TANESCO YAZINDUA MFUMO WA UPOKEAJI TAARIFA KWA SIRI WATAKA WANANCHI KUUTUMIA ILI KURIPOTI VITENDO VYA UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU YA SHIRIKA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

TANESCO YAZINDUA MFUMO WA UPOKEAJI TAARIFA KWA SIRI WATAKA WANANCHI KUUTUMIA ILI KURIPOTI VITENDO VYA UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU YA SHIRIKA.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limezindua mfumo mpya wa kupokea taarifa za siri ufahamikao kama Whistle blower wenye lengo kudhibiti vitendo vya uhalifu, rushwa, na uharibifu wa miundombinu ya umeme lakini pia utakaoweza kutumika na wafanyakazi wa shirika kuripoti matendo ya ukatili wa kijinsia wanayokutana nayo kwenye utendaji wao.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
04 Aug 2025

TANESCO pia inaendelea na kampeni ya kitaifa ya “Lipa Deni Tukuhudumie”, inayolenga kuhakikisha huduma ya umeme inapatikana kwa wakati kwa wananchi wote.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 4,2025 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mfumo huo, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Irene Gowele, amesema mfumo huo wa Whistleblower Portal ni hatua ya kimageuzi katika utendaji wa shirika hilo.

“Kwa muda mrefu tumekuwa tukikumbwa na changamoto kama vile wizi wa miundombinu ya umeme na vitendo vya rushwa kutoka kwa baadhi ya watumishi. Mfumo huu mpya utarahisisha upokeaji wa taarifa na kulinda usalama wa mtoa taarifa,” amesema Gowele.

Ameeleza kuwa taarifa zitapokelewa na kushughulikiwa kwa usiri mkubwa, huku mtoa taarifa akielekezwa hatua stahiki kwa mujibu wa taratibu.

Ameongeza kuwa wananchi wataweza kutumia njia mbili kuwasilisha taarifa zao  kupitia tovuti ya shirika ambayo ni www.tanesco.co.tz kwa kubonyeza kiungo cha Whistleblower Portal na kujaza fomu salama na kupiga simu bila malipo kupitia namba 180, kisha kubonyeza namba 2 kuzungumza na watoa huduma wa shirika

Aidha, shirika limewahimiza wananchi kote nchini kushiriki kikamilifu katika matumizi ya mfumo huo ili kusaidia kulinda rasilimali za shirika na Taifa kwa ujumla.

TANESCO YAANZA ZOEZI LA UKAGUZI WA MITA KUBAINI UPOTEVU NA WIZI WA UMEME  UNAOFANYWA NA BAADHI YA WATEJA.

TANESCO YAANZA ZOEZI LA UKAGUZI WA MITA KUBAINI UPOTEVU NA WIZI WA UMEME UNAOFANYWA NA BAADHI YA WATEJA.

TICEZA Kuwapa Watanzania Maeneo Bure Kujenga Viwanda

TICEZA Kuwapa Watanzania Maeneo Bure Kujenga Viwanda

SERIKALI  KUTOA  BILIONI 277 KILA MWAKA KUGHARAMIA HUDUMA ZA VVU NA UKIMWI.

SERIKALI KUTOA BILIONI 277 KILA MWAKA KUGHARAMIA HUDUMA ZA VVU NA UKIMWI.

VIONGOZI WA DINI WAASWA KUSHUGHULIKIA MIGOGORO YAO YA NDANI PASIPO KUZUA TAHARUKI ILI KULINDA AMANI YA NCHI.

VIONGOZI WA DINI WAASWA KUSHUGHULIKIA MIGOGORO YAO YA NDANI PASIPO KUZUA TAHARUKI ILI KULINDA AMANI YA NCHI.

ELAF YAITAKA SERIKALI KUUNDA CHOMBO MAALUMU CHA KUSHUGHULIKIA UPOTEVU WA WATU NCHINI.

ELAF YAITAKA SERIKALI KUUNDA CHOMBO MAALUMU CHA KUSHUGHULIKIA UPOTEVU WA WATU NCHINI.