TUME YA TEHAMA NA TAASISI YA KASI KUJA MWAROBAINI WA UDUKUZI MTANDAONI. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

TUME YA TEHAMA NA TAASISI YA KASI KUJA MWAROBAINI WA UDUKUZI MTANDAONI.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya tehama nchini Dr.Nkundwe Mwasaga amesema serikali wamedhamiria kuongeza wataalamu wa teknolojia ambao watasaidia kuunda mifumo ya kutatua matatizo ya udukuzi na hatari za kimitandao.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
12 Aug 2025
TUME YA TEHAMA NA TAASISI YA KASI KUJA MWAROBAINI WA UDUKUZI MTANDAONI.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya tehama nchini Dr.Nkundwe Mwasaga amesema serikali wamedhamiria kuongeza wataalamu wa teknolojia ambao  watasaidia  kuunda mifumo ya  kutatua matatizo ya udukuzi na hatari za  kimitandao.

Hayo ameyasema 11 Agosti 2025,jijini Dar es salam wakati akifungua mafunzo ya usalama mitandaoni yaliyoandaliwa na ofisi ya TEHAMA kwa kushirikiana na Taasisi inayoshughulika mambo ya usalama wa mitandao ya Korea kusini (KISA) yenye lengo la kujenga ufasini wa wataalamu nchini ili kuendelea kujenga uchumi wa kidigital.

Dr.Mwasaga amesema kuwa mafunzo hayo yatakayofanyika kwa  siku tano yana tafsiri kubwa katika ujenzi wa uchumi wa kidigitali ambao utasaidia kuongeza wawekezaji na kipato kwa wananchi wa kawaida. 

Dkt.Nkundwe amesisitiza kuwa ili mtu awe na  Imani ya kutumia mifumo hiyo ya akiliunde ni lazima kuwe na mifumo ya usalama wa taarifa binafsi,kulinda faragha za watu na kumlinda mlaji wa mifumo ya kidigitali .

"Kuna jambo jipya limejitokeza sasa hivi na limeanza kuonekana lina umuhimu mkubwa yaani sasa hivi kupitia mitandao watu sio tu wanaweza wakaingilia mifumo lakini pia wanaweza kumbadilisha mtu fikra zake na kufikiria jinsi wanavyotaka wao huo unaitwa Udukuzi wa fikra na baadhi ya nchi wamesema ni hatari kwa jamii kwa hiyo tumeona ni vizuri wataalamu wetu wakajifunza ujanja gani unatumika na namna gani unavyofanywa",alisema. Dokta

Dkt.Nkundwe ametoa shukrani kwa KISA kwa kukubali kufanya mafunzo hayo nchini  ambayo imepata fursa ya kuhudhuriwa na wataalamu kutoka taasisi 33 ambapo watapata ujuzi na kuwasaidia watu wengine.

"Mbinu za watu wabaya mitandaoni zinabadilika kila siku hivyo kupata elimu kutoka kwa nchi nyingine itasaidia kujifunza mambo mapya na Wakorea ni wataalam na watafanya mifumo yetu iwe vizuri zaidi kwa hiyo ni njia ambayo serikali imenuia kujenga uchumi madhubuti wa kidigitali".alisema Nkundwe

Kwa upande wake mtafiti kutoka taasisi ya KISA, Minyoung Kim amesema kuna umuhimu wa kutengeneza ushirikiano wa pamoja ili kuzishinda changamoto za mifumo ya kimitandao.

"katika nchi yetu Korea Kusini  tumedhamiria kuwa na wataalamu 10,000 wenye uwezo wa kulinda mambo ya mitandao ya kidigitali".Ameongeza Minyoung. 

Naye,mtaalamu wa mawasiliano ya teknolojia ya habari katika kitengo cha ulinzi wa tehama Venance Mwachabike amesema mafunzo hayo yatamsaidia kuboresha kazi zake katika kitengo anachofanyia kazi na kuongeza ufanisi lakini pia kujifunza mbinu mpya za kiteknolojia.

MHANDISI SANGA AONGEZA MWEZI MMOJA KLINIKI YA ARDHI KIVULE KUONGEZA KASI YA UTOAJI HATI

MHANDISI SANGA AONGEZA MWEZI MMOJA KLINIKI YA ARDHI KIVULE KUONGEZA KASI YA UTOAJI HATI

Kwa Miaka 4 MSD Imefikisha Vituo 8776 Ikiwa Ni Ongezeko La Vituo 1681.

Kwa Miaka 4 MSD Imefikisha Vituo 8776 Ikiwa Ni Ongezeko La Vituo 1681.

Serikali Yaagiza Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali Kuzingatia Uwazi na Uwajibikaji

Serikali Yaagiza Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali Kuzingatia Uwazi na Uwajibikaji

NGO's zatakiwa Kuwa Mawakala wa mabadiliko chanya katika Jamii.

NGO's zatakiwa Kuwa Mawakala wa mabadiliko chanya katika Jamii.

TANESCO YAANZA ZOEZI LA UKAGUZI WA MITA KUBAINI UPOTEVU NA WIZI WA UMEME  UNAOFANYWA NA BAADHI YA WATEJA.

TANESCO YAANZA ZOEZI LA UKAGUZI WA MITA KUBAINI UPOTEVU NA WIZI WA UMEME UNAOFANYWA NA BAADHI YA WATEJA.