WACUBA WAVUTIWA NA HIFADHI YA NGORONGORO | The Dodoma Post
The Dodoma Post Utalii

WACUBA WAVUTIWA NA HIFADHI YA NGORONGORO

Baadhi ya wananchi wa Cuba waliotembelea banda la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika tamasha la kimataifa la Kiswahili wameeleza kufurahishwa kwao kutokana na kupata taarifa mbalimbali zinazohusu vivutio vya Tanzania ikiwemo hifadhi ya Ngorongoro.

Na Hamis Dambaya,Havana
By Na Hamis Dambaya,Havana
11 Nov 2024
WACUBA WAVUTIWA NA HIFADHI YA NGORONGORO

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika banda hilo baadhi ya watu kutoka Cuba waliotembelea banda hilo wamesema wamekuwa wakiiona hifadhi hiyo kupitia picha mbalimbali ikiwemo filamu ya The Royal Tour iliyoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

“Tunavutiwa na juhudi hizi za kuutangaza utalii wenu katika nchi hizi za Karibe,tunaiona Ngorongoro kupitia picha na makala mbalimbali mitandaoni,natamani siku moja kufika Ngorongoro”,alisema Alejendro Alex mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Havana cha jijini Cuba.

Naye Marie Alexndrea kutoka taasisi ya utangazaji wa utalii nchini Cuba alipongeza jitihada kubwa zinazofanywa na watanzania katika kutangaza vivutio vyao vya utalii kwa mataifa mengine ambapo alieleza kuwa kitendo hicho kinasaidia kuonesha ni kwa jinsi gani watu wengi duniani watakavyoweza kuvijua vivutio hivyo.

“Hii inapendeza,tumemuona hata Rais wenu akifanya kazi kubwa ya kutangaza utalii,bila shaka kadri mtakavyotangaza vivutio vyenu katika ukanda huu wa karibe itasaidia pia kuongeza idadi ya watalii katika hifadhi ya Ngorongoro na Tanzania kwa ujumla”,alisema Marie.

Balozi wa Tanzania nchini Cuba  mheshimiwa Humphrey Polepole pembezoni mwa mkutano huo aliipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa uamuzi wake wa  kushiriki tamasha hilo na kusema kuwa yupo mbioni kuandaa mkakati mahsusi katika kuandaa mpango wa kutangaza utalii katika maeneo mbalimbali ya ukanda wa karibe.

Tamasha la Kimataifa la lugha ya Kiswahili lililofanyika nchini Cuba liliwaleta pamoja wadau wa lugha hiyo kutoka mataifa mbalimbali duniani ambapo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro nayo ilishiriki kwa lengo la kutangaza vivutio vilivyopo katika eneo hilo.

TANZANIA NA UTURUKI KUSHIRIKIANA SEKTA YA MALIASILI NA UTALII

TANZANIA NA UTURUKI KUSHIRIKIANA SEKTA YA MALIASILI NA UTALII

TUKIFANYA KAZI KWA PAMOJA TUTAPATA WATALII WA KUTOSHA UKANDA WA KARIBE NA MAENEO JIRANI - BALOZI POLEPOLE

TUKIFANYA KAZI KWA PAMOJA TUTAPATA WATALII WA KUTOSHA UKANDA WA KARIBE NA MAENEO JIRANI - BALOZI POLEPOLE

BAROZI DKT CHANA AFUNGA ONESHO LA S!TE ASIFU MAFANIKIO YALIYOPATIKANA.

BAROZI DKT CHANA AFUNGA ONESHO LA S!TE ASIFU MAFANIKIO YALIYOPATIKANA.

KILI MEDIAIR WABORESHA HUDUMA KUVUTIA UTALII NCHINI.

KILI MEDIAIR WABORESHA HUDUMA KUVUTIA UTALII NCHINI.

KITANDULA; SERIKALI KUTANGAZA UWEKEZAJI KUPITIA SEKTA YA UTALII.

KITANDULA; SERIKALI KUTANGAZA UWEKEZAJI KUPITIA SEKTA YA UTALII.