya sekta ndogo ya fedha  inayokuwa kwa kasi hapa nchini.

“Hii ni sehemu ya jitihada zetu za pamoja kuanzisha mazingira rafiki ya sera na kisheria kwa sekta ndogo ya fedha , ambayo imekua kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni.

“Kwa kuongezeka kwa idadi ya watoa huduma wa daraja la pili, ni wajibu wetu kuhakikisha kuwepo kwa mazingira wezeshi yanayoboreshwa ubora na upatikanaji wa huduma hizi. Hatua hii ni muhimu katika kuongeza ufanisi na uwajibikaji katika sekta ya huduma za kifedha,” amesema Gavana Tutuba.

Aidha ameongeza kuwa BoT ilianzisha kanuni za kusimamia taasisi za fedha ndogo mwaka 2019, ikiwa na lengo la kuziorodhesha na kuzisajili ili kulinda watumiaji wa huduma hizo.

Amesema Kupitia makubaliano hayo mapya, TAMFI na TAMIU watakuwa na jukumu la kusimamia mwenendo wa taasisi wanachama wao, kuhakikisha wanazingatia maadili bora na viwango vya kitaaluma ili kukuza uaminifu katika sekta hiyo.

Amesema Sekta ya fedha ndogo ya daraja la pili imekua kwa kasi, ikiwa na taasisi zaidi ya 2,600 zinazofanya kazi kote nchini. Taasisi hizi zina mchango mkubwa katika maendeleo, hasa kwa watu binafsi na wafanyabiashara wasioweza kupata huduma za kibenki za kawaida.

Hata hivyo, licha ya umuhimu wake, sekta hii bado inakabiliwa na changamoto kadhaa, ikiwemo kiwango kidogo cha elimu ya fedha. Kutokuwepo kwa uelewa huu mara nyingi husababisha watu kukopa bila maandalizi, jambo linalowaumiza kifedha.

“Watu wengine wanachukua mikopo bila ya kuwa na malengo mtu akiona tu bango limeandikwa ‘Mikopo Inapatikana’ bila kupanga ataingia na kuchukua mkopo hii si tabia nzuri ya kifedha,” ameeleza Gavana Tutuba.

Ameongeza kuwa chini ya makubaliano haya, TAMFI na TAMIU pia watatakiwa kuanzisha na kusimamia mifumo bora ya kushughulikia malalamiko kuanzia ngazi za awali, ili kuhakikisha huduma zinazotolewa zinatimiza malengo yaliyokusudiwa.

Aidha, ametoa rai kwa taasisi zote za fedha ndogo za daraja la pili kujiunga na mojawapo ya vyama viwili—TAMFI au TAMIU—ndani ya kipindi cha miezi sita kuanzia tarehe ya tangazo hilo.

“Lengo ni kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizi. Baada ya kipindi hicho, taasisi yoyote itakayoshindwa kujiunga na mojawapo ya vyama hivyo, itapokonywa leseni yake,” amesema Gavana Tutuba.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TAMFI,  Devotha Minzi, amesema  mpango huo kama ni hatua kubwa ya mafanikio kwa sekta ya fedha ndogo, akisema utaongeza kwa kiasi kikubwa ufanisi na uwajibikaji.

SHERIA ZILIZOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI KUTOKA MWEZI AGOSTI.

SHERIA ZILIZOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI KUTOKA MWEZI AGOSTI.

WAZIRI KIKWETE AIPONGEZA OFISI YA MSAJILI WA HAZINA.

WAZIRI KIKWETE AIPONGEZA OFISI YA MSAJILI WA HAZINA.

NISHATI SAFI YA KUPIKIA NI AJENDA YA DUNIA, WIZARA INAITEKELEZA KWA VITENDO - DKT. KAZUNGU.

NISHATI SAFI YA KUPIKIA NI AJENDA YA DUNIA, WIZARA INAITEKELEZA KWA VITENDO - DKT. KAZUNGU.

UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.

UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.

UKUAJI WA UCHUMI WA TANZANIA BARA UNAKADILIWA KUFIKIA ASILIMIA 5.8:BoT.

UKUAJI WA UCHUMI WA TANZANIA BARA UNAKADILIWA KUFIKIA ASILIMIA 5.8:BoT.