NYUMBA 2,500 ZAKAMILIKA MSOMERA, USAMBAZAJI WA UMEME WAFIKIA ASILIMIA 98, MIUNDOMBINU MINGINE MBIONI KUKAMILIKA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Utalii

NYUMBA 2,500 ZAKAMILIKA MSOMERA, USAMBAZAJI WA UMEME WAFIKIA ASILIMIA 98, MIUNDOMBINU MINGINE MBIONI KUKAMILIKA.

Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) tarehe 21 Novemba, 2024 imefanya ziara ya kikazi kijiji cha Msomera Handeni mkoani Tanga kukagua utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwa ajili ya wananchi wa Ngorongoro wanaoendelea kuhamia eneo hilo.

Kassim Nyaki, Msomera Tanga.
By Kassim Nyaki, Msomera Tanga.
22 Nov 2024
NYUMBA 2,500 ZAKAMILIKA MSOMERA, USAMBAZAJI WA UMEME WAFIKIA ASILIMIA 98, MIUNDOMBINU MINGINE MBIONI KUKAMILIKA.

Akiongoza bodi hiyo Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi NCAA Jenerali Venance Mabeyo (mstaafu) amezipongeza Sekta zote zinazohusika kutekeleza mradi huo kijiji cha Msomera kwa kukamilisha Nyumba 2500, ujenzi wa miundombinu ya Maji, mawasiliano, barabara, minada, majosho, kituo cha kuuzia maziwa, shule, zahanati, shule, kutenga maeneo ya malisho na miundombinu mingine kijijini hapo.

"Tumetembelea eneo la Block F ambapo nyumba 1,000 zimekamilishwa katika awamu ya kwanza iliyohusisha ujenzi wa Nyumba 5,000, kitalu hiki pekee kuna matenki matatu ya maji yenye ujazo la lita laki 3 kwa kila moja, tenki lingine la ujazo wa lita laki 650,000 linajengwa, hii inathibitisha kuwa wananchi wanaopisha shughuli za uhifadhi Ngorongoro wakija hapa watafurahia maisha yao" ameongeza Jenerali Mabeyo.

Akiambatana na Bodi ya Wakurugenzi NCAA, mkuu wa Wilaya ya Handeni Wakili Albert Msando amewahakikishia wananchi wa Ngorongoro wanaohamia eneo hilo kuwa hali ya usalama  ni shwari, nyumba zimekamilika, huduma za kijamii zipo katika eneo lote la Msomera na huduma zingine zinaendelea kujengwa ili kukidhi mahitaji ya wananchi wanaohamia.

Kaimu Kamanda wa Operesheni wa Ujenzi wa Nyumba 5000 za Msomera, Kitwai na Saunyi Luteni Kanali Edward Mwanga ameieleza bodi hiyo kuwa SUMA JKT wamekamilisha ujenzi wa Nyumba zote 2500 kwa asilimia 100 zikiwa katika kiwango cha kisasa na ubora wa hali ya juu na wako tayari kwa kazi ya ujenzi wa Nyumba zingine 2,500 ambapo Nyumba 1000 zitajengwa kijiji cha Saunyi Wilaya ya Kilindi na Nyumba 1500 zitajengwa kijiji cha kitwai B Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara

Mwakilishi wa Kamishna wa Uhifadhi NCAA, SACC Gloria Bideberi amesema kuwa uongozi wa NCAA utahakikisha kuwa kazi ya uelimishaji na uhamasishaji kwa wananchi inaendelea kwa kasi zaidi ili wananchi waliopo Ngorongoro waendelee kuhamia Msomera. Ameongeza kuwa  kaya takribani 30 kutoka Ngorongoro zitahamishiwa katika kijiji hicho mwisho wa mwezi Novemba,2024 baada ya kukamilisha uthamini na kulipwa stahiki zao kwa mujibu wa sheria.

TANZANIA NA UTURUKI KUSHIRIKIANA SEKTA YA MALIASILI NA UTALII

TANZANIA NA UTURUKI KUSHIRIKIANA SEKTA YA MALIASILI NA UTALII

TUKIFANYA KAZI KWA PAMOJA TUTAPATA WATALII WA KUTOSHA UKANDA WA KARIBE NA MAENEO JIRANI - BALOZI POLEPOLE

TUKIFANYA KAZI KWA PAMOJA TUTAPATA WATALII WA KUTOSHA UKANDA WA KARIBE NA MAENEO JIRANI - BALOZI POLEPOLE

WACUBA WAVUTIWA NA HIFADHI YA NGORONGORO

WACUBA WAVUTIWA NA HIFADHI YA NGORONGORO

BAROZI DKT CHANA AFUNGA ONESHO LA S!TE ASIFU MAFANIKIO YALIYOPATIKANA.

BAROZI DKT CHANA AFUNGA ONESHO LA S!TE ASIFU MAFANIKIO YALIYOPATIKANA.

KILI MEDIAIR WABORESHA HUDUMA KUVUTIA UTALII NCHINI.

KILI MEDIAIR WABORESHA HUDUMA KUVUTIA UTALII NCHINI.