Naibu Waziri ,Wizara ya Maliasili na Utalii, Dunstan Kitandula amesema serikali imejipanga kuendelea kuutangaza utalii ili kuvutial uwekezaji katika sekta ya Utalii kwani sekta hiyo imekuwa na mchango mkubwa kwenye ajira za watanzania pamoja na kuchangia pato la taifa.
Naibu Waziri ,Wizara ya Maliasili na Utalii, Dunstan Kitandula amesema serikali imejipanga kuendelea kuutangaza utalii ili kuvutial uwekezaji katika sekta ya Utalii kwani sekta hiyo imekuwa na mchango mkubwa kwenye ajira za watanzania pamoja na kuchangia pato la taifa.Hayo ameyasema leo Octoba 12,2024 wakati akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam wakati wa mkutano wa Jukwaa la kitaifa la Uwekezaji kupitia Utalii ambalo lilienda sambamba na Onesho la Swahili International Tourism Expo (S!TE) linaloendelea katika ukumbi wa Mlimani City.
Amesema kukua kwa sekta ya utalii ni matokeo na juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kufungua Utalii Kwa kuvitangaza vivutio hapa nchini ambapo imepelekea ongezeko la watalii.
Aidha Naibu Waziri huyo amesema juhudi hizo ndio zimepelekea pia kuwepo kwa mkutano huo uliowakutanisha wadau mbalimbali ikiwemo wawekezaji katika sekta ya Utalii.
“Mkutano huu ni muhimu kwani umehusisha pia watu wanataka kuwekeza katika sekta ya Utalii ikiwemo wa mahoteli na tumekuja hapa kujadiliana fursa zilizopo nchini” amesema.
Amesema mkutano huo wa Uwekezaji katika sekta ya Utalii ambao unafanyika kando ya Onesho la S!TE 2024 ni udhibitisho na hakikisho kwa wawekezaji mbalimbali wa ndani na wa nje kupitia Utalii kuwa Tanzania ni sehemu salama ya kuwekeza ambapo asilimia 25 ya mapato ya fedha za kigeni hapa nchini huchangiwa na sekta ya Utalii.
“Kupitia mkutano huu pia tumewambia watanzania na wawekezaji kuwa kufuatia mazingira mazuri yaliyowekwa na serikali Kwa mabenki hapa nchini sasa wanaweza pia kupata mikopo na kufanya Uwekezaji katika Utalii kupitia mabenki hayo kwani Kwa sasa Kuna sera rafiki za Uwekezaji”amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)Balozi Ephraim Mafuru amesema kuwa Kwa mwaka huu kupitia Onesho la S!TE kama Moja ya mazao ya Utalii limezidi kuvitangaza vyema Tanzania Kimataifa na kupelekea kupata washiriki wengi zaidi kutoka mataifa mbalimbali duniani.
“Kwa mwaka huu washiriki wote walioshiriki Katika Onesho hili kubwa la Kimataifa la Utalii barani Afrika la S!TE 2024 watapata nafasi ya kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii hapa nchini kujionea Yale mazuri tuliyobarikiwa kama Taifa kupitia Utalii”amesema
Aidha Balozi Mafuru amewataka watanzania na wasio watanzania kuendelea kuwekeza katika sekta ya Utalii ambayo imekuwa ni miongoni mwa sekta zenye mafanikio makubwa kutokana na kuzidi kukua mwaka hadi mwaka jambo lililoiweka Tanzania katika ramani nzuri ya Utalii Kimataifa kupitia vivutio vyake.
Naye,Mkurugenzi wa Masoko kutoka Serena Hotel Dar es Salaam Seraphin Lusala amesema bado kuna haja ya Serikali kuendelea kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya hotel nchini kwani kukua kwa utalii na kuongezeka kwa watalii wengi kunahitaji pia kuwepo kwa hoteli nyingi nchini zenye hadhi ya kimataifa.
REA KUSHIRIKIANA NA NJOMBE KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI ZAIDI YA 13,000
TANZANIA NA UTURUKI KUSHIRIKIANA SEKTA YA MALIASILI NA UTALII
SHEKHE wa mkoa wa Dodoma atunukiwa Udaktari wa Heshima
BALOZI NCHIMBI KUONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA KIBIKI LEO.
RAIS DK.SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI.
SHEKHE wa mkoa wa Dodoma atunukiwa Udaktari wa Heshima
Kuelekea Maadhimisho ya UKIMWI Duniani,Serikali yaeleza ushamiri wa VVU kitaifa kuwa ni asilimia 4.4
BOT YAWATAKA WANANCHI KUKOPA KWENYE TAASISI ZENYE LESENI YA BENKI HIYO.
RAIS DK.SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI.
Kuelekea Maadhimisho ya UKIMWI Duniani,Serikali yaeleza ushamiri wa VVU kitaifa kuwa ni asilimia 4.4