TBC KURUSHA MICHUANO YA AFCON | The Dodoma Post
The Dodoma Post Michezo

TBC KURUSHA MICHUANO YA AFCON

SHIRIKA la Utangazaji Tanzania (TBC) linatarajia kuonesha na kutangaza michuano ya Mpira ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2024 ambapo michuano hiyo inatarajiwa kufanyika nchini Ivory Coast mwaka huu.

Sophia Kingimali
By Sophia Kingimali
09 Jan 2024
TBC KURUSHA MICHUANO YA AFCON

SHIRIKA la Utangazaji Tanzania (TBC) linatarajia kuonesha na kutangaza michuano ya Mpira ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2024 ambapo michuano hiyo inatarajiwa kufanyika  nchini Ivory Coast   mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo Januari 9 ,Mkurugenzi Mkuu TBC, Dkt Ayub Rioba amesema michuano hiyo itaoneshwa kupitia katika chaneli zote za TBC Tv na Redio ambayo yataanza Januari 13,2023 huku fainali kuchezwa Februari  11 mwaka huu.

Amesema TBC inawatangazaji mahiri wenye vipaji vya uhakika ambao wataweza kutangaza michuano hiyo.
"TBC tumejitahidi  kuboresha maudhui yetu Sasa hivi tupo "FULL HD" visimbuzi vyote lazima TBC iwepo atazame bure mechi hizi sio za kukosa "amesema na kuongeza kuwa 
"Mbali na kuwepo na uchambuzi pia kutakuwa na vipindi vya katikati ambavyo vitakuwa vikifanya uchambuzi wa masuala mbalimbali katika michuano hiyo"amesema Dkt Rioba

Amesema  wakati michuano hiyo ikiendelea kutakuwa na uchambuzi ambao utakuwa ukifanywa na wataalamu ambao ni waandishi wa habari.

Vilevile amesema michuano hiyo imebeba ujumbe mahususi wa kipute mseleleko ambapo amewahakikishia watanzania kuwa mda wote wataweza kuona michuano hiyo hata kama mtu amelipa kisimbuzi au ajalipa.

“Kuanzia enzi hizo ikiwa RTD hadi miaka ya sasa tuna watangazaji mahiri sana, tunaibua vipaji kila mwaka. Mwaka jana tulikuwa na Upete [Nazareth Upete], mnamfahamu, Upete yupo TBC. Tuna watu mahiri kwelikweli, kuna wakati watu wanadhani ubunifu ni ule ubabaishaji, mbwembwe za kibabaishaji, hapana, TBC tuna vijana mahiri kama Muhando ambao ni wabunifu na wanafanya vizuri,” amesema Dkt. Rioba.

Aidha amewaomba wadau kujitokeza kutangaza katika mechi hizo kwani sio za kukosa Ili waweze kuendelea kuziona katika ubora zaidi.

Ndaisaba azidi kumwaga  Fedha katika sekta ya Michezo Wilayani Ngara

Ndaisaba azidi kumwaga Fedha katika sekta ya Michezo Wilayani Ngara

MAKAMU WA RAIS ZANZIBAR ATAKA KANUNI NA MAADILI MICHEZONI ZIWEKWE ILI KUONDOA MITIZAMO HASI.

MAKAMU WA RAIS ZANZIBAR ATAKA KANUNI NA MAADILI MICHEZONI ZIWEKWE ILI KUONDOA MITIZAMO HASI.

BONAZA LA MICHEZO KUFANYIKA JULAI 20-28 PEMBA.

BONAZA LA MICHEZO KUFANYIKA JULAI 20-28 PEMBA.

NDOTO YA LEBRON JAMES YA KUCHEZA NA MWANAE TIMU MOJA YATIMIA BADO YA RONALDO NA MWANAE

NDOTO YA LEBRON JAMES YA KUCHEZA NA MWANAE TIMU MOJA YATIMIA BADO YA RONALDO NA MWANAE