RAIS DK.SAMIA awaongoza watanzania maadhimisho ya siku ya mashujaa. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

RAIS DK.SAMIA awaongoza watanzania maadhimisho ya siku ya mashujaa.

Dodoma.RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan,amewaongoza Viongozi mbalimbli wa Chama na Serikali katika siku ya kumbukumbu ya mashujaa waliopigania uhuru wa Tanzania iliofanyika eneo la Mtumba Jijini Dodoma.

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
25 Jul 2024
RAIS DK.SAMIA awaongoza watanzania maadhimisho ya siku ya mashujaa.

Rais Samia pamoja na mambo mengine ameweza kuweka  Mkuki na Ngao katika mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa hao akiwemo Mkuu wa Majeshi,Brigedia Jenerali Mkunda  ambaye aliweka Sime katika Mnara huo huku Balozi wa Korea Nchini Tanzania akiwawakilisha Mabalozi kwakuweka shada.


Hafla hiyo imehudhuriwa na Viongozi mbalimbli wa Kitaifa  akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya nne DK.Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,,Naibu Waziri Mkuu Doto Biteko na Naibu Spika wa Bunge Mussa Zungu wakiwemo Viongozi wa Dini pamoja na Wanasiasa mbalimbli.

Kwa upande wake Brigedia Jenerali mstaafu Simba Waziri Simba  ni mwakilishi wa wapigania uhuru ambaye alipigaa Vita ya Kagera mnamo Mwaka 1978 hadi 79 ameeleza namna alivyotekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kihakikisha usalama wa nchi na wananchi na kupata Tanzania iliyo salama yenye Amani na utulivu.


Nao baadhi ya Wananchi wametoa  maoni  yao kuhusiana na siku ya Mashujaa wakishauri Serikali kuenzi familia za Mashujaa.

"Kiukweli tunawashukuru mashujaa wetu kwa kuweza kutupigania kwani nchi yetu inaamani  kwasababu yao,kama wananchi tungetamani kuona familia za mashujaa hao zinaangaliwa kwa jicho la tatu na Serikali yetu,lakini pia kwa wale walio hai waenziwe na wapewe kipaumbele popote pale wanapokwenda kwani wao ni tunu ya taifa letu,na sisi tunajivunia wao kwa kuweza kutoa Maisha yao kwa ajili yetu" Amesema John Chibwete mkazi wa mtumba.

EKARI 1,165 za mashamba ya bangi zateketezwa Morogoro

EKARI 1,165 za mashamba ya bangi zateketezwa Morogoro

DCEA YAFANYA OPARESHENI MAALUM YA SIKU TISA MKOANI MOROGORO.

DCEA YAFANYA OPARESHENI MAALUM YA SIKU TISA MKOANI MOROGORO.

FCS KUADHIMISHA WIKI YA AZAKI SEPTEMBA 9,ARUSHA.

FCS KUADHIMISHA WIKI YA AZAKI SEPTEMBA 9,ARUSHA.

JAMII YA KIMASAI IMEANZA KUENDANA NA KASI YA UTANDAWAZI.

JAMII YA KIMASAI IMEANZA KUENDANA NA KASI YA UTANDAWAZI.

TBS YAFUNGUA MASHINDANO YA TUZO ZA UBORA KITAIFA.

TBS YAFUNGUA MASHINDANO YA TUZO ZA UBORA KITAIFA.