NGO's zatakiwa Kuwa Mawakala wa mabadiliko chanya katika Jamii. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

NGO's zatakiwa Kuwa Mawakala wa mabadiliko chanya katika Jamii.

Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yametakiwa kuwa mawakala wa mabadiliko chanya katika jamii katika utekelezaji wa miradi mbalimbali kwenye jamii.

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
12 Aug 2025
NGO's zatakiwa Kuwa Mawakala wa mabadiliko chanya katika Jamii.

Hayo yamesemwa leo Agosti 12, 2025 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt John Jingu wakati anazungumza katika Kongamano la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali linaloendelea kwa siku ya pili katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Dkt. Jingu amesema Mashirika hayo yanawajibu wa kuleta mabadiliko ya kiuchumi, kifikra na maendeleo katika jamii kupita utekelezaji wa miradi yao mbalimbali.

“Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali, yamesajiliwa kisheria kwa lengo la kutoa huduma na elimu katika nyanja tofauti kwa jamii hivyo mtambue kwamba ajenda ya maendeleo endelevu katika Taifa ni pamoja na kuwa mawakala wa mabadiliko chanya katika jamii” amesema Dkt Jungu.

Aidha ameeleza kwamba Mashirika hayo yanapaswa kutekeleza miradi ya uzalishaji ambayo ni endelevu na kuondoa utegemezi kutoka kwa wafadhili, kwa sababu kwa sasa Sera za nchi za Ulaya na Marekani zimebadilika.

Ameongeza kwamba Mashirika yanapaswa kujitafakari vizuri ili kuhakikisha yanakuwa njia mbadala kuendeleza huduma na miradi kwa kutumia rasilimali zinazopatikana katika maeneo yao.

Sanjari na hayo ameongoza na Kufunga moja ya mjadala wa siku ya pili ya kongamano la mwaka la mashirika yasiyo ya Kiserikali(NGOForum 2025)akisisitiza umuhimu wa upatikanaji wa fedha na ubunifu katika kuhakikisha mashirika yasiyo ya Kiserikali yanaendelea kuwa injini ya maendeleo ya jamii.

Mjadala huo ulilenga kujadili mada ya "Upatikanaji wa ufadhili na mikakati ya uendelevu Kwa mashirika yasiyo ya Kiserikali 2020/21- 2024/25 ukichambua mwenendo wa ufadhili nchini Tanzania, changamoto za kupungua kwa misaada kutoka kwa wafadhili wakubwa na mikakati bunifu ya kujitegemea.

Washiriki pia walijadili utekelezaji wa mkakati wa Kitaifa wa uendelevu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali (MKIUMA)2022/23- 2026/27 unaohimiza maandalizi ya mipango thabiti ya uendelevu na kuanzishwa kwa Mfuko wa Ruzuku kusaidia NGOs kupata rasilimali fedha.

MHANDISI SANGA AONGEZA MWEZI MMOJA KLINIKI YA ARDHI KIVULE KUONGEZA KASI YA UTOAJI HATI

MHANDISI SANGA AONGEZA MWEZI MMOJA KLINIKI YA ARDHI KIVULE KUONGEZA KASI YA UTOAJI HATI

Kwa Miaka 4 MSD Imefikisha Vituo 8776 Ikiwa Ni Ongezeko La Vituo 1681.

Kwa Miaka 4 MSD Imefikisha Vituo 8776 Ikiwa Ni Ongezeko La Vituo 1681.

Serikali Yaagiza Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali Kuzingatia Uwazi na Uwajibikaji

Serikali Yaagiza Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali Kuzingatia Uwazi na Uwajibikaji

TUME YA TEHAMA NA TAASISI YA KASI KUJA MWAROBAINI WA UDUKUZI MTANDAONI.

TUME YA TEHAMA NA TAASISI YA KASI KUJA MWAROBAINI WA UDUKUZI MTANDAONI.

TANESCO YAANZA ZOEZI LA UKAGUZI WA MITA KUBAINI UPOTEVU NA WIZI WA UMEME  UNAOFANYWA NA BAADHI YA WATEJA.

TANESCO YAANZA ZOEZI LA UKAGUZI WA MITA KUBAINI UPOTEVU NA WIZI WA UMEME UNAOFANYWA NA BAADHI YA WATEJA.