KAMPUNI ya inayojihusisha na ukoaji katika vivutio vya utalii Nchini, Kili MediAir Aviation katika kuboresha huduma zake inatarajia kuzindua kifurushi kipya cha huduma chenye lengo la kusaidia watalii wa ndani na nje ili kuweza kufarahia Mlima Kilimanjaro bila kuhofia usalama wa afya zao.
KAMPUNI ya inayojihusisha na ukoaji katika vivutio vya utalii Nchini, Kili MediAir Aviation katika kuboresha huduma zake inatarajia kuzindua kifurushi kipya cha huduma chenye lengo la kusaidia watalii wa ndani na nje ili kuweza kufarahia Mlima Kilimanjaro bila kuhofia usalama wa afya zao.
Akizungumza leo Oktoba 12, 2024, kwenye maonyesho ya nane ya S!TE yanayoendelea katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam Daktari wa Uokozi wa Kampuni hiyo, Jimmy Daniel amesema katika kutimiza miaka mitatu ya kampuni hiyo tangu kuanzishwa kwake wamejipanga kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa watalii ili kuendelea kuwavutia kutembelea vivutio vilivyopo nchini.
Kuna watu wengi tunakutana nao wanatamani kufanya utalii mfano kupanda mlima Kilimanjaro ila umri au maradhi na vitu vingine vimekuwa changamoto wanashindwa kutimiza lengo lao sasa sisi Kili MediAir tumekuja na kifurushi ambacho kinamsaidia mtalii aweze kufika ajionee mwenyewe kwa kutumia Helkopta katika maeneo ambayo mtu wa kawaida asingeweza,"amesema.
Ameongeza kuwa endapo mtalii ambae anatarajia kufika mlima Kilimanjaro wanampa daktari pamoja na mtu wa kuwa na yeye wakati unafanya safari hiyo
"Tumejidhatiti kuongeza wigo katika kutoa huduma kwani hatufanyi tu uokozi bali tunatoa huduma kwa wanaofanya utaliii wa anga"Amesema.
Aidha amesema kampuni hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa kwani watu wengi wanajua kuwa huduma yao ni uokozi hivyo wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili watambue huduma zinazotolewa na kampuni hiyo.
"Changamoto ni kuwahudumia watu wote na watalii ambao wana bima ya afya wanaweza kutumia katika kuwasaidia Kuna wakati tunakutana na watu wenye shida ya uchumi ambao wanapanda milima na wanabeba mizigo wakipata changamoto tunajitahidi kujitolea kuwaokoa kama watanzania bila kuangalia gharama pamoja na vitu vingine",Amesema.
Aidha Dkt Jimmy ameongeza kuwa kampuni hiyo haijihusishi tu na mambo ya uokozi bali wameongeza huduma nyingine ikiwemo ya utalii wa Anga.
"Sisi tunajihusisha na wokozi kwa njia ya anga kwa kutumia helkopta pia kwa njia ya ardhini lakini pia tuna huduma ya utalii wa Anga hivyo nitoe rai kwa watalii kuja kwa wingi nchini ili kuja kujionea vivutio vilivyopo" Ameongeza Dk. Jimmy.
kampuni ya Kili MediAir inajishughulisha na usalama wa watalii katika vivutio na kwa sasa imejikita zaidi kanda ya Kaskazini huku wakiwa na malengo ya kufikia vivutio vyote nchini.
REA KUSHIRIKIANA NA NJOMBE KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI ZAIDI YA 13,000
TANZANIA NA UTURUKI KUSHIRIKIANA SEKTA YA MALIASILI NA UTALII
SHEKHE wa mkoa wa Dodoma atunukiwa Udaktari wa Heshima
BALOZI NCHIMBI KUONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA KIBIKI LEO.
RAIS DK.SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI.
SHEKHE wa mkoa wa Dodoma atunukiwa Udaktari wa Heshima
Kuelekea Maadhimisho ya UKIMWI Duniani,Serikali yaeleza ushamiri wa VVU kitaifa kuwa ni asilimia 4.4
BOT YAWATAKA WANANCHI KUKOPA KWENYE TAASISI ZENYE LESENI YA BENKI HIYO.
RAIS DK.SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI.
Kuelekea Maadhimisho ya UKIMWI Duniani,Serikali yaeleza ushamiri wa VVU kitaifa kuwa ni asilimia 4.4