UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA | The Dodoma Post
The Dodoma Post Nishati

UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA

Ujenzi wa Mradi wa Bwawa la kufua umeme kwa maji kupitia mto Malagarasi (MW49) umefikia hatua muhimu, kwa kuweza kuchepusha maji ya kwenye mto (kutengeneza njia ya maji) ili kuruhusu ujenzi wa Tuta kuu,litakalotumika katika kufua umeme.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
13 Aug 2025
UJENZI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MTO MALAGARASI , WAPIGA HATUA MPYA

*Mto wachepushwa ili kujenga tuta la kufulia Umeme

*Kasi yapamba moto kukamilisha Mradi

Ujenzi wa Mradi wa Bwawa la kufua umeme kwa maji kupitia mto Malagarasi (MW49) umefikia hatua muhimu, kwa kuweza kuchepusha maji ya kwenye mto (kutengeneza njia ya maji) ili kuruhusu ujenzi wa Tuta kuu,litakalotumika katika kufua umeme.

Akizungumza katika hafla fupi ya uchepushaji maji, Agosti 13,2025 Meneja wa Mradi Mha. Saidi Kimbanga amesema kuwa hatua hiyo ni muhimu katika utekelezaji wa mradi huo ambao kwa sasa ujenzi wa mradi umefikia kwa Asilimia 10, na unatarajia kukamilika mwanzoni kwa mwaka 2027.

“Ujenzi wa mradi unaenda kwa kasi sana, uchepushaji maji ulitakiwa kufanyika tarehe 27, mwezi huu, lakini tumefanikisha zoezi hili leo, siku zaidi ya kumi nyuma, hivyo tunatarajia hata mradi utakamilika mapema zaidi” alisema Mha. Saidi

Akizungumzia umuhimu wa uchepushaji maji, Mha. Saidi amesema kuwa maana nzima ya ujenzi wa Bwawa la kufua umeme unahitaji kuweza kudhibiti maji ili yaweze kupita katika njia maalum, na kuweza kufua umeme, hivyo hatua hii ni muhimu ilikuweza kuzalisha umeme uliokusudiwa kupatikana.

Naye Mkurugenzi wa Kanda ya Magharibi Mha. Andrew Swai akizungumza amesema kuwa hatua hiyo muhimu imetokana na Mchango mkubwa wa Serikali,  Wizara ya Nishati na TANESCO kwa  kuweza kuhakikisha na kumsimamia Mkandarasi (Dongfang Electric International Corporation kutoka China) ili kukamilisha kazi hiyo na ameahidi kuwa Mradi wa Malagarasi utakamilika na TANESCO haitalala, itashirikiana na Mkandarasi katika kuhakikisha mradi una kamilika kwa wakati.

Kwa upande mwingine, Meneja wa Mkoa wa Kigoma Mha. Julius Sabu, amesema kuwa Kukamilika kwa Mradi wa Malagarasi kutaongeza umeme hata katika Mkoa wa Kigoma na kusema kuwa Kigoma sasa itakua na umeme wa uhakika, na kuwataka wawekezaji kuanza kuwekeza katika Mkoa wa Kigoma.

Ujenzi wa Mradi wa Malagarasi wa Megawati 49.5 unatekeleza na Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania, ambapo ulianza Aprili 10,2024 na unatarajia kukamilika Oktoba 10,2027, gharama za Mradi za ujenzi wa Bwawa ikiwa ni Shilingi Bilioni 300 za Kitanzania.

TUKITUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA TUTAOKOA HEKTA 400,000 ZA MISITU ZINAZOTEKETEA KWA MWAKA-MJIOLOJIA NSAJIGWA.

TUKITUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA TUTAOKOA HEKTA 400,000 ZA MISITU ZINAZOTEKETEA KWA MWAKA-MJIOLOJIA NSAJIGWA.

ELIMU YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA YAWAFIKIA WANAWAKE MKOANI MBEYA

ELIMU YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA YAWAFIKIA WANAWAKE MKOANI MBEYA

DKT. BITEKO AZINDUA PROGRAMU YA UGAWAJI MAJIKO YA UMEME KWA BEI YA RUZUKU KWA WAFANYAKAZI WA TANESCO.

DKT. BITEKO AZINDUA PROGRAMU YA UGAWAJI MAJIKO YA UMEME KWA BEI YA RUZUKU KWA WAFANYAKAZI WA TANESCO.

REA YAZIDI KUHAMASISHA NISHATI SAFI, YATOA BILIONI 4.37 KWA JESHI LA KUJENGA TAIFA.

REA YAZIDI KUHAMASISHA NISHATI SAFI, YATOA BILIONI 4.37 KWA JESHI LA KUJENGA TAIFA.

PBPA YAELEZEA MAFANIKIO YAKE YA MIAKA MINNE KATIKA UONGOZI WA RAIS DK.SAMIA.

PBPA YAELEZEA MAFANIKIO YAKE YA MIAKA MINNE KATIKA UONGOZI WA RAIS DK.SAMIA.