JAMII YA KIMASAI IMEANZA KUENDANA NA KASI YA UTANDAWAZI. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

JAMII YA KIMASAI IMEANZA KUENDANA NA KASI YA UTANDAWAZI.

Jamii ya kimasai imeanza kuendana na kasi ya utawazi kwa kuanza kujitokeza kuimba kwenye matamasha, lengo likiwa ni kutangaza utamaduni wao na kujumuika na makabila mengine ambayo yamekuwa yakitumbuiza kwenye matamasha ya kitaifa.

Moreen Rojas (Dodoma)
By Moreen Rojas (Dodoma)
21 Aug 2024
JAMII YA KIMASAI IMEANZA KUENDANA NA KASI YA UTANDAWAZI.

Hayo yameelezwa na MIRHI Kipawa msemaji wa kikundi cha sanaa kilichoundwa na wamasai ishirini na tisa waliokuwa wamejitokeza wakati wa kilele cha maonyesho ya 88 Nzuguni jijini Dodoma kwa ajili ya kuimba nyimbo za kudumisha utamaduni wao.

Aidha amesema malengo yao ni kuleta ufahamu kwa watu juu ya utamaduni zao na matarajio yao ni kushiriki katika matamasha makubwa mbalimbali duniani ili kuhakikisha utamaduni wao haupotei.

"Kiukweli tumekuwa tukiona makabila mbalimbali yakitangaza tamaduni zao na sisi tukaona hebu tuache kuimba huku porini tusogee mjini na sisi tuanze kuchangamana na wengine maana sisi asilimia kubwa tunaogopa sana watu wanaovaa kawaida lakini tukakaa kama kikundi tukasema hapana wenzetu wanatangaza tamaduni zao na serikali inawapa mialiko kwenye matamasha makubwa ambayo mengine Rais anakuwepo kwa nini sisi tushindwe?ndipo tukaamua sasa kuchukua hatua na tunaamini tutafika mbali zaidi ya hapa" Amesema

Aidha kikundi hiki kinatumia sanaa kama njia ya kuendeleza utamaduni wa wamasai na kuonesha uzuri wa desturi zao kwa ulimwengu,kwani jamii ya wamasai ni miongoni mwa makabila machache yanayojulikana ulimwenguni kote kwa sababu ya utamaduni wao wa kipekee na desturi za kuvutia ambapo tamaduni zao zenye mvuto zimekuwa kivutio kikubwa kwa watalii kutoka pande mbalimbali za dunia.

"Tumeanzisha kikundi hichi lakini lazima kiwe na muendelezo kwa watoto wetu kwani tunaamini jamii ikishatufahamu tutapata mialiko kutoka sehemu mbalimbali za nchi,lakini pia tumepanga kuanza kuimba na wake zetu ili na wao waweze kutoka huko vijijini na kuchangamana na wanawake wengine ikiwa ni pamoja na kuchangamkia fursa za kiuchumi" Amesisitiza

Sanjari na hayo Ufugaji, uwindaji, kuimba, na kucheza ni sehemu muhimu ya tamaduni za Wamaasai,ni desturi ambazo zimepita kizazi hadi kizazi, zikiwa zimebeba maana na historia kubwa kwa jamii hii.


Aidha Ufugaji wa mifugo umekuwa nguzo kuu ya maisha yao, huku uwindaji ukiwa njia yao ya jadi ya kujipatia chakula na malighafi kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Hata hivyo, kutokana na kasi ya utandawazi, jamii hii imeanza kuzoea mazingira tofauti na yale ya utamaduni wao wa awali,Wamaasai wengi sasa wanahamia mijini na kushiriki katika shughuli mbalimbali kama vile ulinzi na biashara ndogondogo,haya ni mabadiliko yanayoonyesha jinsi jamii hii inavyojaribu kuendana na ulimwengu wa kisasa bila kuacha kabisa mizizi yao ya kitamaduni.

Kikundi hiki kinaiomba serikali na wadau mbalimbali kuwasaidia ili waweze kuendeleza sanaa yao na kuhakikisha utamaduni wa Kimaasai unadumishwa kwa vizazi vijavyo,maombi yao ni wazi wanahitaji msaada wa kifedha na vifaa ili waweze kufanikisha malengo yao na kulinda urithi huu wa kipekee wa kitamaduni.

EKARI 1,165 za mashamba ya bangi zateketezwa Morogoro

EKARI 1,165 za mashamba ya bangi zateketezwa Morogoro

DCEA YAFANYA OPARESHENI MAALUM YA SIKU TISA MKOANI MOROGORO.

DCEA YAFANYA OPARESHENI MAALUM YA SIKU TISA MKOANI MOROGORO.

FCS KUADHIMISHA WIKI YA AZAKI SEPTEMBA 9,ARUSHA.

FCS KUADHIMISHA WIKI YA AZAKI SEPTEMBA 9,ARUSHA.

TBS YAFUNGUA MASHINDANO YA TUZO ZA UBORA KITAIFA.

TBS YAFUNGUA MASHINDANO YA TUZO ZA UBORA KITAIFA.

FCS YAIOMBA SERIKALI KUWAWEZESHA MAKUNDI MAALUM MIUNDOMBINU YA KIDIGITAL

FCS YAIOMBA SERIKALI KUWAWEZESHA MAKUNDI MAALUM MIUNDOMBINU YA KIDIGITAL