YANGA SC KUTAFUTA MSHAMBULIAJI TISHIO DIRISHA DOGO. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Michezo

YANGA SC KUTAFUTA MSHAMBULIAJI TISHIO DIRISHA DOGO.

Klabu ya Yanga sc licha ya kuwa miongoni mwa klabu zinazofanya vizuri kwasasa kwenye kikosi chao lakini kuelekea dirisha dogo kocha amependekeza usajili wa maeneo kadhaa ili kuboresha kikosi hiko cha wananchi.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
30 Nov 2023
YANGA SC KUTAFUTA MSHAMBULIAJI TISHIO DIRISHA DOGO.

Yanga sc wanahitaji kutafuta natural wingers wenye ubora mkubwa wa kuichezea Yanga sc na kuipambania klabu hiyo kweye michuano mikubwa ndani na nje ya Tanzania.

Lakini pia Yanga sc ipo mawindoni kutafuta mshambuliaji tishio ambaye ataenda kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji katika kikosi hiko cha wananchi.

Ni kweli wanao washambuliaji kadhaa akiwemo Hafiz Konkoni, Kennedy Musonda na Clement Mzize lakini bado klabu inahitaji mshambuliaji hatari zaidi ukizingatia Hafiz tetesi zinaeleza ataachwa katika dirisha dogo la usajili baada ya kuonekana hajakidhi mahitaji ya klabu.

Yapo majina mengi ya wachezaji wanaohusishwa na Yanga sc akiwemo Karamoko Sankara pamoja na Lionel Kateba wote hao wanahusishwa kujiunga na wananchi kwenye dirisha dogo la usajili.
 
YANGA na Azam Fc zapishana Robo Finali ASFC

YANGA na Azam Fc zapishana Robo Finali ASFC

WIZARA YA FEDHA YASHIRIKI BONANZA LA PASAKA JIJINI DODOMA

WIZARA YA FEDHA YASHIRIKI BONANZA LA PASAKA JIJINI DODOMA

JURGEN KLOOP KUONDOKA LIVERPOOL MWISHO WA MSIMU.

JURGEN KLOOP KUONDOKA LIVERPOOL MWISHO WA MSIMU.

ONANA AKIRI KIWANGO CHAKE KUSHUKA ALIPOTUA MAN UNITED

ONANA AKIRI KIWANGO CHAKE KUSHUKA ALIPOTUA MAN UNITED