

Serikali kupitia Wizara ya Nishati imetoa wito kwa wananchi kuachana na matumizi ya nishati isiyo safi ya kupikia na kutumia nishati safi ya kupikia kama vile umeme na gesi ikiwa ni njia pia ya kulinda afya, mazingira na kuimarisha uchumi wa kaya.
*Ni kupitia Kongamano la Wanawake na Fursa za Kiuchumi*
*Wizara ya Nishati yasisitiza matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ili kulinda afya na mazingira*
Mbeya.
Serikali kupitia Wizara ya Nishati imetoa wito kwa wananchi kuachana na matumizi ya nishati isiyo safi ya kupikia na kutumia nishati safi ya kupikia kama vile umeme na gesi ikiwa ni njia pia ya kulinda afya, mazingira na kuimarisha uchumi wa kaya.
Wito huo umetolewa leo na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Nishati Safi ya Kupikia kutoka Wizara ya Nishati, Ndg. Deo Alex katika Kongamano la Wanawake na Wajasiriamali kuhusu fursa za kiuchumi lililofanyika mkoani Mbeya.
Ndg. Deo Alex amesema kuwa mwaka 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alitoa maelekezo ya kuandaliwa kwa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ikiwa ni mwanzo wa safari ya kuelekea katika matumizi ya nishati iliyosafi ya kupikia.
Ameeleza kuwa kufuatia agizo hilo, Wizara ya Nishati iliandaa mkakati huo na kuuzindua rasmi mwaka 2024 ambapo utekelezaji wake umeanza rasmi.
Ameeleza kuwa, kwa mujibu wa mkakati huo, matumizi ya nishati isiyo safi yameonekana kuwa chanzo kikuu cha athari mbalimbali, ikiwemo uharibifu wa mazingira na matatizo ya kiafya kwa watumiaji, miongoni mwa athari za kiafya zilizobainishwa ni pamoja na saratani, homa za mapafu, ujauzito kuharibika na kujifungua watoto kabla ya muda.
Ameeleza kuwa gharama za kumtibu mtu mwenye saratani ni kubwa ukilinganisha na gharama ya ununuzi wa nishati safi ya kupikia kama vile mtungi wa gesi, hivyo wananchi wanahimizwa kuwekeza katika matumizi ya nishati salama kwa ajili ya afya zao na mazingira,
Ndg. Alex amebainisha kuwa mkakati huo umefungua fursa mbalimbali kwa wajasiriamali, ikiwa ni pamoja na kuwa mawakala wa gesi na nishati nyingine mbadala.
Amezitaja aina za nishati safi zinazopendekezwa kuwa ni pamoja na umeme, gesi na mkaa mbadala.
Wanawake mbalimbali waliohudhuria Kongamano hilo kwa nyakati tofauti wameishukuru Wizara ya Nishati kwa kuwapa elimu hiyo ya Nishati Safi ya Kupikia na kutoa wito kuwa iendelee hadi ngazi ya vijiji.
Kongamano hilo limeandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, likiwa na kauli mbiu isemayo “Changamkia Fursa, Jenga Leo na Kesho Yako.”
WATANZANIA WAASWA KUJITAFAKARI KABLA YA KUCHUKUA MIKOPO.
TUKITUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA TUTAOKOA HEKTA 400,000 ZA MISITU ZINAZOTEKETEA KWA MWAKA-MJIOLOJIA NSAJIGWA.
MHANDISI SANGA AONGEZA MWEZI MMOJA KLINIKI YA ARDHI KIVULE KUONGEZA KASI YA UTOAJI HATI
SERIKALI YAFUNGUA MILANGO YA FURSA, KWA WAKULIMA WA MWANI TANGA
WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA KATIKA UTEKELEZAJI WA MAUDHUKUMU YAO HASA KATIKA KIPINDI HIKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025
Serikali Inaendelea Kuimarisha Mazingira Kuwawezesha Vijana Kuanzisha Shughuli Za Uzalishaji Mali.
NGO's zatakiwa Kuwa Mawakala wa mabadiliko chanya katika Jamii.
INEC YAMKABIDHI FOMU ZA UTEUZI MGOMBEA URAIS WA CHAMA CHA NLD DOYO HASSAN DOYO
MGOMBEA KITI CHA URAIS KWA TIKETI YA CHAMA CHA NRA ACHUKUA FOMU TUME
TUME YA TEHAMA NA TAASISI YA KASI KUJA MWAROBAINI WA UDUKUZI MTANDAONI.