Vijiji 151 vimebaki nchi nzima kupata huduma ya umeme - Kapinga | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

Vijiji 151 vimebaki nchi nzima kupata huduma ya umeme - Kapinga

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga amesema Vijiji 151 tu nchi nzima ndio ambavyo bado havijafikiwa na huduma ya umeme kati ya Vijiji zaidi ya 12,000 ambapo wilayani Ludewa mkoani Njombe vimebaki Vijiji nane.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
20 Jul 2024
Vijiji 151 vimebaki nchi nzima kupata huduma ya umeme - Kapinga

Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga amesema Vijiji 151 tu nchi nzima ndio ambavyo bado havijafikiwa na huduma ya umeme kati ya Vijiji zaidi ya 12,000 ambapo wilayani Ludewa mkoani Njombe vimebaki Vijiji nane.

Mhe. Kapinga ameyasema hayo jana 19 Julai 2024 wakati wa ziara ya kikazi katika Vijiji vya Lubonde na Maweni wilayani Ludewa mkoani Njombe akikagua miradi ya nishati.

Wakati wa ziara hiyo Mhe. Kapinga alifanikisha kuingiwa makubaliano kati ya Kampuni binafsi ya kuzalisha umeme ya Madope iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ya kukabidhi miundombinu ya kusafirisha na kusambaza umeme kwa Shirika hilo baada ya kusainiwa kwa mkataba kati ya pande hizo mbili.

Kapinga amesema kuwa Serikali inathamini kazi kubwa inayofanywa na Kanisa Katoliki kwa kushirikiana na Serikali kwenye uwekezaji katika sekta mbalimbali.

Kwa upande wake Askofu wa jimbo la Njombe Eusebio Kyando ameupongezi Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa ushirikiano wao na kutoa fedha zilizowezesha kufanikisha mradi huo.

Kampuni ya Madope ni miongoni mwa wazalishaji wadogo wa umeme katika Wilaya ya Ludewa ambayo inamilikiwa kwa asilimia 55 na Kanisa Katoliki jimbo la Njombe

JESHI LA POLISI LATOA TAMKO UTATA WA KIFO CHA MSANII MANDOJO.

JESHI LA POLISI LATOA TAMKO UTATA WA KIFO CHA MSANII MANDOJO.

RC CHALAMILA AIPONGEZA TPDC KWA KUTOA ELIMU YA UTUNZAJI MIUNDOMBINU YA SHIRIKA HILO.

RC CHALAMILA AIPONGEZA TPDC KWA KUTOA ELIMU YA UTUNZAJI MIUNDOMBINU YA SHIRIKA HILO.

Asali ya Tanzania Yapata Kibali Kuuzwa China.

Asali ya Tanzania Yapata Kibali Kuuzwa China.

BENKI YA BIASHARA TANZANIA (TCB) KUSHIRIKIANA NA  BUNGE LA TANZANIA KUWAINUA WAJASIRIAMALI NCHINI.

BENKI YA BIASHARA TANZANIA (TCB) KUSHIRIKIANA NA BUNGE LA TANZANIA KUWAINUA WAJASIRIAMALI NCHINI.

REA YAAHIDI KUENDELEA KUWAWEZESHA WAENDELEZAJI BINAFSI WA UMEME NCHINI.

REA YAAHIDI KUENDELEA KUWAWEZESHA WAENDELEZAJI BINAFSI WA UMEME NCHINI.