Serikali Yaagiza Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali Kuzingatia Uwazi na Uwajibikaji | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

Serikali Yaagiza Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali Kuzingatia Uwazi na Uwajibikaji

Serikali imeyatakia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) kote nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi ya uwazi, uwajibikaji na uzalendo, ili kuimarisha utawala bora na kuongeza mchango wao katika maendeleo ya Taifa

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
13 Aug 2025
Serikali Yaagiza Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali Kuzingatia Uwazi na Uwajibikaji

Hayo yameelezwa Agosti 13, 2025 na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe Dkt. Dorothy Gwajima wakati alipomwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Philip Isdori Mpango katika kilele cha Kongamano la Mwaka la NGOs jijini Dodoma

Gwajima amesisitiza kuwa mashirika hayo lazima yaendelee kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa miradi ya kijamii na kiuchumi sambamba na vipaumbele vya kitaifa.

Aidha, amezindua Mwongozo wa Uzingatiaji wa Uwazi wa Masuala ya Kifedha na Ushirikiano kati ya Serikali na Asasi Zisizo za Serikali, pamoja na Kamati ya Kitaifa ya Mchakato wa Uanzishwaji wa Mfuko wa Pamoja wa Ruzuku kwa NGOs (NBF).

Amesema mfuko huo utasaidia mashirika kupata ufadhili bila masharti magumu na kuongeza uhimilivu wa miradi yao.

Pia amewataka viongozi wa NGOs kutumia fursa ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano kuendeleza mchango wao katika sekta za afya, elimu, kilimo, maji, mazingira na uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2025, NGOs zilizopewa vibali vya kutoa elimu ya mpiga kura na uangalizi wa uchaguzi zimetakiwa kufanya kazi kwa weledi na kuhamasisha wananchi kushiriki kwa amani na utulivu.

Katika kongamano hilo, Serikali ilipongeza mashirika kwa mchango wao katika kutoa ajira, kuboresha huduma za kijamii na kushirikiana katika mchakato wa maboresho ya sheria, sera na miongozo ya sekta hiyo.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Hajjat Mwantumu Mahiza, amewaomba wanasekta hiyo kuendeleza mashirikiano kwaajili ya faida ya taifa na kizazi kijacho.

"Ndugu zangu hii nchi tinaijenga sote na kila mmoja ana dhamira njema kwa nchi yake, ni wasihi sana kila mmoja kwenye nafasi aliyopo kila unalolifanya tanguliza maslahi ya nchi kwanza, Tanzania hii ni yetu sote na inatutegemea na tunahitaji kuijenga Tanzania iwe mahali salama na penye neema nyingi kuliko tulivyoikuta sisi,"amesema.

Katika kongamano hilo, Serikali ilipongeza mashirika kwa mchango wao katika kutoa ajira, kuboresha huduma za kijamii na kushirikiana katika mchakato wa maboresho ya sheria, sera na miongozo ya sekta hiyo.

MHANDISI SANGA AONGEZA MWEZI MMOJA KLINIKI YA ARDHI KIVULE KUONGEZA KASI YA UTOAJI HATI

MHANDISI SANGA AONGEZA MWEZI MMOJA KLINIKI YA ARDHI KIVULE KUONGEZA KASI YA UTOAJI HATI

Kwa Miaka 4 MSD Imefikisha Vituo 8776 Ikiwa Ni Ongezeko La Vituo 1681.

Kwa Miaka 4 MSD Imefikisha Vituo 8776 Ikiwa Ni Ongezeko La Vituo 1681.

NGO's zatakiwa Kuwa Mawakala wa mabadiliko chanya katika Jamii.

NGO's zatakiwa Kuwa Mawakala wa mabadiliko chanya katika Jamii.

TUME YA TEHAMA NA TAASISI YA KASI KUJA MWAROBAINI WA UDUKUZI MTANDAONI.

TUME YA TEHAMA NA TAASISI YA KASI KUJA MWAROBAINI WA UDUKUZI MTANDAONI.

TANESCO YAANZA ZOEZI LA UKAGUZI WA MITA KUBAINI UPOTEVU NA WIZI WA UMEME  UNAOFANYWA NA BAADHI YA WATEJA.

TANESCO YAANZA ZOEZI LA UKAGUZI WA MITA KUBAINI UPOTEVU NA WIZI WA UMEME UNAOFANYWA NA BAADHI YA WATEJA.