

Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) inashiriki Maonesho ya NaneNane Kitaifa yanaendelea katika Viwanja vya Maonesho vya Nzuguni Jijini Dodoma kutoa elimu kuhusu ununuzi wa Umma kwa wazabuni, hususan elimu kuhusu Moduli ya kupokea na kushughulikia Malalamiko na Rufaa katika mfumo wa NeST
Akiongea kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma, Bw. Nelson Kessy amesema PPAA imejipanga kutoa elimu kwa wadau wa ununuzi wa umma na wananchi kwa ujumla ili kutoa wigo mpana zaidi kwa wazabuni na wadau wa sekta hiyo.
Pamoja na mambo mengine, Bw. Kessy amewasihi wadau wa ununuzi na wananchi kwa ujumla kutembelea Banda la PPAA linalopatikana ndani ya Banda la Wizara ya Fedha katika viwanja vya Nzuguni, Dodoma.
Maonesho haya kwa mwaka 2025 yamebeba kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025”. Maonesho ya NaneNane Kitaifa yalifunguliwa rasmi tarehe 1 Agosti, 2025 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mapango. Maonesho hayo yalianza tarehe 1 hadi 8 Agosti 2025.
DKT.SAMIA,DKT.NCHIMBI KUCHUKUA FOMU YA URAIS KESHO AGOSTI 9,2025.
TUME YATANGAZA RATIBA YA VYAMA KUCHUKUA FOMU ZA WAGOMBEA WA URAIS
TANESCO YAANZA ZOEZI LA UKAGUZI WA MITA KUBAINI UPOTEVU NA WIZI WA UMEME UNAOFANYWA NA BAADHI YA WATEJA.
CUF KUPITISHA WAGOMBEA URAIS AGOSTI 9 MAJINA YATAJWA.
PBPA YAELEZEA MAFANIKIO YAKE YA MIAKA MINNE KATIKA UONGOZI WA RAIS DK.SAMIA.
VIONGOZI WA DINI WAASWA KUSHUGHULIKIA MIGOGORO YAO YA NDANI PASIPO KUZUA TAHARUKI ILI KULINDA AMANI YA NCHI.
Coop Bank Imejipanga Kutoa Huduma Maalum kwa Washiriki wa Maonesho ya NaneNane.
SENYAMULE AIPONGEZA DIB UTOAJI WA ELIMU KWENYE MAONESHO NANENANE.
CUF KUPITISHA WAGOMBEA URAIS AGOSTI 9 MAJINA YATAJWA.
WAANDISHI WA HABARI WAHIMIZWA KUHAMASISHA USHIRIKI WA WANANCHI KUPIGA KURA