MHANDISI SEFF AMTAKA MKANDARASI UJENZI WA BARABARA YA KASULU-KABANGA-MUYAMA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

MHANDISI SEFF AMTAKA MKANDARASI UJENZI WA BARABARA YA KASULU-KABANGA-MUYAMA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff amemtaka Mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kasulu-Kabanga-Muyama yenye urefu wa Km. 12.5, Salum Motors Transport Ltd (SAMOTA) kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa muda uliopangwa.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
25 Jul 2024
MHANDISI SEFF AMTAKA MKANDARASI UJENZI WA BARABARA YA KASULU-KABANGA-MUYAMA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff amemtaka Mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kasulu-Kabanga-Muyama yenye urefu wa Km. 12.5,  Salum Motors Transport Ltd (SAMOTA) kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa muda uliopangwa.

Mhandisi Seff ameyasema hayo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya ujenzi na matengenezo ya barabara zilizo chini ya TARURA katika Mkoa wa Kigoma.

Mhandisi Seff amesema kuwa mkandarasi huyo anapaswa kuongeza muda wa kufanya kazi na kuhakikisha ubora wa kazi unazingatiwa na endapo itaonekana mradi huo unaendelea kusuasua basi hatosita kumchukulia hatua za kimkataba.

Aidha, Mhandisi Seff amemuagiza Mkandarasi  huyo pamoja na Mhandisi Msimamizi Kampuni ya Ambicon kutatua changamoto ya upatikanaji wa kokoto zenye ubora unaotakiwa ili kazi ya uwekaji wa tabaka la lami ngumu uwe umekamilika ifikapo tarehe 31 Agosti, 2024.

Awali Mkurugenzi wa SAMOTA, Bw. Ally Abdallah ameeleza kuwa changamoto kubwa wanayoipitia ni upatikanaji wa  kokoto zenye ubora kwa ajili ya tabaka la juu la lami ambapo wanaendelea na upimaji wa ubora wa kokoto katika maabara na kuendelea kutafuta mwamba utakaotoa kokoto zenye ubora zaidi.

JESHI LA POLISI LATOA TAMKO UTATA WA KIFO CHA MSANII MANDOJO.

JESHI LA POLISI LATOA TAMKO UTATA WA KIFO CHA MSANII MANDOJO.

RC CHALAMILA AIPONGEZA TPDC KWA KUTOA ELIMU YA UTUNZAJI MIUNDOMBINU YA SHIRIKA HILO.

RC CHALAMILA AIPONGEZA TPDC KWA KUTOA ELIMU YA UTUNZAJI MIUNDOMBINU YA SHIRIKA HILO.

Asali ya Tanzania Yapata Kibali Kuuzwa China.

Asali ya Tanzania Yapata Kibali Kuuzwa China.

BENKI YA BIASHARA TANZANIA (TCB) KUSHIRIKIANA NA  BUNGE LA TANZANIA KUWAINUA WAJASIRIAMALI NCHINI.

BENKI YA BIASHARA TANZANIA (TCB) KUSHIRIKIANA NA BUNGE LA TANZANIA KUWAINUA WAJASIRIAMALI NCHINI.

REA YAAHIDI KUENDELEA KUWAWEZESHA WAENDELEZAJI BINAFSI WA UMEME NCHINI.

REA YAAHIDI KUENDELEA KUWAWEZESHA WAENDELEZAJI BINAFSI WA UMEME NCHINI.