Mavunde awavuta nyota wa Yanga, Ujirani mwema ndondo Cup Dodoma | The Dodoma Post
The Dodoma Post Michezo

Mavunde awavuta nyota wa Yanga, Ujirani mwema ndondo Cup Dodoma

Mchezaji wa klabu ya yenye maskani yake mitaa ya Jangwani jijini Dar es Salaam Stephan Azizi KI amesema kuwa miongoni mwa vitu anavyofurahia ni kushuhudia michezo ya ndondo hapa Tanzania, kwa sababu vipaji vingi vinapatikana kwenye timu na ligi za mitaani.

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
15 Jun 2024
Mavunde awavuta nyota wa Yanga, Ujirani mwema ndondo Cup Dodoma

KI amesema kuwa imani yake ni kuona shirikissho la  mpira wa miguu Nchini wanaweza kupita ngazi za chini na kuyatumia mashindano ya ndondo cup kupata wachezaji wengi watakao isaidia timu ya Taifa ya Tanzania.

Ameyasema hayo leo Juni 15, 2024 alipofanya ziara mkoani Dodoma na mchezajaj mwenzake Djigui Diarra wakiwa na mwaliko wa Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo hilo Anthony Mavunde kwa lengo la kuvitembelea viwanja na kushuhudia michezo inayochezwa kwenye ligi ya Ujirani mwema Cup inayodhaminiwa na Mbunge huyo.

Mbali na hilo Nyota huyo amempa salamu nyota wa zamani wa timu hiyo Feisal Salum kuwa ajiandae vyema na msimu ujao kwani amefurahishwa na ushindani wa msimu huu.

Wachezaji hao kwa pamoja wamemkabidhi jezi za timu zao za taifa na mipira miwili kutoka kwa Azizi KI ambayo aliyaipata kwa kufunga bao tatu kwa mpigo "Hat trick" kwenye michezo tofauti ya ligi kuu Tanzania bara.

Kwa upande wake Mavunde amesema kuwa kupitia mashindano mbalimbali ikiwemo ya ujirani mwema Ndondo Cup yanayoendelea yamekuwa ni ngazi kwa  vijana wengi wa Dodoma kupata timu ligi kuu soka Tanzania bara na hata nje ya mipaka ya Tanzania.

Mavunde amewataka vijana wa kitanzania kutumia fursa ya michezo kuwa nyenzo moja wapo ya kutengeneza ajira zao.
 
NDOTO YA LEBRON JAMES YA KUCHEZA NA MWANAE TIMU MOJA YATIMIA BADO YA RONALDO NA MWANAE

NDOTO YA LEBRON JAMES YA KUCHEZA NA MWANAE TIMU MOJA YATIMIA BADO YA RONALDO NA MWANAE

TIMU ya mahakama mpira wa miguu yaibuka na ushindi dhidi ya timu ya Bunge.

TIMU ya mahakama mpira wa miguu yaibuka na ushindi dhidi ya timu ya Bunge.

YANGA na Azam Fc zapishana Robo Finali ASFC

YANGA na Azam Fc zapishana Robo Finali ASFC

WIZARA YA FEDHA YASHIRIKI BONANZA LA PASAKA JIJINI DODOMA

WIZARA YA FEDHA YASHIRIKI BONANZA LA PASAKA JIJINI DODOMA

JURGEN KLOOP KUONDOKA LIVERPOOL MWISHO WA MSIMU.

JURGEN KLOOP KUONDOKA LIVERPOOL MWISHO WA MSIMU.