

Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya mikopo ya SELF Microfinance Santieli Yona amewataka wananchi kabla ya kukopa wafanye tathmini ya kina kuhusu matumizi ya fedha wanazozichukua kwa ajili ya shughuli zao kwani wakijipanga vema watakuwa na uhuru,kujiamini pamoja na kuweza kurejesha mikopo yao bila matatizo yeyote.
Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya mikopo ya SELF Microfinance Santieli Yona amewataka wananchi kabla ya kukopa wafanye tathmini ya kina kuhusu matumizi ya fedha wanazozichukua kwa ajili ya shughuli zao kwani wakijipanga vema watakuwa na uhuru,kujiamini pamoja na kuweza kurejesha mikopo yao bila matatizo yeyote.
Akizungumza leo 15,agosti 2025 kwenye kikao na jukwaa la Wahariri na Waandishi wa Habari Kilichoandaliwa na ofisi ya msajili wa Hazina jijini Dar es salaam Santieli amebainisha kuwa kuna changamoto ya wananchi wengi kukosa elimu ya fedha na kushindwa kufanya tathmini kabla ya kukopa ambapo husababisha baadhi watu wawe na hulka ya kutojali urejeshaji wa mikopo waliyoichukua.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa suluhuhisho ya kuzishinda changamoto za fikra potofu za ukopaji ni muhimu kuweka mkazo katika kutoa elimu kwa raia ili kuimarisha huduma za fedha kwa kuwa elimu hiyo imewafikia wachache.
Aidha bi Santieli alifafanua mafanikio ya SELF ikiwa ni kutoa mikopo kwa ajili ya nishati safi ya kupikia ili kutekeleza agenda ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na manufaa ya mikopo hiyo itasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi.
"Moja ya mafanikio tuliyoyapata ni kutengeneza ajira,sisi tunatoa mikopo kwa taasisi zinazokopesha na wajasiriamali sasa wanapopewa fedha, wanajiajiri na kutoa fursa kwa watu wengine na katika kipindi hiki tumeweza kutoa ajira zipatazo 183,000, jambo ambalo ni mafanikio makubwa kwa taifa, kwani si serikali pekee inayoweza kutoa ajira, bali kila mmoja anaweza kujiajiri na kujikimu.,” alieleza
Hata hivyo aliongeza kuwa Microfinance yao inatoa elimu ya fedha mara kwa mara kupitia majukwaa mbalimbali, ikiwemo maonesho ya Nanenane, Sabasaba, makongamano na kupitia vyombo vya habari lengo ni kuhakikisha wananchi wengi wanafikiwa na kusaidiwa kifikra kuhusu mikopo.
"Tuna dhamira ya kufika kila mkoa na tunawaalika Watanzania waje kushiriki na sisi kwa sababu hatuwezi kwenda peke yetu ila na wao pia huwa tunafuatilia na kuona kama huduma zetu zinabadilisha maisha ya wanufaika na niwajuze kila baada ya muda tunapenda kujua walikuwa wapi na mikopo imenufaishaje na wapo viwango gani sasa ,” alisema Santieli
Taasis hiyo ya kifedha imelenga kuongeza mtaji wa mikopo hadi Tsh billion 300 ndani ya miaka mitano ijayo na itawafikia zaidi ya wanufaika 20000 moja kwa moja pia imeweza kujenga uwezo kwa taasisi 549 kwa kutoa ushauri mbalimbali.
TUKITUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA TUTAOKOA HEKTA 400,000 ZA MISITU ZINAZOTEKETEA KWA MWAKA-MJIOLOJIA NSAJIGWA.
MHANDISI SANGA AONGEZA MWEZI MMOJA KLINIKI YA ARDHI KIVULE KUONGEZA KASI YA UTOAJI HATI
SERIKALI YAFUNGUA MILANGO YA FURSA, KWA WAKULIMA WA MWANI TANGA
WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA KATIKA UTEKELEZAJI WA MAUDHUKUMU YAO HASA KATIKA KIPINDI HIKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025
ELIMU YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA YAWAFIKIA WANAWAKE MKOANI MBEYA
Serikali Inaendelea Kuimarisha Mazingira Kuwawezesha Vijana Kuanzisha Shughuli Za Uzalishaji Mali.
NGO's zatakiwa Kuwa Mawakala wa mabadiliko chanya katika Jamii.
INEC YAMKABIDHI FOMU ZA UTEUZI MGOMBEA URAIS WA CHAMA CHA NLD DOYO HASSAN DOYO
MGOMBEA KITI CHA URAIS KWA TIKETI YA CHAMA CHA NRA ACHUKUA FOMU TUME
KADEGE WA CHAMA CHA UPDP ACHUKUA FOMU ZA URAIS