YANGA na Azam Fc zapishana Robo Finali ASFC | The Dodoma Post
The Dodoma Post Michezo

YANGA na Azam Fc zapishana Robo Finali ASFC

Droo ya robo fainali na nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) imefanyika huku timu za Yanga na Azam Fc zikikosana kwenye hatua hii, Shirikisho la Soka Nchini limepanga fainali kufanyika Juni 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Tanzanite, Babati.

kaka mzalendo
By kaka mzalendo
17 Apr 2024
YANGA na Azam Fc zapishana Robo Finali ASFC

Katika droo hiyo, Ihefu iliyoitoa KMC kwa mabao 3-0 itakutana na Mashujaa iliyoiondosha Simba kwa mikwaju ya penalti 6-5, baada ya timu hizo kufungana bao 1-1, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma.

Coastal Union iliyoitoa JKT Tanzania kwa penalti 5-4 itacheza na Geita Gold iliyoifunga Rhino Rangers mabao 2-1, huku Azam FC iliyoitoa Mtibwa Sugar kwa 3-0 itacheza na Namungo iliyoifunga Kagera Sugar kwa penalti 5-3 baada suluhu dakika 90.

Mabingwa watetezi wa michuano hiyo msimu uliopita, Yanga ambao walifuzu kwa kuifunga Dodoma Jiji mabao 2-0, watakutana na Tabora United ambayo iliitoa Singida Fountain Gate kwa mabao 3-0, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kwenye hatua ya nusu fainali, mshindi kati ya Azam FC na Namungo atakutana na atakayepenya kati ya Coastal Union na Geita Gold huku mshindi wa Ihefu na Mashujaa atacheza na atakayefuzu kati ya Yanga na Tabora United.

Michezo ya robo fainali ya michuano hiyo inatarajiwa kuchezwa kati ya Mei 2-4 huku ile ya nusu fainali ikipigwa kati ya Mei 18 hadi 19.

Fainali ya michuano hiyo kwa msimu huu inatarajiwa kupigwa Juni 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Tanzanite, uliopo Babati Manyara.

Tangu kuanza kwa michuano hiyo mwaka 1967 ikifahamika kwa jina la FAT kabla ya 2015 kubadilishwa na kuitwa ASFC, Yanga ndio timu iliyotwaa mara nyingitaji hilo ikifanya hivyo mara saba kuanzia 1967, 1974, 1998, 2001, 2015-2016, 2021-2022 na 2022-2023.

Mbali na Yanga, timu nyingine iliyofika hatua hii iliyochukua ubingwa wa michuano hiyo ni Azam FC iliyofanya hivyo msimu wa 2018-2019 baada ya kuifunga Lipuli ya Iringa kwa bao 1-0, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Ilulu uliopo mjini Lindi.

BONAZA LA MICHEZO KUFANYIKA JULAI 20-28 PEMBA.

BONAZA LA MICHEZO KUFANYIKA JULAI 20-28 PEMBA.

NDOTO YA LEBRON JAMES YA KUCHEZA NA MWANAE TIMU MOJA YATIMIA BADO YA RONALDO NA MWANAE

NDOTO YA LEBRON JAMES YA KUCHEZA NA MWANAE TIMU MOJA YATIMIA BADO YA RONALDO NA MWANAE

TIMU ya mahakama mpira wa miguu yaibuka na ushindi dhidi ya timu ya Bunge.

TIMU ya mahakama mpira wa miguu yaibuka na ushindi dhidi ya timu ya Bunge.

Mavunde awavuta nyota wa Yanga, Ujirani mwema ndondo Cup Dodoma

Mavunde awavuta nyota wa Yanga, Ujirani mwema ndondo Cup Dodoma

WIZARA YA FEDHA YASHIRIKI BONANZA LA PASAKA JIJINI DODOMA

WIZARA YA FEDHA YASHIRIKI BONANZA LA PASAKA JIJINI DODOMA